Niliwahi kuisoma elimu ya logic (Mantiki/Ilmul Kalam) elimu hii wao na ukweli wako mbali mbali.Jifunzeni kujenga hoja kabla hamjaleta hoja
Huu ni mfano mzuri wa "circular Argument" au hoja duara,ambayo kwenye majadiliano/debate ni hoja yenye makosa (fallacy)
Huwezi kuhitimisha juu ya "Circular Argument" bila kuichambua hoja husika na kujua msingi wake ni upi na ukweli wake ni upi.
Nyinyi huwa mnafikiri kitoto kwa kujenga kanuni zenye ukomo na dhaifu kushinda nyumba ya bui bui.
Ukisoma kitabu kiitwacho "Adabul Bahth wa al munadhara" (The etiquette of research and debate/Adabu za kujadiliana na kufanya utafiti) utaona makosa mengi kwenye mtindo wa kiyunani wa kuhoji na ndiyo asili ya logic huko hasa kwa Aristoto mnayo ishi nayo nyinyi.
Mimi nakupa kazi hii ukiweza naacha kutumia hii ID. Onyesha ufallacy wa hiyo hoja kwa kutumia misingi hiyo ya logic kisha iwe kweli na uwe umepatia.
Kosa la kwanza liko hapa katika namna dhaifu ya kuhoji,kwanza inaonyesha wazi Qur'aan huijui.1.Quran ni kitabu kisicho na shaka ndani take
Amesema nani?
Jibu amesema Allah kupitia Malaika muheshimiwa kufika kwa mtume Muhammad amani ya Allah iwe juu yake.
Swali la pili halija utofauti na swali la kwanza,na jibu lake ni hilo huko juu.2.Amesema Allah (SWT)
Amesema wapi?
Mbinguni kuna ubao huitwao "Lawhul mahfoodh" ubao wa kuhifadhia mambo,ubao umeandikwa kila kitu na mambo yote yaliyo kadiriwa kutokea. Malaika Jibrili huchukua maneno yale ya Allah kumfikishia mtume na mtume katufikishia sisi.
Kurudi pale siyo hoja,hoja ni wewe kuangalia kosa liko wapi na uweke usahihi wa mambo. Inaonekana kama vile mgeni wa somo la "logic" yaani kama umelisoma au unalisoma basi hushughulishi akili yako kutafakari.3.Kwenye Quran
Hakuna mtu mwenye akili timamu na kufikiria sana,akaunga mkono somo la logic kama fani,sababu linamfanya mtu kuwa mvivu wa kutafakari mambo katika uhalisia wake na kuishi katika misingi dhaifu walio iweka kina Aristoto na wengine.
Ukisoma elimu ya uhakiki wa habari,nafsi ya kwanza huwa shahidi mkubwa sana juu yake. Mathalani,leo hii tukitaka kukujua wewe kiundani na kwa hakika hasa,tuanze na wewe au tuwafate wale wanao kufahamu ? Jibu sahihi la haraka haraka lazima tuanze na wewe,kisha tunahakiko kile unachokisema kisha tukiona haja tunawauliza wale wanao kujua.Yaani umerudi pale pale,hapa unataka kuthibitisha uhalali wa Quran kupitia Quran yenyewe ambayo maneno yake ndiyo tunayotaka kuyathibitisha...umeona udhaifu Wa hoja yako?
Narudia tena,onyesha fallacy katika hoja hiyo kwa kuzingatia matini (contents) zake.