Embu twende na uhalisia:
Taifa la Tanganyika, eneo lake ni eneo lote la Tanzania Bara ya sasa.
Kwa hiyo waliokuwa Watanganyika, ndiyo wanaitwa Watanzania kwa sasa.
Kisheria, Watanganyika hawapo na hata ardhi yao haipo. Ila, Watanzania wapo na ardhi yao ipo.
Zanzibar wana eneo lao kisheria. Wana watu, Serikali n.k. Watanzania, ambao Watanganyika wa zamani, nao wana serikali yao na taasisi zake.
Kwa hiyo, Watanganyika unaowataka wapiganie haki zao hawapo kwa sababu sasahivi Wanaitwa Watanzania kuanzia April, 26 1964.
Ila Wazanzibari wapo kisheria na haohao Wanzanzibari wanatambulika kisheria kama Watanzania.
So kuna Watanzania Wanzanzibari na kuna Watanzania ambao siyo Wazanzibari. Yaani, ni sawasawa kusema, kuna Watanzania Wasukuma na kuna Watanzania amabo siyo Wasukuma, maana wengine ni Wachagga, n.k.
Lakini, wewe unayejiita Mtanganyika, kwa mfano, ukienda Zanzibar au kupewa unachokitaka huko, kitabadilishaje maisha yako?
Lakini pia, ukibadilishwa jina ukaitwa Mtanganyika, kimsingi haitabadili kitu. Yaani haina tofauti na Mpare atake aitwe Mchagga.
Kimsingi, iliyokuwa Tanganyika ndiyo sasa Tanzania, ikiwemo Zanzibar.
Na huwezi ukawaita Watanganyika na kuwahimiza maana hawa watu wenye jina hilo la Watanganyika hawapo.