Wa Tz Tutakufa Maskini Kwa Kimbilia Kuchimbia Pesa (Kujenga) Badala ya Kuizungusha Izae Zaidi

sasa wewe uliyeanza na mil.5 kwahiyo sasa unazo mia moja au? Na pia aliyenunua viwanja vyake 2 Tegeta mwaka 1990 wataka kuniambia kwa sasa anaweza kukinunua au angeshindwa kabisa ?na watu wote Dar hawawezi kujenga O.Bay.Usijekuwa kama watu flani wanafika ulaya na kuwauliza wengine kwanini hampeleki watoto wenu Private school ebwana Bongo huwezi ukailinganisha na U.S.A.
 
Nina kiwanja nilinunua mwaka 2005 at 1.5m Tsh, Leo hii nikitaka kukiuza nitapata not less than 100m. Mind you hakina nyumba, yani kiwanja kitupu. sijajua bado ni biashara gani nifanye ya kuweza kuniingizia pesa yote hiyo within short time, na ukizingatia mimi ni muajiriwa.

Kwakweli mimi bado naamini kwenye uwekezaji wa real estate.
 


Ni wachache sana, point ni nzuri sana na mimi nakubaliana naye, hoja ipo ktk utekelezaji wake. Middle class wengi wangali na makovu ya umaskini wa familia zao huko vijijini tulikotoka. Unakuta wengi wanalazimika kujenga kwanza ili ku-upgrade life std ya familia husika, walau familia ipate utulivu wa akili.

Kwa hiyo sasa hivi tuko ktk kipindi cha mpito kuelekea huko unakosema dada, kwa hiyo usitegemee wengi kufanya hivyo hata kama wanajua ukweli huu.
 

Hapa kuna shule ya kutosha....

Binafsi huwa napatwa na hysteria bank account yangu ikiwa na pesa nyingi ambazo sijapangilia kuzitumia. Napendelea kuona pesa zangu sikiwa kwenye vitu na kutembea step kwenda nyingine.

Labda wadau wanieleweshe aina ya biashara ambayo wanaongelea...

Kwa Bongo, mchezo wa kuzungusha pesa (in this context) bado ni kama kamari...siyo kila yuko tayari kuucheza.
 

Kwa ugumu uliopo bongo wa kupata mtaji, fixed assets ndizo zinaweza kutusaidia. Labda kama tunaongelea watoto wa mafisadi wanaoweza kupata mkopo benki bila security.

Kufanya uchuuzi kwa pesa ya kubahatisha kunahitaji roho ya paka...

Hata hivyo sifagilii tabia za kupenda starehe na vitu vya gharama (eg. magari n.k) kwa hela ya kuazima.
 

umesema kweli hapo
.....tusaidiane,hasa hapo kuturn millioni kumi into mamilioni................kwangu mie naona km impossible vileee:confused3:
 

Hapo kwenye RED ni janga la kitaifa, nafikiri inabidi kuwe na special forums za kuelimisha vijana. Mtu anachukua mkopo anaenda nunu gari inayokula mafuta ya 30 -50 thousand a day, sijui wanakuwa wanataka kuprove nini.
 
umesema kweli hapo
.....tusaidiane,hasa hapo kuturn millioni kumi into mamilioni................kwangu mie naona km impossible vileee:confused3:

Hapo sasa ndipo unapojua kuwa tunatofautiana na hatuwezi kuwa na kipimo sawa (standard unit)..

Kuna wengine wanaweza kugeuza milion moja kuwa milion 100 ndani ya muda mfupi wakati wenzao wanazinywea bia.

Ni muhimu kuchukulia mijada kama hii kwa ungalifu. Kuna watu wanashauri wenzao eti wauze nyumba wakazalishe pesa bila kuwaeleza aina ya biashara ambayo itawafikisha kwenye hilo lengo.

Ukitaka kujua kwamba wetu wengi wanapenda sana kuzalisha pesa hata kama hawana ujuzi, fuatilia na kujua idadi ya watu waliozamisha mamilioni kwenye DECI!
 
umesema kweli hapo
.....tusaidiane,hasa hapo kuturn millioni kumi into mamilioni................kwangu mie naona km impossible vileee:confused3:

Inawezekana kabisa dada, ila ujikane sana ili kufanikiwa kuizungusha. Moja ya sifa muhimu ili kufanikiwa ni kufumba macho na kuziba masikio.
 
Natamani kila thread iwe na mvuto kama hii. Ninajifunza mengi sana! Thanks Lara 1.

Inakuvutia kwa sababu inatoa nadharia ya hali halisi iliyopo nchini mwetu, itavutia zaidi kama tutaiingiza ktk matendo zaidi.
 
Hapo kwenye RED ni janga la kitaifa, nafikiri inabidi kuwe na special forums za kuelimisha vijana. Mtu anachukua mkopo anaenda nunu gari inayokula mafuta ya 30 -50 thousand a day, sijui wanakuwa wanataka kuprove nini.


Hili tatizo liko nchi nyingi sana za Afrika...Juzi juzi nilikuwa na washikaji toka Ghana, Nigeria, Cameroon ....hali ni ile ile.

Tunahitaji kujifunza kwa Wakenya....walio wengi hawana hayo maringo maringo!
 
Inawezekana kabisa dada, ila ujikane sana ili kufanikiwa kuizungusha. Moja ya sifa muhimu ili kufanikiwa ni kufumba macho na kuziba masikio.

Ukipewa 10m utafanya biashara gani ifike 100m? Tupe mfano halisi
 

Mi naona huo uamuzi wako wa kuacha kazi ni sahihi ila kwa sera za nchi hii unakuwa SIO sahihi kutokana na sera na miundo mbinu mibaya ya nchi yetu ambayo kila leo inaongeza uwepo wa systematic risk(non-controlable risk) mfano,umeme kukatika,rushwa,utawala mbovu,inflation matapeli na vingine kibao ambavyo vinafanya return iwe uncertain so biashara kwa bongo hapa ni kama gambling,Umesema kuwa una kazi yenye mshahara mzuri kwa nini usiutumie kuanzisha biashara ambazo zinajiadministrate zenyewe i mean ambazo unaweza kuzifanya bila kuathiri muda wako wa kazini maana sio kila mtu aliyepata mizuka ya biashara ilimlipa ipasavyo,tunaona watu kibao wanalipwa pension zao na kuingiza mahela yao kwenye biashara na wakaishia kulia tu.So jiangalie mara mbili kwenye huo uamuzi wako unaotaka kuchukua la sivyo kuchanganyikiwa kunakuita.
 
Dada naomba usome kitabu cha poor dad, rich dad,ni kitabu maarufu kidogo nimesahau jina la mwandishi, Biashara ina factors nyingi sana for it to be successful,aina ya mtu,elimu yake ,kazi anayofanya,mazingira,miundo mbinu ya kibenki,culture ya jamii unayofanya nayo biashara na mengine mengi,so idea yako is not like 1+1=2,NO NO NO NO NO NO
 
Ukipewa 10m utafanya biashara gani ifike 100m? Tupe mfano halisi

Niliwahi kusafirisha mbuzi toka Pombwe kisiwani mpaka Dar, mbuzi mmoja nilinunua Tsh 30,000/,kuna kulipia ushuru wa wilaya kila mbuzi Tsh 1000/, nauli ya mbuzi Tsh 4000/ na posho yangu pamoja na nauli, mbuzi alifika Dar kwa Tsh 40,000/ na nilikuwa na mbuzi 40, kwa hiyo nilitumia Tsh 1,600,000/ mpaka mbuzi anafika kwa mteja wangu. Mteja alichukua kwa Tsh 45,000/ jumla. Kazi hii ilikuwa inachukua siku mbili. Faida yake cash ikawa 5000 x 40 kila trip. Kwa week nilikuwa napiga trip mbili tu. Kwa hiyo kilia week nikawa nakusanya Tsh 400,000/ na kwa hiyo kwa mwezi nilifikisha 1,600,000/.

Sasa kama ningekuwa na 10M ningekuwa na uweza wa kuleta lorry/fuso zima la mbuzi toka Dodoma.

Kwa kuwa hukunipa time frame ya kuizungusha hiyo hela, umeona vile nilivyozungusha hiyo hela ambayo haikuwa hata 5M. Hii bz nimefanya mwenyewe na pengine huko mbele nikawa na ranch ya mbuzi kabisa.
 
Ukipewa 10m utafanya biashara gani ifike 100m? Tupe mfano halisi

Naona watu mmenijia juu kama moto wa kifuuu ila nimejipanga sikukurupuka kuleta huu upembuzi yakinifu..

Kama una 10Mills usitake mambo makubwa. THE MAIN KEY KWENYE BIASHARA YOYOTE NI KUSPOT OPPORTUNITIES NA NA KUZIGRAB BY THE BALLS.

Sasa opportunity inategemea unaishi wapi, na mazingira gani. Opportunity ya Kinondoni sio sawa na za Kkoo.

Ila naomba nikupe story ya client wangu nilimfanyia Market and Sales Consultation.

Huyu Client ni mchina anaitwa Jin, jin alitoka kwao china na mtaji wa 15000$ akaingia kariakoo na kontena 4 za juice flani very cheap kwa bei ya kuuzia 400. Akachemsha sokoni. Mzigo anao hautoki, bishara imemshika pabaya, expiary date inasogea tu. Wahindi kitumbini wamereject mzigo.

Jin akaenda kwenye consultation firm ya rafiki yangu, yuko ready kulipa. (Mind u ana roho ya kutu, biashara imekaza na bado hakati tamaa anatumbukiza mahela) Rafiki yangu akachemkaaa. Kitumbini wamereject mzigo.

Kama bahati tu akaniambia kuna kazi imenishinda kabisaaa, ndo akanielezea. Nikamuuliza itakulipa au mchina kabana sanaa. Akasema maslahi yapo yapo. Mi nikamwambia coz that stuff is cheap tupeleke maduka ya mashuleni. Kids ndo wanapenda hizo makitu.

Mzigo ukapelekwa shule chache tu, Bunge, Olimpyo, shebbyrobi, Zanaki, Mzizima, Tambaza, Jangwani, na shule za pale jirani, tena mzigo unampa muuza duka kwa credit akiuza akulipe.

Wiki tu, Kontena 4 kwisha kabisaaaaaaaaa. Mchina mwenyewe aliblooo mapigo. Ndo kaenda kwao huko anampango wa kushusha mzigo wa laana!!!!!!!!!! Afu mimi sikupata hata senti tano kipande kwa hii kazi. Na mdau nae alipata hela ya mboga tu, Mchina ndo alimwaga razi, kwa mauzo tu ya pale pesa ilifika 40 na kitu Mills kwa mauzo ya 1 week.

THE SECRET IS SPOTTING THE OPPORTUNITY AND GRABBING IT BY THE BALLS
 
ni mtazamo wako, uko huru kusema, lakini usiwapuuze kwani nao ni mawazo yao. zako umezungusha toka lini na ni ngapi sasa
 

HAHAAAAAAAAAAA! sasa coz biahsara ina mambo mengi basi ndo uikwepe? Kwa mantiki hio hata shule mtu hutosoma coz kuna mambo mengi ya kufaulu ama kufeli.

Ujue mimi mwenzio mishemishe zangi ni kkooo na kitumbini daily! So maybe nimezoea kuona watu wanakuja na 10m na kumwaga razi ndani ya mda mfupi.

Sikatai wengine wanaanguka ila kuanguka ndo kujifunza unasimama tena na tena. YAANI UNGEMUONA ZAKARIA PESA ANAYOINGIZA PALE KITUMBINI UNGELIA MACHOZI!!!!!!!!!!! Hana shule kivile wala nini.

Plus hivo vitabu vyote na zaidi kina Kotler, Shapiro, vote nimesoma. Nimemajor in Investments management.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…