Wa-Tanganyika tuamke, tulinde haki zetu

Wa-Tanganyika tuamke, tulinde haki zetu

Tatizo kubwa ni umma kukosa uwakilishi bungeni kufuatia wizi wa Kura mnamo 28/10/2020.
Kwa sasa HAKUNA anayeweza kuhoji huu wizi na unyang'anyi kule bungeni.
Ndugai alijaribu kidogo yakamkuta!
Tanganyika imegeuzwa kinyemela kuwa Shamba la Bibi. Wanavuna mwanzo mwisho!

Tatizo kubwa naona zaidi kwa wananchi kuliko hata wana siasa.

Wamelala utafikiri nchi iko sawa, sijui tumerogwa na nani? Na inawezekana aliyeturoga ameshakufa
 
Waafrika tuna matatizo makubwa sana.

Marekani ni Muungano wa nchi 52 ila husikii kelele za aina yeyote.

Sisi hapa nchi mbili tu kila siku yanaibuka mapya.

Marekani Muungano wao uko well elaborated na nchi mbalimbali zilijiunga kwa hiyari yao wenyewe, pia mgawanyo wa rasilimali na mamlaka unategemea zaidi uwiano wa watu katika jimbo husika
 
Znz wanajengewa vituo vya afya kila umbali wa 5 km..
Mbona kwa Bara hakuna hilo?!!!

Lakini pia wanatumia kofia ya Muungano kunufaika na mengi, hata ulipaji wa hiyo mikopo tutalipa sisi kama wabara, maana hata deni la Tanesco tu liliwashinda
 
Mkuu, wamepewa fedha kwa ajili ya miradi ya maji tu. Ni maji tu ya kuoga, kufulia, kupikia na kunywa.
Wala hata sio hela ya bia na bata.

Au kuna ubaya mkuu ?
Maana naona msingi wa hoja yako umeanzia kwenye mgawo wa huo mkopo wa "mabeberu".
Ingekuwa hela ya bia, kungekuwa na uprising siyo!!😂😅
 
Ok twende na Logic yako.

Mtanzania mwenye asili ya upande wa bara anafaidika vipi na huu muungano?

Kipi hasa anakipa akienda Zanzibar ambacho waZanzibari wakija bara wanapata??

Tusaidie hapo Mtaalam
Swali lako halina tofauti na kuuliza Mmakonde wa Mtwara anafaidika nini na Mkoa wa Kilimanjaro. Faida ni nyingi na inategemea raia anahitaji kitu gani. Mfano, mimi ni wa Kilimanjaro, ila siwezi kuishi Kilimanjaro japo mimi ni mwenyeji kule, isipokuwa, hapa nilipo ndipo ninapata faida kulingana na mahitaji yangu.

Kwa hiyo, mtu wa Bara na mtu wa Zanzibar, wana faida kwa pande zote mbili katika namna moja au nyingine.
 
Umesema “muungano wa nchi 52 vs Muungano wa nchi mbili”

Muungano hauna muundo?

Ukilinganisha idadi bila ya kuhusisha muundo uliopelekea hiyo idadi ya kwenye muungano, ni ukosefu wa hoja yoyote kwenye bandiko lako.
Hapana

Nimezungumzia idadi na kuachana na muundo kwakua inashangaza sana nchi nyingi zimefanikiwa kuishi pamoja kwa amani na uelewano mkubwa kuliko nchi chache jambo ambalo linaongeza viashiria vya matatizo makubwa kwa hao wachache.
 
Swali lako halina tofauti na kuuliza Mmakonde wa Mtwara anafaidika nini na Mkoa wa Kilimanjaro. Faida ni nyingi na inategemea raia anahitaji kitu gani. Mfano, mimi ni wa Kilimanjaro, ila siwezi kuishi Kilimanjaro japo mimi ni mwenyeji kule, isipokuwa, hapa nilipo ndipo ninapata faida kulingana na mahitaji yangu.

Kwa hiyo, mtu wa Bara na mtu wa Zanzibar, wana faida kwa pande zote mbili katika namna moja au nyingine.

Acha kupotosha, hivyo ni vitu viwili tofauti.

Wewe wa Mtwara unaweza kununua eneo Kilimanjaro, ukajenga nyumba aunukaamua kuwekeza kwenye Kilimo.

Je? Unaweza kufanya hivi Zanzibar?

Wewe wa Kilimanjaro unaeeza kugombea nafasi yoyote ya uongozi Mtwara na ukachaguliwa, Je unaweza kufanya hivi Zanzibar?

FYI! Mzanzibari ana haki zote kama ulizonazo wewe, ila Mtanganyika hana chochote!

So be informed
 
Kwa kweli mgawanyo wa rasilimali kama ndio upo kwa % hizo sio sawa kabisa. Kigezo kikuu ambacho walipaswa watumie ni ratio ya idadi ya watu na ukubwa wa eneo. Kwa sababu ukitaka uigawanye Tanganyika kwa ukubwa wa eneo la Zenj unaweza kutoa nchi nyingi tu za size hiyo. Ingawa mtoa mada ukitaka iwe kwa usawa, inabidi iwe 50 - 50
 
Una uhakika Watanganyika hatupo kweli? Ccm acheni kucheza na akili zetu bhana! Sasa huo Muungano wa 26/04/1964 ulikuwa ni kati ya nani na nani?

Siyo kati ya Tanganyika na Zanzibar! Sasa kwa nini leo mtuite watu wa Tanzania Bara? Nakuhakikishia Tanganyika itadumu milele. Na binafsi naamini ipo siku tu Tangaanyika itamuondoa huyu kupe anayeitwa Zanzibar kwenye ngozi yake.
Rejea maamuzi ya Mahakama ya Rufaa ya Tanzania kwenye kesi ya uhaini wa kujaribu kupindua Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iliyokuwa inawakabili akina Machano na Wenzake.

Katika uamuzi ule, pamoja na mambo mengine, Mahakama ya Rufaa ilitoa hukumu kwamba nchi/dola za Tanganyika na Zanzibar zilifariki tarehe 26 April, 1964 na kuzaliwa Tanzania nchi huru inayotambulika kimataifa wit full sovereignty.

Hivyo basi, Zanzibar ni nchi isiyokuwa dola kamili, na kwa maana hiyo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar haiwezi kupinduliwa, na hivyo akina Machano hawakuwa na hatia kwa sababu Mapinduzi hufanyika dhidi ya dola kamili inayotambulika kimataifa na yenye Mamlaka kamili.

Kwa Tafsiri ya Kisheria, Tanganyika haipo, ila eneo lililoitwa dola la Tanganyika kabla ya April 26, 1964, ndiyo sasa Tanzania Bara na Watanganyika ndiyo Watanzania Bara; na eneo lililoitwa Zanzibar (dola kamili) ndiyo sasa ilipo nchi ya Zanzibar (ambayo siyo dola kamili).

Kimsingi, Tanganyika ilipoteza uhuru wake, na Zanzibar pia ilipoteza uhuru wake na hatimaye ikapatikana Tanzania.
 
Acha kupotosha, hivyo ni vitu viwili tofauti.

Wewe wa Mtwara unaweza kununua eneo Kilimanjaro, ukajenga nyumba aunukaamua kuwekeza kwenye Kilimo.

Je? Unaweza kufanya hivi Zanzibar?

Wewe wa Kilimanjaro unaeeza kugombea nafasi yoyote ya uongozi Mtwara na ukachaguliwa, Je unaweza kufanya hivi Zanzibar?

FYI! Mzanzibari ana haki zote kama ulizonazo wewe, ila Mtanganyika hana chochote!

So be informed
Mimi binafsi, hata Kigamboni pale siwezi kumiliki ardhi japo ninaruhusiwa. Sababu ni kwamba, kusafiri majini sipendi na kuishi karibu na bahari sipendi pia.

Halafu, ishu ya kumiliki ardhi ni rahisi sana. Ni wewe tu hujataka. Hata Tanzania Bara raia wa kigeni anaweza akamiliki ardhi kupitia uwekezaji na mianya mingine ya kisheria. Ni vile tu watu hamfatalii.

Labda, tuache hilo, twende huku huku Bara. Pale Kilimanjaro, ni ngumu sana mtu wa nje ya Mkoa ule kumiliki ardhi wakati sheria inaruhusu. Kwa ufahamu wangu, hapa Tanzania, hakuna eneo gumu kununua na kumiliki ardhi kama Kilimanjaro.

Kwa hiyo, kama Zanzibar ni ngumu kumiliki ardhi kwa sababu za kisheria, je ni vipi Kilimanjaro ambapo sheria inaruhusu ila ugumu upo?

Hata Mzanzibari akienda Moshi atapata tabu kumiliki ardhi.
 
Rejea maamuzi ya Mahakama ya Rufaa ya Tanzania kwenye kesi ya uhaini wa kujaribu kupindua Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iliyokuwa inawakabili akina Machano na Wenzake.

Katika uamuzi ule, pamoja na mambo mengine, Mahakama ya Rufaa ilitoa hukumu kwamba nchi/dola za Tanganyika na Zanzibar zilifariki tarehe 26 April, 1964 na kuzaliwa Tanzania nchi huru inayotambulika kimataifa wit full sovereignty.

Hivyo basi, Zanzibar ni nchi isiyokuwa dola kamili, na kwa maana hiyo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar haiwezi kupinduliwa, na hivyo akina Machano hawakuwa na hatia kwa sababu Mapinduzi hufanyika dhidi ya dola kamili inayotambulika kimataifa na yenye Mamlaka kamili.

Kwa Tafsiri ya Kisheria, Tanganyika haipo, ila eneo lililoitwa dola la Tanganyika kabla ya April 26, 1964, ndiyo sasa Tanzania Bara na Watanganyika ndiyo Watanzania Bara; na eneo lililoitwa Zanzibar (dola kamili) ndiyo sasa ilipo nchi ya Zanzibar (ambayo siyo dola kamili).

Kimsingi, Tanganyika ilipoteza uhuru wake, na Zanzibar pia ilipoteza uhuru wake na hatimaye ikapatikana Tanzania.

Bado hujajibu hoja, you’re just eating around the bush
 
Mimi binafsi, hata Kigamboni pale siwezi kumiliki ardhi japo ninaruhusiwa. Sababu ni kwamba, kusafiri majini sipendi na kuishi karibu na bahari sipendi pia.

Halafu, ishu ya kumiliki ardhi ni rahisi sana. Ni wewe tu hujataka. Hata Tanzania Bara raia wa kigeni anaweza akamiliki ardhi kupitia uwekezaji na mianya mingine ya kisheria. Ni vile tu watu hamfatalii.

Labda, tuache hilo, twende huku huku Bara. Pale Kilimanjaro, ni ngumu sana mtu wa nje ya Mkoa ule kumiliki ardhi wakati sheria inaruhusu. Kwa ufahamu wangu, hapa Tanzania, hakuna eneo gumu kununua na kumiliki ardhi kama Kilimanjaro.

Kwa hiyo, kama Zanzibar ni ngumu kumiliki ardhi kwa sababu za kisheria, je ni vipi Kilimanjaro ambapo sheria inaruhusu ila ugumu upo?

Hata Mzanzibari akienda Moshi atapata tabu kumiliki ardhi.

Naona wewe unapenda ubishi tu! Huna hoja.

Ondoa matamanio yako binafsi na jibu hoja kisheria.

Je? Kuna Mtanzania anayekatazwa kumili ardhi Mkoa wa Kilimanjaro kisheria? Au ni hisia zako tu?

Kwa taarifa yako, kisheria Mtanzania Bara haruhusiwi kwa mujibu wa sheria kumili ardhi wala kuhombea nafasi yoyote upande wa Zanzibar.

Lakini Mzanzibari anaweza kumuondoa Mchaga wa Kibosho na ukoo wake wote na kumiliki ardhi hiyo kisheria, anaweza pia kuwa kiongozi wao kisiasa.

Kuhusu kumiliki ardhi kama muwekezaji, bado kuna privileges ambazo zitakuwa compromised ukimiliki ardhi namna hiyo, ikiwemo ukomo wa umiliki huo na kufaidika na ardhi hiyo kibiashara kama kuiuza baada ya kuiongezea thamani.

So get your facts right
 
Mimi binafsi, hata Kigamboni pale siwezi kumiliki ardhi japo ninaruhusiwa. Sababu ni kwamba, kusafiri majini sipendi na kuishi karibu na bahari sipendi pia.

Halafu, ishu ya kumiliki ardhi ni rahisi sana. Ni wewe tu hujataka. Hata Tanzania Bara raia wa kigeni anaweza akamiliki ardhi kupitia uwekezaji na mianya mingine ya kisheria. Ni vile tu watu hamfatalii.

Labda, tuache hilo, twende huku huku Bara. Pale Kilimanjaro, ni ngumu sana mtu wa nje ya Mkoa ule kumiliki ardhi wakati sheria inaruhusu. Kwa ufahamu wangu, hapa Tanzania, hakuna eneo gumu kununua na kumiliki ardhi kama Kilimanjaro.

Kwa hiyo, kama Zanzibar ni ngumu kumiliki ardhi kwa sababu za kisheria, je ni vipi Kilimanjaro ambapo sheria inaruhusu ila ugumu upo?

Hata Mzanzibari akienda Moshi atapata tabu kumiliki ardhi.
Jinga wewe
 
Huu muungano ni wa ccm, wao ndio wanajua maagano ya kishirikina waliyoingia kwenye muungano huu. Na kwa sasa kwa ajili ya hizi kelele, mama atahakikisha anatupiga ya mwisho mwisho ili hata tukitengana wawe wameshafaidika.
Mimi naamini Nyerere alijua ndo maana aliwahi kutamka"ningekuwa na uwezo ningekitupa kisiwa cha Zanzibar katika bahari ya Hindi" lkn kwa kuwa hakuwa na uwezo huo akatafuta namna ya kukimaliza na akaja na huu muungano. Wakati watanganyika leo wanalalamika, Wazanzibari walishalalamika sana na wanaendelea kulalamika lkn hawasikilizwi. Ukidhani hutendewi haki leo elewa kwamba Wazanzibari hawatendewi haki zaidi ya nusu karne iliyopita. Ukilalamikia 21% leo, Wazanzibari wanalalamika kutokupewa hata gawio la mapato katika benki kuu ambayo ina hisa 11.5% kwa zaidi ya miaka 50 sasa. Hebu kuwa muungwana basi na haya uyaseme angalau Watanganyika wengine nao wajue. Kule Waswahili husema "ukiona kwako kwungua kwa mwenzio kwateketea" .
 
Kosa moja halihalalishi jingine.

Kama kuna namna wazanzibari waliminuwa wangeweka wazi na ushahidi ukawepo,

Kimsingi bado hujajibu hoja yangu.

Je, Wa Tanzania upande wa bara tuna nufaika vipi na muungano wetu?
 
Munanufaika kwa kuikandamiza Zanzibar na sasa munanung'unika Kwa sababu rais ni Mzanzibari.
 
Mimi naamini Nyerere alijua ndo maana aliwahi kutamka"ningekuwa na uwezo ningekitupa kisiwa cha Zanzibar katika bahari ya Hindi" lkn kwa kuwa hakuwa na uwezo huo akatafuta namna ya kukimaliza na akaja na huu muungano. Wakati watanganyika leo wanalalamika, Wazanzibari walishalalamika sana na wanaendelea kulalamika lkn hawasikilizwi. Ukidhani hutendewi haki leo elewa kwamba Wazanzibari hawatendewi haki zaidi ya nusu karne iliyopita. Ukilalamikia 21% leo, Wazanzibari wanalalamika kutokupewa hata gawio la mapato katika benki kuu ambayo ina hisa 11.5% kwa zaidi ya miaka 50 sasa. Hebu kuwa muungwana basi na haya uyaseme angalau Watanganyika wengine nao wajue. Kule Waswahili husema "ukiona kwako kwungua kwa mwenzio kwateketea" .

Mimi sio muumini wa huo muungano uchwara, niwe muungwana vipi kwa muungano nisioutaka?
 
Wasalaam wana Jamvi!

Moja kwa moja kwenye mada.

1. Hakuna watu wenye raha katika nchi hii kama Wazanzibari. Wao wana privillages nyingi sana katika taifa kuliko mwananchi wa sehemu yoyote. Wao ni kama wana wa Mfamle na Watanganyika ni vijakazi wao.

Wana Uhuru wa kuishi upande wowote wa muungano na kupata haki zote bila shida yoyote, kitu ambacho ni ndoto kwa Watanganyika wakienda Zanzibar. Hawapewi haki yoyote ile katika visiwa hivyo. Sina haja ya kuelezea kila kitu kwa kuwa kuna nyuzi nyingi humu zimeeleza kwa upana sana.

2. Sasa limekuja swala la mikopo ya nje na ajira. Zanzibar wanatunyonya sana waTanganyika kama vile hamnazo hivi.
Kweli inaingia akilini kwa nchi yenye idadi ya watu 2M kupata Mkopo kwa 25% na ajira 21% dhidi ya nchi yenye watu 58 M?

3. Yote tisa, kumi mimi ninawataka Watanganyika ambao ni Pro-Muungano wa aina hii wanipe faida zinazotokana na Muungano huu kwa watu wa Upande wa Bara? Kwa Lugha nyepesi, mimi mtu wa Morogoreo nina faidika vipi na uwepo wa Muungano huu zaidi ya hasara.?

MWISHO! Jamani tuamke tulisemee taifa letu, tunataka usawa katika nchi yetu na sio vinginevyo
Kawaulize hao watanganyika wezako kina lukuvi na mzee vijisenti na wengine waliofanya figisu figisu wakati wa bunge la katiba walipopinga muundo wa serikali tatu. Wazanzibari tokea enzi za karume mkubwa hatukupendezwa na ukoloni huu wa tanganyika na hizo asilimia unazozisema ndizo walizokubaliana wakati huo 1964 lakini tu kulikuwa hakuna utekelezaji kwa sababu maraisi wote walitoka tanganyika.
 
Back
Top Bottom