Wa-Tanganyika tuamke, tulinde haki zetu

Tafuta video clip ya mbunge wa Isimani mh Lukuvi akiongea pahala flani utajua kwa nini wabara ndiyo mnang'ang'ania muungano....
 
Tatizo kubwa ni umma kukosa uwakilishi bungeni kufuatia wizi wa Kura mnamo 28/10/2020.
Kwa sasa HAKUNA anayeweza kuhoji huu wizi na unyang'anyi kule bungeni.
Ndugai alijaribu kidogo yakamkuta!
Tanganyika imegeuzwa kinyemela kuwa Shamba la Bibi. Wanavuna mwanzo mwisho!

 
Waafrika tuna matatizo makubwa sana.

Marekani ni Muungano wa nchi 52 ila husikii kelele za aina yeyote.

Sisi hapa nchi mbili tu kila siku yanaibuka mapya.
 
Mkuu, wamepewa fedha kwa ajili ya miradi ya maji tu. Ni maji tu ya kuoga, kufulia, kupikia na kunywa.
Wala hata sio hela ya bia na bata.

Au kuna ubaya mkuu ?
Maana naona msingi wa hoja yako umeanzia kwenye mgawo wa huo mkopo wa "mabeberu".
Znz wanajengewa vituo vya afya kila umbali wa 5 km..
Mbona kwa Bara hakuna hilo?!!!
 
Katiba mpya wananchi walioendekeza serikali tatu!CCM Kwa ulafi wao wa madaraka wakatupa maoni ya wananchi!
Kweli tumepigwa na kitu kizito sisi wadanganyika!
 
Huu ndiyo ujinga wetu kuwa proud na jambo la kipuuzi
 
Ok twende na Logic yako.

Mtanzania mwenye asili ya upande wa bara anafaidika vipi na huu muungano?

Kipi hasa anakipa akienda Zanzibar ambacho waZanzibari wakija bara wanapata??

Tusaidie hapo Mtaalam
Hawezi kukujibu bali bla bla za watawala
 
Tatizo ni ccm wabunge na mawaziri ni mazuzu
 
Waafrika tuna matatizo makubwa sana.

Marekani ni Muungano wa nchi 52 ila husikii kelele za aina yeyote.

Sisi hapa nchi mbili tu kila siku yanaibuka mapya.
Ya USA yana ukweli. Lakini hii ya hapa hata wananchi hawashirikishwi, na ni mwiko kuujadili !!
 
Waafrika tuna matatizo makubwa sana.

Marekani ni Muungano wa nchi 52 ila husikii kelele za aina yeyote.

Sisi hapa nchi mbili tu kila siku yanaibuka mapya.
Vitu viwili tofauti kabisa. Huwezi kufananisha muungano wetu na ule wa wamarekani hata kidogo.
 
Sajazungumzia muundo

Bali idadi.
Umesema “muungano wa nchi 52 vs Muungano wa nchi mbili”

Muungano hauna muundo?

Ukilinganisha idadi bila ya kuhusisha muundo uliopelekea hiyo idadi ya kwenye muungano, ni ukosefu wa hoja yoyote kwenye bandiko lako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…