Waafrika tulipotoshwa kuhusu Chifu Mangungo wa Msovero sio mjinga, Watanzania tuiombe familia yake msamaha na tumuenzi kama shujaa wa uwekezaji

Shida ni kwamba kila walichokuwa wanakizalisha kilipelejwa Nje kwenda kutengeneza material ya kutumia. Vibarua wa Kiafrika walifanya kazi Kwa mazingira magumu na ujira mdogo. Kila walichokifanya ni Kwa manufaa Yao na sio Kwa mwafrica
Bora walipata kidogo kuliko kushinda msituni kuwinda na kula matunda kama ndege
 
Shida ni kwamba kila walichokuwa wanakizalisha kilipelejwa Nje kwenda kutengeneza material ya kutumia. Vibarua wa Kiafrika walifanya kazi Kwa mazingira magumu na ujira mdogo. Kila walichokifanya ni Kwa manufaa Yao na sio Kwa mwafrica
Kwani sahiv serikali yako na wahindi wanakulipeni sh. ngapi yakusema ndo mshahara mkubwa tofauti na wazamani zile
 
Lengo la wazungu lilikuwa ni kutuua wote na kuchukua bara. Bahati nzuri wakakutana na magonjwa ya kitropiki kama Malaria, Malale, Homa ya manjano nk nk. Ndiyo yaliyotuokoa. Tunapokaririshana Economic advantage of diseases tukumbuke kuweka na hili.
 
Nauliza TU historia ya ukoloni..kwanini walikuwa wakitulipisha Kodi..kwanin wasingewekeza TU na kuchukua wanavyovitaka...why Kodi??
 
Umenifungua kitu.
 
Nauliza TU historia ya ukoloni..kwanini walikuwa wakitulipisha Kodi..kwanin wasingewekeza TU na kuchukua wanavyovitaka...why Kodi??
Alafu kazi wangefanya kina nani? Na je bila kumlipisha mtu kodi angefanya kazi?
 
Asante sana kwa andiko hili. Haya ndiyo tunayotaka yajadiliwe hapa! Umefikiri na kuchambua vizuri mno. Huu mjadala unaoweza kuwa topic ya thesis ya mtu anayechukuwa PhD. au topic ya kufundisha chuo kikuu!
 
Wakoloni walikaa miaka zaidi ya 200 humu! hatukuwa ba barabara nzuri km za leo, miundo mbinu km ya leo! tangu tumepata uhuru ni miaka 60 tu!! tuna kila kitu kizuri nchi nzima!

Pili Mangungo kuwa mjinga haihalalishi kuwa asiwepo Mtawala mwingine mjinga kama yeye!! au pengine mjinga zaidi yake!..na bado watakuja wengine wajinga zaidi na zaidi!

mwingine mbinafsi, mchoyo, umimi mpaka ukamuua sitaki kumtaja msije nipiga mawe humu!!...kunawatu wataachia mianya ya unyonyaji km huyo! lkn hatuta waacha kuandika kuwa walikuwa wajinga!

Ila baba wa Taifa heko..........tusinge fika hapa......leo! usiteteee upuuzi! tafadhali nakuomba.
 
Nauliza TU historia ya ukoloni..kwanini walikuwa wakitulipisha Kodi..kwanin wasingewekeza TU na kuchukua wanavyovitaka...why Kodi??
Wengi waliishi namna hii, unalima unavuna unakula maisha yanaenda. Sasa kama mtu pesa haijui asingeweza kujitesa .
 
Chifu mangungo hakuwa mjinga, watanzania tulipotoshwa, tunapaswa kuiomba familia yake msamaha
Weye ndo ulipotoshwa! sisi watanzania tuko njia sahihi kabisa huyo kiongozi muoga alikuwa hafai hata kuigwa!! hata hao wanaoiuza nchi leo wana fungu lao ktk historia!!

haina maana kwamba kwa kuwa tumejitawala basi tusiliwe kidogo big nooo!! mbona nyie mnakula vyao halafu mnashangilia???........lkn huyo chifu wako alijtoa kijinga mnoo! na kiuoga zaidi! bila kuhoji wala kupinga!

kama walivyo pinga wenzake kina chifu Mkwawa . Mukama Malumbo wa Majita Nk!! hiyo ya huyo Mangungo siyo sifa ya kiongoi Bora!.......

ni mifano wa viongozi vihiyo, waoga ,wasio maono, wabinafsi, wasijali watu wa chini, hao wapo mpaka leo hii! ninapo andika hapa, na wataendelea kuwepo!

Huyo chifu alikuwa na mazuri yake pia, lkn sisi tunapima mazuri na Mabaya ..na endapo Mabaya yatakuwa mengi basi tunampa Ubaya!!!.........siyo kwamba eti

viongozi wengine hawakuwa na ubaya nooo!! walikuwa nao, ..... ila je huo ubaya umekujaje?? wapi?Lini? nani? na kwa nini?...hii ndo inamuhukumu CHIFU MANGUNGO WAMSOVERO!
 
Au ulitaka Mangungo awadanganye watu kama kinjikitile ndio umuone shujaa?

Lengo la huu uzi sio kuyatangaza maovu ya Mangungo hayo yalishafanywa na wengine. Mini nimejaribu kumweleza mangungo katika fikra za leo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…