Wa Tz Tutakufa Maskini Kwa Kimbilia Kuchimbia Pesa (Kujenga) Badala ya Kuizungusha Izae Zaidi

Huyu lara 1 inawezekana ni mrembo na anajirahisisha kwa ma don ili dili zake zifanikiwe.

Kuna wadada huwa nawaona mipakani wanapitisha vipodozi vya mahela, nenda wewe mwanaume uone.
 
Last edited by a moderator:
Na kwa mawazo yangu hapo ndipo opportunity ilipo,kwamba watu bado wamelala na kuishia kulalamika kwamba biashara ngumu,na misamiati mingi ya kiuchumi ya lugha za kigeni na theory za darasani,mtu anaongelea vitu vya kwenye eneo la tukio sisi tunabishana.

kwakweli mimi imenifungua macho sana hii thread kwamba nafasi ya kutoka bado ipo kwakuwa bado watu wamelala,ndio maana utakuta wanaojua wanaanza hata kama kuna vikwazo vipi wanapambana wakati wengine tunakaa pembeni tunasubiri washindwe,sasa unakuta hawa watu wanafanikiwa na sasa milango na ugumu wa hiyo biashara inafunguka ndio kilamtu anataka kuingia kwenye hiyo biashara sasa hapo ndio mnakutana watu kibaaooo mmefungua biashara inayofanana mtaa mmoja mnagombea wateja wakati wajanja walishapiga hela zamaniii na washaachana nayo kwakuona hailipi tena washatafuta nyingine wanaanza tena.

nimegundua vikwazo ndio vinafanya biashara iwepo,kungekuwa hakuna vikwazo kwamfano barabara safi,kilakitu kiko kirahisirahisi basi kilamtu angefanya biashara au mkulima angeleta mazao yake mpaka sokoni tena kwakutumia usafiri wake(gari lake)kwahiyo utaona kwamba,madalali,wasafirishaji nk wangekosa kazi au wangepungua au wangetafuta shughuli nyingine ya kufanya.

kiukweli wasomi wengi ndio wanaotukwamisha,inaonekana elimu tunayopata haitusaidii kubadilika,kwasababu utakuta mtu kasomea BIASHARA au MASOKO na kafaulu vizuri tu lakini hawezi kufungua biashara yake anasubiri kuajiriwa ataanza kuangalia vikwazo kibaoo,mara biashara ya nyanya sio nzuri zinaweza kuoza itakuwa hasara na mambo kama hayo wakati kunamtu darasa la saba hakufika haangalii hiyo misamiati ya kibiashara sjui feasibility study sjui nini na nini,anapita K/KOO anakuta uhaba analeta.kwahiyo mimi binafsi nakubaliana na mleta maada tunatakiwa tubadilike kifikra ndio mambo haya yatawezekana na zaidi mtu hulazimishwi kuufata ushauri huu unaweza kuendelea kufanya unayoona kwako ni sawa.nawasilisha
 

Nigga (call you so out of respect) you goddamn nailed it. Mtu yuko mid 20 ameajiriwa anajitutumua kujenga kwa bajeti iliyovuka kikomo...matokeo yake anamis opportunity kibao za kuongeza kipato na ndio kila siku amekazana kusoma vitabu vya richdaddy poor daddy...nyumba yenyewe in 10 years unayiona out of place sababu imejengwa under austerity measures....yaani hapa ndipo vijana wa-kikenya wanatupotushindia....wao angalau ufanya morgaging ambayo sio capital intensive. Word up for that....pia niliwahi ona article ya bbc kuhusu nyumba za moshi na bukoba ambazo hazina wakaaji watu wanalipwa wakae....we can do better than this...
 
Mkuu patriot.

Huo ndio ukweli wengi wetu ambao ni waajiriwa ni wavivu wa kufikiri and not not ready to take risk. Tuko busy kubeba majina ya makampuni tunayofanyia kazi kama vile ni yakwetu ( iam working with so and so company our offices are at this building in this street) hamna kitu ujinga mtupu.

 

.....Tena utaona watu wapo biize wamevaa ma uniform na badges za kampuni flani huku wanajisikia wamefika kweliweli....huu upuuzi mtupu!
 
daisy umeniacha hoi kwa haya maneno yako!
"tatizo letu sehemu tunayohitajika kufikiri sisi huwa tunawaza. Mimi na concur na mawazo ya Lara1. Somewhere tuna problems ya kufikiri, nadhan ni lishe ya utotoni"

Mkuu daisy tofauti ya kuwaza na kufikiri ni nini mkuu? usije ukasema nimeanza kuleta theories, teh teh teh!!
 
Sorry (hapo juu kwenye comment yangu) kumbe ni maneno ya Patriote
 

Penye miti hakuna wajenzi lara 1
Hata hivyo maneno mja hunena, muungwana ni vitendo (!!!).

ha ha ha....halafu ndio maana wachaga ni wachaga, wakinga ni wakinga na wazaramo ni wazaramo.
 
Last edited by a moderator:
Kiongozi kuwaza ni kama una daydreams hivi. Kufikiri ni kudirect akili yako katika kutafuta suluhisho la kitu flani. Kuwaza hakukupelekei kusaka suluhisho lolote yan ni mimawazo inakujiajia tu, mara unawaza upo kwenye jumba la kifahari bila kuelezea namna ya kukufikisha kwenye hiyo hali. Hapo chini ni a) mkao wa kufikiri na b) ni mkao wa kuwaza/wa daydreamers

a)



b)

 
Patriote kumbe hata signature yako tu imebeba ujumbe wa kutosha, nilikuwa sijaisoma!! pamoja mkuu!
 

Nimefuatilia toka mwanzo NA ulikuwa unajibu hoja vizuri ila Hapa Dada yangu umeharibu maana unaonyesha ni namna gani bado hujakomaa kifkra NA nmana NA Kujibu hoja.

Mimi binafsi naona either wewe hujaanza Kuwa NA majukum Kwa maana ya familia lakin pia inawezekana kabisa umetoka katika familia ambayo imejaaliwa Kuwa NA maisha mazuri of which wazazi NA ndugu zako hawakutegemei NA ndo maana yeyote anaye kusupport kuhusu kutozika hela nahakika atakuwa katika mazingira kama yako ya kutikuwa NA majukum ya extended family maana nakuhakikishia hakuna anaweza kukaa akafikiria kuboresha mradi au biashara kama bado familia yake haina uhakika wa mahala pa kuishi.
Nahakika as days goes by iko siku utakuja kukumbuka hizi comments ambazo zinatofautiana NA wewe Kwa maana zina kuchallenge NA naona hutaki changamoto sasa napata wasiswasi NA uzoefu wako wa maswala ya masoko maana marketing is full of challenges hasa Kwa maeneo unayokwenda maana hao wote hao wana deal NA FMCG/PCG.

Ntakuwa tayari kuchangia hoja kama utaonyesha kukubali changamoto maana mada yako ni nzuri sana ila tusipotoshane.



fuodenr and CEO of wwwdotoricdotcodottz and wwwdotaiodotcodottz
 
Alicho Ongea huyu Dada ndo ukweli wenyewe mkuu, Na hata Serukali inafahamu kabisa madhara ya watu kujenfa nyumba kwa kutumia pesa zao wenyewe, ila sema tu imepiga kimya, Tafuta mchumi mzuri anaweza kukupa hayo madhara make wengine sisi unaweza sema tunakudanganya

Ruturn ya Nyumba inachukua miaka mingi sana, na dhat is why Ulaya watu hulipa Mikopo ya Nyumba mpaka wanakufa na wajukuu wanaendelea kulipa, na zipo nchi nyingi sana ambazo kisheria huruhusiwi kujenga nyumba kwa pesa yako wewe mwenyewe, ni lazima uchukue mkopo Benki na si uchukue mkopo then uende Madukani kuanz kununua Misumari na bati, no kuna kampuni zinajenga and then unauziwa,

ULISHA WAHI KUJULIZA KWA NINI MAREJESHO YA MKOPO WA NYUMBA HUCHUKUA MUDA MREFU SANA KULIKO AINA NYINGINE ZOTE ZA MIKOPO?
 

Chasha, sio kwamba nampinga Dada yetu, hapana ila hoja yangu ni ngumu hiyo theory kui apply kutokana NA namna uchumi wetu ulivyo NA zaidi ni jinsi kila mmoja wetu alivyobahatika kulingana NA makuzi maana priorities zinatofautiana, mf: kama umezaliwa katika familia duni isiyo hata NA baiskeli wala kakibanda, hivi priority yako inakuwa katika miradi? Let's be honest and realistic!

Ila kama umezaliwa NA umekuta wazee wameisha jitosheleza kiuchumi nahakika hata wewe focus yako itaaanzia pale wao walipoishia maana huwezi kufikiria kuzika hela wakati baba au mama alishazizika Kwa ajiri yako, au huwezi kufikiria kununua usafiri maana tayari upo.

So issue ya kuzika hela ni swala la kibnafsi zaidi japo si vizuri kiuchumi
 
Mkuu
Kuwaza ni kama having illusions, while kufikiri is more of having constructive ideas. And is true as you put it "pale tunapohitaji kufikiri tunawaza" mfano unaweza mtu anafanya shughuli zake amefanikiwa badala na wewe ufikirie ufanye nini ili ufanukiwe unajikuta ukiwaza ningekuwa na hela kama za fulani....

 
Mada ni nzuri na ina ukweli sana ndani yake , kinachofanya watu washindwe kuelewana na mtoa mada ni kuwa baadhi yetu tunadhani ina apply kwa kila mtu. Nilichomwelewa dada ni kuwa kama unaweza kuraise na kushika say 10 milion , ni bora uzungushe biashara kuliko kuzizika kwenye nyumba .
Remember 10 milion ni recomended not dictated amount. capital threshold inaweza kuwa kiasi chochote kutegemeana na aina ya biashara .Ninachokiona hapa kwanza kuna makundi kama matatu:-

1: Si kila mtu ana uwezo wa kuishika hiyo 10 milion kwa wakati mmoja au muda mfupi, so watu wa aina hiyo mada hiyo haiwahusu. (Japokuwa wanaweza kudunduliza mostly kwenye ujenzi na kupata propery yenye thamani tajwa ,mind you ;hii ni time investment pia so inategemea malengo yako yatatimia muda gani )
2: kuna watu tayari wana uwezo wa kushika mabilion kwa wakati mmoja. watu hawa pia mada hii haiwahusu sababu wanauwezo hata wa kuestablish na kumudu ushindani real estate ambayo nadhani ni moja ya biashara kubwa duniani inayohusisha majengo .
3: kuna watu wako makazini wana mishahara mizuri na opportunity kibao' a good job has to offer' , wafanyabiashara na wengineo ambao hiyo 10 million wanaweza kuipata kwa njia mbali mbali hapa hata wale ambao walidunduliza senti wakafanikiwa kupata kitu ambacho (nyumba kwa mfano) thamani yake inafika 10 mil hawa ndio walengwa hasa wa mada hii.

My take ; Jipime kwanza mwenyewe uko kundi lipi financialy kabla ya kumpinga mtoa mada . Binafsi naupokea ushauri wa mtoa mada bila kipingamizi!!!!
 
Ndio naelekea kugraduate sista, Je mmi naweza niawa na fursa gani kiuchumi uanzia sasa maana nimepigika wei dada yangu, aau majuumu kibao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…