Wa Tz Tutakufa Maskini Kwa Kimbilia Kuchimbia Pesa (Kujenga) Badala ya Kuizungusha Izae Zaidi

Amani iwe nanyi ndugu zanguni ni takribani miezi3 sijapanda humu jukwaani yote kwa ajiri ya pulukushani za maisha niliimiss sana jf,haya niende kwenye mada niukweli usiopingika kukimbilia kujenga nyumba kwa pesa ya kuunga unga ni sawa na kuzika pesa zako ambazo ungeweza kuzitumia ktk kuzalisha kama wengi walivyo eleza.Kama wewe ni kijana huna wategemezi au huna hata mke hofu ya nini kubari kutake risk kuingia kwenye biashara.Usiogope kula hasara,hasara ni kama ajari tu,na kadri unavyo fanya makosea ndivyo unavyo pata zaidi maarifa inamaana pale ulipo kosea ukijafanya tena nilazima ufanye vizuri. Asante.
 
ii topic ni kwa ajil ya uhamasishaji, we should have ppl talking of what you are doing
otherwise gud idea!
 
Asikwmbie mtu mjini Hakuna baba mwenye Gari au baba mwenye biashara kuna baba mwenye nyumba ama mama mwenye nyumba zingine zootee porojo jenga nyumba then biashara na endelea kujenga na kujengaaa
 
Asikwmbie mtu mjini Hakuna baba mwenye Gari au baba mwenye biashara kuna baba mwenye nyumba ama mama mwenye nyumba zingine zootee porojo jenga nyumba then biashara na endelea kujenga na kujengaaa

Wewe umesema acha wadanganyane'
 
uko sahihi..biashara ni about taking risks.....ila inatakiwa usimamie mwenyewe..kwa mfano unaweka hiyo 10m kwenye biashara ambayo huna control nayo 100% (let say ni muajiriwa) ....unategemea nini zaidi ya kupewa stori??Kwa mfano,mimi kabla sijaacha utumwa(kuajiriwa) nilipopata 20m kwa mara moja yote niliifukia chini(nyumba nilishaanza kujenga wakati huo) kwa sababu niliona ujinga kuinvest wakati huko nyuma nilishainvest zaidi ya mara 7 bila mafanikio na tatizo langu niligundua ni usimamizi......baada ya muda ,nikajipanga,nikaamua kuacha kazi nikachukua mkopo wa 30m benki kutumia ile nyumba ..,,nikawekeza kwenye ufugaji wa nguruwe na kuku wa kienyeji.....then sasa samaki ....huu ni mwaka wa nne,ingawa haikuwa rahisi, lakini mambo yapo kwenye mstari.....Jamani Tuthubutu! Fursa zipo tele!!!
 
kweli mkuu,tatizo mazingira ya biashara tanzania sio rafiki kabisa!na zinataka wewe mwenyewe uwe msimamizi kila process vinginevyo wafanyakazi wezi
Point yako inakuwa explained na hii quote "Some people see the glass half full. Others see it half empty. wewe umeamua kuchagua kuitazama glass ya iliyowekwa maji nusu kama half empty na sio half full. Yaani umejikita kwenye kuidentify problems zaidi na sio opportunities. We cant move that way.

Tanzania ina watu 45m, wakulima ni 85% na wapo vijijin. Kimsingi ni wakulima wa jembe la mkono ambao tumashajiridhisha kuwa hawana uwezo wa kufeed 45 people. Hivi hii wewe unahitaji mwekezaji kuiona kuwa ni opportunity???Serikali yetu pmj na mapungufu yake, inajitahd kuweka mazingira rafiki kwa wanaojishughulisha. Huwezi letewa hela nyumbani.

Take tu initiative nenda hata wizara ya kilimo ulizia fursa zilizopo, Nenda walayani ipo hapo mirad ya district agri dev plans (DADPS) zipo hela hapo, nenda TIB, ipo pesa pale sasa tunataka nn cc jaman??? wizara ya kilimo inaweza ikakuwezesha ukapata hata heka 100 bure! i mean bure. ila hatutak kujituma. Cc ni wababaishaji tu, ndo the only expalnation. Anayebisha nipo tayari kusonga naye then tuone km hatutatoka.

Tanzania zipo opportunities nyingi sana, ila ni kwamba watu tu hawana uthubutu kama anavyosema Lara1. Biashara is all about how you execute na sio about how well your business plan/idea is. Mimi sio bizman ila naona kabisa kuwa zipo opportunities ambazo zinantaka uthubutu tu tena nyingine wala hata co mtaji at all.

Imagine mtu unalipwa mshahara wa 1 million, hii ukitoa kodi na mausafiri, ma lunch ukiwa kazin na nn mwisho wa cku ni kama umepata laki 6 kwa mwezi, tena hapo ujiminye hasa. ukigawanya kwa siku 30, utagundua kuwa umepata 20,000 per day. Kuhusu kukosa muda nalo ni tatizo lilelile, kwann ukose muda wa kukuzalishia pesa ming afu ukapata muda wa kukuzalishia 20,000 kwa mwajiri wako????

Tuassume wewe una degree moja. Unachotaka kusema hapa ni kuwa umeshindwa kutumia akili yako kupata kipato zaid ya 20,000 kwa siku na ndomana umeamua kuajiriwa.

Huu ni uvivu tu wa kufikiri. Takwimu zinaonyesha hakuna mwajiriwa Tajiri. Ili kuwa tajir unahitaj kufanya biashara na co kusaka high pay jobs. Katika mtandao wa matajiri wa Forbes, hakuna mwajiriwa pale aliyekuwa tajiri. sasa ni kwamba cc waajiriwa hatupendi kuwa matajiri au ni uvivu tu wa kufkiri???

Tanzania opportunities zipo nying sana. Mfano katika sekta ya kilimo. Leo hii wewe weka mipassion yako miche 500 tu kwenye heka zako mbili afu unambie ukianza kuvuna km hutopata zaid ya 20 per day. Hilo ni zao moja. Yapo mengi sana.

Huyo alopata 10m angesema achukue just 5m akannua miche yake ya maembe ya kisasa kama 500 kwenye kama 5 hekas huko mlandizi. Angepata pesa nyingi kwa mwaka kuliko kodi ya nyumba atakayoijenga kwa 10m au hata nyumba ya 50m. so ni namna ya kufkiri tu.Tatizo letu sehemu tunayohitajika kufikiri sisi huwa tunawaza. Mimi na concur na mawazo ya Lara1. Somewhere tuna problems ya kufikiri, nadhan ni lishe ya utotoni.
 
huyu Kiyosaki nasikia keshafilisika
Hawezi kufilisika huyu coz anajua inner cycle ya kuwa tajiri! As long as anakichwa kile kile, usitegemee kama atafilisika. Zipo ups and downs ila sio kuwa kafilisika. Tajiri anayefilisika ni yule aliyeupata utajiri kwa kubahatisha na sio kwa kujua inner game ya utajiri, Not Kiyosaki at all!
 
Wewe umesema acha wadanganyane'

Sasa unaweza kuwa baba mwenye nyumba lofaaa! Unaishi na wapangaji kama umepanga vile. Au unaweza kuzungusha pesa ukapata nyingi zaidi na kuishi kwenye MANSION lako na jaccuzz ndani! Maisha ni yako chaguo ni lako! HATUWEZI WOTE KUWA MATAJIRI!!!!!!!!!!!
 

Naona umefufukia jukwaa la watu waheshima na adabu,habari za kutoka kuzimu.
 

Ndugu
Kufanya biashara bila kuisimamia at least 90% ni kutafuta lawama....itakufa tu!mimi nilijaribu zaidi ya mara 7 nikawa napata hasara sababu watu wengine niliowaamini ndio walikuwa wanasimamia.....zikawa haziendelei...nikaamua kutake risk.nikaamua kuacha kazi 2008/2009 .....nikachukua mkopo kwa security ya nyumba yangu...nikawekeza kwenye ufugaji wa nguruwe,samaki na kuku ....mkopo nilirudisha ndani ya miaka miwili....sasa napiga mluzi tu...kujenga siyo ishu wala gari si ishu ..ni uthubutu tu
 

Sisi wengine tuliowasoma sana akina Robert Kiyosaki na wengineo tunakuelewa sana tena sana. Sijui kama wengine wanakuelewa. It is very difficult.
 
nakubalina na wewe ila ipo njia mbaadala ya kukomboe hela zilizo zikwa kama umezika kwenye sehemu sahihi na kwa kujenga kwenye ardhi sahihi. bank ukizitumia vizuri zinarudisha hela uliyozika na wakati mwingine hata zaidi na kuanzia pale ulipoishia wakati huo ukiwa una miliki mjengo wako.
 
Usicheze na ardhi,ndugu yangu alijenga nyumba Kwembe wakati huo kukiwa pori,akawa anafuga kidogo ndani ya miaka isiyozidi kumi kuna watu walitaka kununua ile nyumba kwa millioni mia tatu lakini jamaa alikataa.maisha ya kibongo hayatabiriki ukiwa na kanyumba at least unaweza hata ukaweka dhamana kwenye mikopo mikubwa ya Benki
 
shikamoo lara 1... point noted ..

But usituogopeshe bana kuwa na uhakika na mahali pa kuishi ni jambo jema pia!
 
Last edited by a moderator:

Mawazo yako ni sawa but lets be realistic and practical....Kwa mfano hapa nilipo nina Tshs 10m nataka kuizungusha izae mamilioni badala ya kuifukia...je,nifanye biashara gani itakayonilipa? naomba sensible facts na siyo stories za kufikirika na theories! please be focused
 

Mkubwa hii siyo story ya kufikilika, mbona mnakuwa na hamaki hivi!? Watu wanasimulia ushuhuda na mifano hai, hata kama huwezi mishe mishe ya biashara za kuzungusha pesa kuna mfano hai umeshauriwa hapo kwamba ukiwa na milioni 5 unaweza kupanda miembe 500 ambayo faida yake huko mbeleni ni kubwa kuliko ukijenga leo kibanda cha milioni 10. Sasa unachotakiwa kukifanya hebu fanya kautafiti kidogo, ulizia mashamba ya miembe yapo mengi tu, wakueleze gharama walizoingia kuyasimamisha, wakueleze mavuno na kipato chao kwa mwaka, kisha linganisha na hicho kipato cha banda lako la 10m. Huo ni mfano mmoja tu na kunamifano mingi sana! Sasa jiulizeni mbona wahindi hawajengi nyumba, ni wapangaji wakubwa, mbona wanaishi na ufanya biashara?! Kama wewe umefanya uwekezaji wako vizuri na miradi inafoka ipasavyo huwezi kunyanyaswa na mwenye nyumba akishajua wewe mambo yako yako safi na humsumbui kulipa kodi! Kama unacholilia ni kuwahi kwenda kujimwaga kwenye bangaloo lako huna tofauti na anaekimbilia kujitanua kununua gari lake aishie kushindwa kulihudumia na kulialia hili gari linakula mafuta kweli!

Endelea kuwa unarudia rudia kusoma hii thread ipo siku itagonga kwenye ufahamu wako na utachukua hatua itakayobadili maisha yako. Hebu wewe fikiri umepata leo mshiko mnene, kwa nini unanunua Toyota Harrier na siyo Toyota Hiace ili ukipata faida ununue hiyo Harrier? Wafanyabiashara wanaelewa sana concept hii isipokuwa WATUMWA (waajiriwa) hao ndiyo vipofu wanajua kuna pensheni inawasubiri, wakistaafu eti ndiyo wanaamka kufanya uwekezaji mweee!
 
Nakubaliana na wewe mkuu, na hivi hakuna sheria yoyote inayowabana kila mwaka wanapandisha kodi, chezea baba/mama mmwenye nyumba weye......

Asikwmbie mtu mjini Hakuna baba mwenye Gari au baba mwenye biashara kuna baba mwenye nyumba ama mama mwenye nyumba zingine zootee porojo jenga nyumba then biashara na endelea kujenga na kujengaaa
 
Good idea lakini sio kila mtu ni mfanyabiashara wengine tunachojua ni kuajiriwa tuu kwa kazi tuliyosomea na kulipwa mshahara/bonus na maisha yanaendelea,risk tulichukua wakati tulipoenda shule kwa zaidi ya miaka 20.
 
Wewe zungusha hiyo hela TRA waje kuchukua faida ya 30%,property ina appreciate zaidi ya huo mzunguko wako
 
hujaniconvice kuacha kujenga na kuishia kupanga!
Tutajenga na bness tutafanya tukiwa kwetu sio kwny hiz nyumba zinazopanda gharama kila cku
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…