Waafrika tulipotoshwa kuhusu Chifu Mangungo wa Msovero sio mjinga, Watanzania tuiombe familia yake msamaha na tumuenzi kama shujaa wa uwekezaji

Mwanzisha thread ana hoja nzuri kama utakubali kupima pande mbili. Pamoja na kuwa mimi nahusudu sana kujitegemea na kujiletea maendeleo wenyewe lakini hebu niambie viongozi waliokuwepo baada ya chifu Mangungo kuondoka wamefanya nini tofauti naye? Ukiondoa mwalimu Nyerere aliyekuwa na vision na kuhangaika sana kutaka tujiendeleze kwa nguvu zetu ni yupi mwingine ambaye amefanya tofauti? Kwa nini tunamsema vibaya Mangungo wakati mtu kama rais wa sasa, Samia, anadhani bila usaidizi wa nchi nyingine sisi wenyewe ni bure?
 
Au ulitaka Mangungo awadanganye watu kama kinjikitile ndio umuone shujaa?

Lengo la huu uzi sio kuyatangaza maovu ya Mangungo hayo yalishafanywa na wengine. Mini nimejaribu kumweleza mangungo katika fikra za leo.
Mimi nimekuelewa sana. Lengi ni kutufungua macho tuone kuwa mtu ambaye kwenye historia anaitwa alikuwa kiongozi mjinga hakufanya tofauti na kinachofanywa na viongozi wa leo. Haitakuwa fair kumuita Mangungo ni mjinga wakati siku hizi rais anapofanya kile kile alichofanya anasifiwa na kuitwa rais bora. Kila mwekezaji anayekuja rais anapewa credit wakati Mangungo alifanya hivyo hivyo.
 
Au ulitaka Mangungo awadanganye watu kama kinjikitile ndio umuone shujaa?

Lengo la huu uzi sio kuyatangaza maovu ya Mangungo hayo yalishafanywa na wengine. Mini nimejaribu kumweleza mangungo katika fikra za leo.
Kwa fikra za leo ndo ha fit kabisaaa!! Uongo mwingine huu KInje hajawadanganya watu!! bali ile ilikuwa akili kubwa ya kuwatia moyo wapigananaji! ..

si unaona mjermani alivo tishikaa??..mpaka leo akikumbuka Mwili unamsisimka! hato sahahu milele!
 
Hapa naona kuna afrocentric historians na Eurocentric historians mchuano ni mkali. Nani yupo sahihi na Nani hayupo sahihi ni kama Imani za dini, kila mtu abakie na kile anaamini
 

Inaonekana wewe ni kitukuu cha Mangungo!
 
Haitakuwa fair kumuita Mangungo ni mjinga wakati siku hizi rais anapofanya kile kile alichofanya anasifiwa na kuitwa rais bora. Kila mwekezaji anayekuja rais anapewa credit wakati Mangungo alifanya hivyo hivyo.
Zamani za Nyerere tuwalifukuzilia kwa mbali hukoo! wakafanyie ujinga wao hukooo km kina Faza Thom na kundi lake! Leo akifanya hovyo tunaua! km Korimba si unawajua? Mtikila nk?! tupilia mbali kule! ....

Then .tuna subiria kwanza kumuandika vibaya! Nikuulize tuu nani kafanya ujinga na bado tuka mvumilia sisi wabongo??? Bashite unajua?, Sabaya ndo kabisaa, au yule mrafi na Mtekaji? km hujui aliko nenda chato?..

hao wooote si unajua hali zao weye lkn bana ! au huishi Bongo kijana! tena huyo wa Msovero ashukuru tu ni zamani lkn laiti angefanya hayo leo heee!!...wewe/yeye woote manzi ga nyanza!

Nakuuliza weye hujui Bazil Mramba na wenzake walivochapwa mpaka wakawa wanaokota takataka/ usafi Hospitali ya Sinza! ulikuwa wapi??? yaani hiyo huoni ni adhabu tosha kwa viongozi km huyo wa Msovero??

au ulitaka tuwauwe ndo ujue kuwa tumechukia??? ...Well! adhabu tuliyompa kambona , Bibi tii, Mohamed Babu, na yule komandoo aliye fia Msumbiji umesahau mara hii??......kweli weye kichwa chako bOga sana......

ndo tatizo lenu wana vijiji mnaleta mada wkt hata hujui kinachoendelea nchini! kifupi tumeaadhibu wengi sana na weye unastahili adhabu kushadadia waarifu!

Tatizo lako unadhani kuwekeza ni dhambi kwa kuwa hujui maana yake!......wanalipa kodi tunayotaka sisi!! na tunachagua sisi nani awekeze na nani asiwekeze! na kwa wakati gani!! tuna uwezo huo!

Mangungo yeye hakuwa na uwezoo wa kupinga alikuwa dhaifu! na chifu mzima na baraza lake looote alidanganywa sisi hatudanganywi

ikitokea wa ivo yeye huyo aliye mkaribisha na huyo mwekezaji wataipata fresh ile yenyewe!! mifano ni mingi tu!! ....ebu funguka bana weee!...huyo mzee wako ni moja ya mifano mibaya Africa ever!

hata Idd amini, Bokasa, Banda wa Malawi walikuwa ni mifano mibaya Africa, lkn wana wafuasi wao waliokuwa wana faidika nao! lkn wanaficha aibu zao! mbali kabisaaaa!...sasa weye mbraaaa!!
 

Pole sana mtoto wa chief Mangungo ndivyo siasa Ya Africa ilivyo.
 
Samia, anadhani bila usaidizi wa nchi nyingine sisi wenyewe ni bure?
Yes! Mama yuko sahihi sana!! kwanza anatambua sisi siyo kisiwa! anajua watu tunahitajiana sisi km wao, marafiki wa kweli na wa wazi siyo wanyonyaji wa kujipendekeza,

pili anafanya kwa uwazi, tena kwa faida yetu wooote! nani tushirikiane naye (na nani tusishirikiane naye) halazimishwi kijinga km Mangungo!

Na matokeo ni halisi, hapelekwi! pelekwi! (Iron fist Lady).......anajitambua! anachagua nani awe!! na nani asiwe nchi Rafiki!...anajali na kuthamini, michango ya ndugu zake wa AO, EAC, na SADDAC!

Kifupi Mama yuko njema usijaribu kumtania! Amejipanga! na misimamo inayoeleweka labda km una yako! na hakuna km Mama!..........

Stone!! ana la kujibu, ina maana siku zikiendaaa!....lile kaburi lake litapigwa Pingu!. make kafa akiwa hajafikia hatua ya kuwa na kinga ya Urais! na hilo kaburi la Mangungo linastahili kupigwa pingu sasa hivi.!
 
umeandika kitu kizuri lakini si kwa kizazi na watawala wa sasa wanaweza penda hiki
 
Ahsante sana nadhani umenisaidia kunieleweshea.
 
Nakubali asante na uandishi mkubwa na akili kubwa hongera sana, amazing analysis and thinking 🙏🙏🙏
 
Unaonekana unakazi maalumu hapa JF???

Geuka nyuma angalia kwenye ubao .Kama jina lako sio la kwanza pia haliwezi kuwa la mwisho.

Sisi hatuzungumzii mambo ya kulamba nyayo na siasa za maji taka.

Tunamzungumzia Mangungo kama mkazi wa msovero iliyokuwa huru chini ya himaya yake . Wakati huo alikuwa na uhuru wa kukubali au kukataa.

Waliosema alikuwa mjinga wametoa sababu zao acha na sisi tunaosema hakuwa mjinga tutoe sababu kisha wasomaji watapima hoja zipi ni nzito.

Hapa hatupo kulinganisha awamu ya tano na ya sita.

Mjadala huu haupo katika kupima uzalendo wa mtu bali kuchimba yale yasiyoandikwa vitabuni.

NB: kama mjadala upo juu ya uwelewa wako tafadhari ignore huo huzi sio kosa nenda kwenye nyuzi saiz yako.
Usione kila ID mpya basi ni mgeni mwenzako .Watu tulikaa pembeni kama wasomaji zaidi ya miaka 7 tukijifunza namna gani JF watu wanajadiliana.

Tangu kizazi cha FB muhamie Humu mmekua kero sana.
Huyo uliyejiunga kumtetea hata atende mema kumzidi Musa bado kuna siku atafumba. Macho.
Jiheshimu HAMMY
 
Au ulitaka Mangungo awadanganye watu kama kinjikitile ndio umuone shujaa?

Lengo la huu uzi sio kuyatangaza maovu ya Mangungo hayo yalishafanywa na wengine. Mini nimejaribu kumweleza mangungo katika fikra za leo.
Wewe utakuwa ni msagara au mkaguru. Hapa unajaribu kupaka rangi uovu wa Huyo chifu Mangungo ambaye mpaka sasa huko Kilosa hata ukoo wake haujulikani. Mangungo alikuwa chifu dhaifu sana na si
mfano wa kuigwa leo.
 
Inaonekana wewe ni kitukuu cha Mangungo!
Hapana ila naifahamu kilosa in and out . Ndio maana hata mtu akiniambia kilosa sasaivi inaendelea nitabisha na kumwambia Kilosa inajegwa upya ilishawahi kuendelea huko zamani.
 
Mkuu acha kuhalalosha ujinga uliofanywa na huyo chief kwa kutumia kigezo cha uwekezaji katika karne hii.Maana hata kinachofanyika Sasa hivi bado ni ujinga kama alioufanya huyo chief,hamna Taifa lolote la watu wanajielewa akupe ardhi yake eti wewe uwekeze-ni ujinga wa kiwango cha PHD kwa nini wasiwekeze watu wako??
Kwa nini hao wawekezeaji wasiwekeze katika Nchi zao waje kuwekeza kwako,kwanza wanaua ubunifu wa watu wako na unaimarisha chumi za Mataifa yao kuliko lako-sasa hizo ni akili au matope?
 
Wewe utakuwa ni msagara au mkaguru. Hapa unajaribu kupaka rangi uovu wa Huyo chifu Mangungo ambaye mpaka sasa huko Kilosa hata ukoo wake haujulikani. Mangungo alikuwa chifu dhaifu sana na si
mfano wa kuigwa leo.
Hapana sio msagara mimi kwanza kiasili. Wasagara sio kabila moja bali ni watu kutoka maeneo mengi pembezoni mwa Morogoro na KUZAGAA/ Kutawanyika kilosa ndio wakaitwa Wasagara au watawanyikaji. Ndio maana Wasagara hawana lugha maalumu kama kabila zingine sababu ni mwingiliano wa lugha nying wakajikuta wanaongea kiswahili.
 
Wewe utakuwa ni msagara au mkaguru. Hapa unajaribu kupaka rangi uovu wa Huyo chifu Mangungo ambaye mpaka sasa huko Kilosa hata ukoo wake haujulikani. Mangungo alikuwa chifu dhaifu sana na si
mfano wa kuigwa leo.
Hapana sio msagara mimi kwanza kiasili. Wasagara sio kabila moja bali ni watu kutoka maeneo mengi pembezoni mwa Morogoro na KUZAGAA/ Kutawanyika kilosa ndio wakaitwa Wasagara au watawanyikaji. Ndio maana Wasagara hawana lugha maalumu kama kabila zingine sababu ni mwingiliano wa lugha nying wakajikuta wanaongea kiswahili
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…