Wa-Tanganyika tuamke, tulinde haki zetu

Wa-Tanganyika tuamke, tulinde haki zetu

Watanganyika wengi n mazezeta sana! Hoja yako n ya msingi lkn kwa akili za watanganyika sawa na kumpigia gitaa mbuzi! Binafsi nashangaa sana mm kwenda Zanzibar lazima niwe na kibali wao wanakuja Tanganyika bila kibali zaid wale jamaa wanawimbo wao wa taifa lkn cc huku hatuna wimbo wa taifa shida Iko wapi? Vijana tunapaswa kupaza sauti juu ya Tanganyika yetu na sio kukaa kimyaa
 
Mkuu, wamepewa fedha kwa ajili ya miradi ya maji tu. Ni maji tu ya kuoga, kufulia, kupikia na kunywa.
Wala hata sio hela ya bia na bata.

Au kuna ubaya mkuu ?
Maana naona msingi wa hoja yako umeanzia kwenye mgawo wa huo mkopo wa "mabeberu".

Ajira 79% Tanganyika na 21% Zanzibar imekaa sawa ?.Idadi ya WaTanganyika 60 million na Zanzibar 1.5 million ????.
 
Mimi sio muumini wa huo muungano uchwara, niwe muungwana vipi kwa muungano nisioutaka?
Kwa kuwa ulisema mama atakupigeni ndo nikasema uwe muungwana useme dhulma wanazofanya Watanganyika kwa Zanzibar na sio kumzushia rais mambo ambayo hayapo. Ukitaka kutoa kibanzi kwenye jicho la mwinzio, toa kwanza boriti kwenye jicho lako. Hapa sizungumzii kuuchukia au kuupenda muungano.
 
Achana na hao mkuu. Wao kamba zao na ndefu na wamevimbiwa. Mtu qualification ya kuwa mbunge ni kujua kusoma na kuandika tu, yet mshahara 12m/=. Mwalimu, daktari au afisa kilimo aliesotea taaluma miaka mingi analipwa laki9/1.5m/=. Usitegemee mbunge kusemea Jambo lenye maslwhi kwa taifa.
hivi wabunge wa bara huwa hawalioni hili, au ni mwiko kuliongelea? hakuna hata mmoja anajilipua kutoa hoja hii ijadiliwe? ndio ataona watu wengi mtaani watakavyomsapoti. au wanatetea ugali wao tu.
 
Wasalaam wana Jamvi!

Moja kwa moja kwenye mada.

1. Hakuna watu wenye raha katika nchi hii kama Wazanzibari. Wao wana privillages nyingi sana katika taifa kuliko mwananchi wa sehemu yoyote. Wao ni kama wana wa Mfamle na Watanganyika ni vijakazi wao.

Wana Uhuru wa kuishi upande wowote wa muungano na kupata haki zote bila shida yoyote, kitu ambacho ni ndoto kwa Watanganyika wakienda Zanzibar. Hawapewi haki yoyote ile katika visiwa hivyo. Sina haja ya kuelezea kila kitu kwa kuwa kuna nyuzi nyingi humu zimeeleza kwa upana sana.

2. Sasa limekuja swala la mikopo ya nje na ajira. Zanzibar wanatunyonya sana waTanganyika kama vile hamnazo hivi.
Kweli inaingia akilini kwa nchi yenye idadi ya watu 2M kupata Mkopo kwa 25% na ajira 21% dhidi ya nchi yenye watu 58 M?

3. Yote tisa, kumi mimi ninawataka Watanganyika ambao ni Pro-Muungano wa aina hii wanipe faida zinazotokana na Muungano huu kwa watu wa Upande wa Bara? Kwa Lugha nyepesi, mimi mtu wa Morogoreo nina faidika vipi na uwepo wa Muungano huu zaidi ya hasara.?

MWISHO! Jamani tuamke tulisemee taifa letu, tunataka usawa katika nchi yetu na sio vinginevyo
Tanganyika haina viongozi wanaojali maslahi ya taifa Lao.wengi ni wachumia matumbo Yao,wenye hulka ya kujipendekeza ili waendelee Kula.Ni wanafiki na wabinafsi.Hawawezi kujitoa mhanga kupinga na kuelezea ukweli,kwa maslahi ya wanaowaongoza.Hongera Job Ndugai kwa kujaribu.
 
Ili kulinda maslahi ya eneo kubwa la nchi, rais wa Tanzania hatakiwi kuwa mzanzibari............nafikiri wote mnashuhudia kinachoendelea kwa sasa.
 
Muungano wa michongo, nchi mbili kuungana kuwa nchi mbili.
 
Ajira nyingi kazitoa kwa wanzanzibar wenzake
 
Sielewi kwanini mnateseka sana na suala hili..
Roho za ubaguzi zinawasumbua hawa waungwana, wanadhani wakishakuwa na Tanganyika yao kila tatizo litakuwa limepata suluhisho.

Haina njia ya mkato maishani, ukidhani ipo na inakusaidia tambua huo ni mtego ambao kuchomoka itatumika nguvu nyingi na muda mwingi.
 
Ajira 79% Tanganyika na 21% Zanzibar imekaa sawa ?.Idadi ya WaTanganyika 60 million na Zanzibar 1.5 million ????.
Kwaiyo unataka "wao" wapate 1% mkuu ?

Unajua dhana ya Muungano ni kuleta umoja, tukienda kwa mtazamo wa "hii yangu sio yako" nadhani hatuwezi kufika.

Muungano ni sawa na urafiki, haufanyi kazi kama mnataka "kuvimbiana" kwenye kila kitu.

Tatizo la msingi la sisi watanzania haliwezi kuwa "wao wanapata sana, sisi tunapata vichache".
Tutumie nguvu zetu wote kwa pamoja kukabiliana na matatizo serious ya karne ya 21. Kenya na Dunia wanazidi kutupiga bao huko ujue.

Hii ni sawa na watoto wa nyumba ndogo na nyumba kubwa (baba yao ni mmoja) wanatoana roho kwa kugombea bakuli la mchuzi.

Haya ni maoni yangu binafsi mkuu.
 
Kosa mojawapo kubwa alilolifanya Mwalimu, ni huu Muungano usio na vigezo vya tija.

Mwalimu alifanya kosa kuwakubalia Wamarekani waliotaka Tanganyika iichukue Zanzibar.

Kama Wazanzibar wanautaka huu Muungano, wanatakiwa wakubali kuwa na Serikali moja. Au la Watanganyika waridhie serikali tatu.
 
Mkuu, wamepewa fedha kwa ajili ya miradi ya maji tu. Ni maji tu ya kuoga, kufulia, kupikia na kunywa.
Wala hata sio hela ya bia na bata.

Au kuna ubaya mkuu ?
Maana naona msingi wa hoja yako umeanzia kwenye mgawo wa huo mkopo wa "mabeberu".

Maji ni uhai
 
Tuulinde muungano wetu kwanguvu zote anaeona Muungano hauna faidi hajielewi na hajitambui
 
Wasalaam wana Jamvi!

Moja kwa moja kwenye mada.

1. Hakuna watu wenye raha katika nchi hii kama Wazanzibari. Wao wana privillages nyingi sana katika taifa kuliko mwananchi wa sehemu yoyote. Wao ni kama wana wa Mfamle na Watanganyika ni vijakazi wao.

Wana Uhuru wa kuishi upande wowote wa muungano na kupata haki zote bila shida yoyote, kitu ambacho ni ndoto kwa Watanganyika wakienda Zanzibar. Hawapewi haki yoyote ile katika visiwa hivyo. Sina haja ya kuelezea kila kitu kwa kuwa kuna nyuzi nyingi humu zimeeleza kwa upana sana.

2. Sasa limekuja swala la mikopo ya nje na ajira. Zanzibar wanatunyonya sana waTanganyika kama vile hamnazo hivi.
Kweli inaingia akilini kwa nchi yenye idadi ya watu 2M kupata Mkopo kwa 25% na ajira 21% dhidi ya nchi yenye watu 58 M?

3. Yote tisa, kumi mimi ninawataka Watanganyika ambao ni Pro-Muungano wa aina hii wanipe faida zinazotokana na Muungano huu kwa watu wa Upande wa Bara? Kwa Lugha nyepesi, mimi mtu wa Morogoreo nina faidika vipi na uwepo wa Muungano huu zaidi ya hasara.?

MWISHO! Jamani tuamke tulisemee taifa letu, tunataka usawa katika nchi yetu na sio vinginevyo
Huu upuuzi sio wa Wana CCM
 
Back
Top Bottom