Waafrika ni muda sasa wa kurudia kuabudu Mizimu yetu

Waafrika ni muda sasa wa kurudia kuabudu Mizimu yetu

Kuna wengine huyo unaemuomba hatoi majibu........ Dunia kila mtu na formula zake wengine mizimu inajibu
Ndo maana nimemwambia yeye aendelee kuabudu mizimu kwakua inajibu na mie naamuabudu Allah anipa majibu asishawishi watu kila mmoja ana Uhuru wa kuabudu anachokiamini mizimu jua moto masanamu etc.
 
Hizi hoja za kumpinga mungu skuiz zipo nyingi sana humu
Sio kupinga ukweli ndio huo naambatanisha ushahidi
2023_11_16_15.22.49_edit.jpg
 
Laiti ungeijua nguvu ya MUNGU usingewaza vibaya.Ukifikia level flani ya kumjua MUNGU huwezi sema hivyo.MUNGU hapendi dhihaka.Kumbuka alikukomboa kwa damu ya thamani ya Mwanae
Ukisha sema Mungu apendi tayari usha fanya dhihaka.
 
hizi zote ni stori za kipuuzi tu kuanzia ukristo uislamu na hata za mizimu zote ni ujingaa
kfikiria kwa namna hii

unajua ni kwanini ilikua rahisi watu kuacha asili zao na kuwa wakristo?
sababu waliokua wakiabudu walitaka kuona matokeo ya ukwelii lakini haikotokea mfano vita ya kinjekitile watu waliishia kufa kwa sababu ya kuamini uganga

mzungu akaaja na mungu wake ambae akatudanganganya kuwa hauwezi kumuona hadi ufe na hata ukimuomba vipi hakupi unachotaka anakupa unachostahilii
ikawa mtu ukibahatisha jambo kwenye maisha basi credit zote anapewa mungu
hii imefanya sasa watu wanashindwa kupambana wanaakaa wanatumaini kupambaniwa na mungu mwisho wa siku wanaloose

point yangu ni kuwa kila mtu aamue kufanya anachotaka ukiamua kuabudu mizimu au dini ni juu yako ukiamua kutoabudu chochote pia ni juu yako kwa sababu dunia iko random
chochote kinatokea wakati wowote inaweza kuwa ni juhudi zako au ni matokeo ya juhudi za wengine
[emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122]
 
Rejea kichwa cha habari tajwa hapo juu.

Dini ndio chanzo cha matatizo mengi Duniani. Katika Dunia ya leo raia wanakosa ushirkiano tu kwa sababu wanatofautiana Kidini, Mkristo anambagua Muislamu na Muislamu anambagua Mkristo. Na ubaguzi wa kidini hauzungumzwi sana ila kiukweli ndio unaotendeka kwenye ofisi nyingi na taasisi nyingi, siku hizi ubaguzi wa kikabila unaenda ukipungua, huku ubaguzi wa kidini ukizidi kukuwa.

Je Dini zilianza kuingia Afrika karne zipi;

Dini za Kiislamu na Ukristo zilianza kuingia Afrika muda mrefu uliopita. Ukristo uliingia Afrika kwa mara ya kwanza karne ya 1 BK (Baada ya Kristo) kupitia wamishonari na biashara na Waafrika wa Kaskazini. Ukristo uliendelea kuenea katika maeneo tofauti ya Afrika.

Uislamu ulianza kuingia Afrika katika karne ya 7 BK (Baada ya Kristo) kupitia kazi ya Muhammad na Waislamu wa kwanza. Kupitia biashara na uvumbuzi wa safari za jangwani, Uislamu ulienea kwa kasi katika maeneo mengi ya Afrika, haswa katika Afrika Kaskazini.

Je Kabla ya Dini hizi waafrika tulikuwa tunaabudu nini?

Kabla ya kuingia kwa dini za Kiislamu na Ukristo, tamaduni za Kiafrika zilikuwa na dini na imani za kiasili zilizojumuisha ibada ya miungu ya asili, roho za wafu, na nguvu za asili. Dini za Kiafrika zilitofautiana sana kutoka eneo moja hadi lingine na kati ya jamii tofauti za Kiafrika.

Mara nyingi, dini za Kiafrika zilijumuisha ibada ya miungu au roho za wakubwa wa kale, kama vile mababu au wazee wa kabila. Kwa mfano, jamii nyingi za Kiafrika ziliabudu miungu ya jua, mvua, na ardhi, kwa sababu vitu hivyo vilikuwa muhimu kwa maisha yao ya kila siku.

Dini za Kiafrika pia zilijumuisha ibada ya wazee na mababu waliokufa, kwa kuwa waliona kumbukumbu na heshima kwa wafu kama sehemu muhimu ya utamaduni wao. Imani hizi za kiasili zilikuwa sehemu ya utamaduni wa Kiafrika na zilisimulia hadithi za uumbaji, maisha, na mazishi.

Kwa hiyo, kabla ya kuingia kwa dini za nje, Waafrika walikuwa wanaabudu miungu yao ya asili na walikuwa na imani za kiasili zilizohusiana na maisha yao ya kila siku na utamaduni wao, na maombi yalikuwa yanafanya kazi.

MY TAKE: Ukitizama Dini hizi za Ukristo na Uislamu ni dini zilizoletwa tu Afrika. Walikuja na kutuambia Imani zao ni bora kuliko zetu, hivyo tuache Imani zetu tufate Imani zao. Dini hizi mbili zinaimiza katika Kusameheana, kutokuua, kutokudhuru, na zinaamini katika Kupendana. Inasikitisha sana hawa wenye dini zao wamekuja Afrika na kutuhubiria Amani lakini wao hawafuati hiyo Amani wala hayo mafundisho. Mbona wenye dini zao wenyewe Waisraeli na wapalestina wameshindwa kufuata maandiko na wanauana kama kuku, inakuaje mimi muhaya wa Bukoba ambaye hapo mwanzo nilikuwa naabudu mizimu nifuate maandiko hayo ambayo wahusika wenyewe wameshindwa kuyafuta.

Mimi kwa mtazamo wangu naona walitumia dini zao kama chambo hili kutuweka katika ukoloni miaka hiyo maana waarabu ndio walikuwa walanguzi wa watumwa kisha wanaenda kuwauzia wazungu. Hivyo walitumia mafundisho ya dini zao kutufanya kutufumba akili na uwezo ili iwe rahisi kututawala.

Mbona hatuoni ishara yoyote kutoka juu kwa muumba mwenyewe baada ya mapigano hayo, maana tunaambiwa maeneo yale ni matakatifu, hivyo kwa akili tu lazima kungetokea ishara ya kukataza mapigano, ila naona tu Aliakibar ndio nyingi huko Gaza, huku Shalom zikiwa nyingi huko Israel.
Kila mtu akiomba mwenyezi hamsaidie.

Sasa tumeona ni namna gani Dini hizi za kuletwa vile hazifanyi kazi, ni bora kurudi kwenye kuabudu Mizimu yetu ambayo hapo mwanzo tulikuwa tukiiomba, mwandishi mashuhuri wa vitabu Yericko Nyerere aliwahi kugusia hili, kwamba turudi kwenye Imani zetu za hawali, na mimi sasa naona umuhimu wake
Wa kulaumiwa kaka ni haya majamaa mawili
1.YESU
2.MUDY S.A.W
 
Mizimu ni kitu dhaifu sana kama ilishindwa muokoa mwafrika asichukuliwe utumwani plus kutawaliwa kuna haja Gani kuiabudu
 
Back
Top Bottom