Waafrika tulipotoshwa kuhusu Chifu Mangungo wa Msovero sio mjinga, Watanzania tuiombe familia yake msamaha na tumuenzi kama shujaa wa uwekezaji

Chifu Mangungo wa Msovero ni mmoja kati ya machifu wa Afrika ambao waliamua kushirikiana na wakoloni kama moja ya njia ya kukwepa kutawaliwa katika maeneo yao au kwa kufaidika na mgao ulokuwa ukipitishwa na wakoloni wa kijerumani baada ya kutuma mzigo wa malighafi kwenda kwao barani Ulaya.

Kama unavyofahamu moja ya malengo makuu ya wakoloni kuja Afrika pamoja na kututawala ilikuwa ni kufuata malighafi.

Wakoloni khasa wa kijerumani walipokuja Afrika walikutana na vikwazo vya aina tatu kutoka kwa waafrika wakiongozwa na machifu kama Mirambo wa Wanyamwezi, Mkwawa wa Wahehe , Chifu Machemba wa Wayao na Kinjekitile Ngwale wa Wangoni.

Kipingamizi cha kwanza ulohusisha ulihusisha mbinu kama kuharibu mashamba ya wakoloni au pia kuwaua. Kilingamizi hiki kiklitokana na mifumo imara ilojengwa na machifu kama Mkwawa na Mirambo ambao walikuwa ni viongozi imara waso legelege, wenye jeshi imara na umoja ulotukuka. Pia tawala hizi zilikuwa na mifumo imara ya uchumi, vyombo vya utawala na jamii zilokuwa zajielewa na pia kuwa na mbinu za hali ya juu za kivita. Kwa mfano machifu hawa waliweza kutumia milima kujilinda na kuiona adui atokea pande zipi.

Upinzani wa aina ya pili dhidi ya wakoloni ulikuwa ni kuwaacha wakoloni wafanye yao bila kushirikiana nao kwa maana ya kuwapatia vibarua wa mashambani na pia kutotumia vita kupigana nao. Pia aina hii ya upingaji ulohusisha kutolipa kodi ya kichwa, kutokuzalisha mazao ya biashara mashambani na kukataa kufanya kazi za mashambani.

Sasa hawa walokosa silaha, hawakuwa na jeshi imara, viongozi wao kuwa dhaifu, watu wao wenyewe kuwa waso na mshikamano na ushirikiano na pia kutokuwa na vyombo imara vya kusimamia jamii zao.

Kwanini Chifu Mangungo wa Msovero aliamua kushirikiana na wakoloni wa kijerumani kwa kuwauzia ardhi yake?

1. Alikuwa ni kiongozi ambae alikuwa ni dhaifu na pia hakuwa na jeshi imara ambalo lingeweza kukabiliana na jeshi la wajerumani. Wajerumani walikwishanya ujasusi wa kutosha ambao uliwapa taarifa au "dossier" yote juu ya udhaifu Chifu Mangungo na ndo maana wakamtuma Carl Peters.

2. Kwa kuwa Chifu Mangungo alikuwa ni dhaifu alitumia mwanya huo kushirikiana na wajerumani kwa minajili ya kutaka kunufaika kijeshi ili apate nguvu ya kupambana au kujilinda kwenye mipaka yao dhidi ya uvamizi wa machifu ambao walikuwa na nguvu kwelikweli kama Mkwawa, Machemba na wengine.

3. Walitaka utulivu na amani ili kila mmoja awe mpole katika aneo lake hivyo ilibidi kushirikiana na wakoloni hao katika kuhakikish amambo hayo mawili.

4. Hii ndo twasema kutojitambua au kujidharau au kwa kiingereza twasema ni "ignorance" na ambayo inamkumba kila mara Chifu Mangungo wa Msovero. Chifu Mangungo hakuelewa ulaghai wa walokoni khasa Carl Peters ambae ndie alietumwa kwenda kwake. Hivyo alipomuona aja na zawadi kemkem, mzee wa wtu akachanganyikiwa na alipopewa mkataba asaini haikuwa jabo gumu.

Na si tu Chifu Mangungo hata machifu wa washona na ndebele pia nao walikubali vijizawadi na kulaghaiwa kisha kutia saini mikataba hewa walopewa na jasusi mwingine aitwae John Moffat. Chifu Lobengula alisaini mikataba zaidi ya mitano katika vipindi tofauti kati ya mwaka 1850 na 1890 akisaini na majasusi kama huyo Moffat, Grobbler, Lippart na Rudd.

Ndo kusema hadi leo bado zawadi zaja kwa aina tofauti na ukishindwa kugundua nini kilicho nyuma ya zawadi hizo kinotokea mwisho ni majanga.

Lakini mwisho. sisi waafrika tuna mengi ya kujifunza na hadi leo bado twapata fursaq zaidi za kujifunza kuwa ni nani khasa alikuwa ni kiongozi imara aliekataa zijizawadi ka kuuza ardhi yake. Je, ni akina Mtemi Mirambo, Chifu Mkwawa na Kinjekitile Ngwale na kwamba je. ni kwanini Chifu Mangungo alikuwa ni kiongozi dhaifu ambae alikubali kulaghaiwa tena mbele ya washauri wake wa karibu na kuamua kutia saini mkataba wa kilaghai wa wawakilishi wa wakoloni wa kijerumani?
 
Yes hao ni watumwa tu
 
Haujawasaidia kitu hao wakenya ndio maana bado kuna ukabila na wakenya wengi wanakimbilia ughaibuni kwenda kuwa watumwa mambo Leo (Diaspora )
 
Historia ya Tanzania haina ukweli hata chembe! Nilishangaa sana walipodanganya eti Nyerere alizaliwa Butiama? Eti Nyerere babake ni mzee Burito? Yule mzee siyo damu ya Mzanaki, sema wenzetu wakishatoa mahari mtoto yeyote atakayezaliwa anakuwa mali yao!😁😁😁
 
Ipi tofauti baina yao hali wote wanashikilia uchumi wa nchi.
Kwangu bora ya wakoloni kuliko wawekezaji
Mi nilishindwa kumjibu mana niliona kaja kama mwalimu wa history na anataka tujadili mambo kama anavyoyafundisha yeye huko shuleni.
 
Huyo mkalimqni alisoma wapi kijerumani? Mgeni au mwenyeji? Hapa ndipo tu narudi kule kule alisomeshwa tu
Muhimu jua

Karl peter aliishi London miaka mingi alikojifunza falsafa za ukoloni . Kwahiyo alijua kuongea kingereza vizuri. Alifijia Zanzibar na kumpata mkalimani anaitwa Ramadhani. Uwezekano wa Ramadhan kujua kingereza upo kutokana na Zanzibar kutembelewa na watu wa maeneo tofaut tangu karne za mwanzano. Pia Ramadhani kufaham kiswahili inawezekana kutokanana ushahidi unaonesha Zanzibar wameanza kizungumza kiswahili mapema sana
Ko mangungo tuseme tu alisaini kitu anachokielewa.
 
Na swali jingine ni hili: Hawa "wasomi" wetu wanaosaini mamikataba haya mabovu na kuuza madini, gesi na wanyama wetu kwa wazungu nao ni akina Mangungo? Hawajui kusoma na kuandika kama Mangungo?
Ukijadili mikataba ya sasa unatoka kwenye historia na kurudi kwenye siasa.
Na swali jingine ni hili: Hawa "wasomi" wetu wanaosaini mamikataba haya mabovu na kuuza madini, gesi na wanyama wetu kwa wazungu nao ni akina Mangungo? Hawajui kusoma na kuandika kama Mangungo?

Kitendo cha kuwapokea wazungu nimekizungumzia kama kukaribisha wawekezaj.
Kitendo cha kuishi nao vizuri tumekizungumzia kama mwanadiplomasia.
Kitendo cha kusaini mikataba mbele ya ramadhan na familia yake tunaona namna Mangungo alivyokuwa muwazi kwenye mikataba yake.
Kama mangungo mjinga kweli kama mnavyoamini na mkataba wake ulikuwa wa wazi sasa kwanini hawa wajanja wenu wa leo mikataba yao ni ya siri wakati ni mikataba ya KIJANJA ??
Jambo la msingi ni aidha tumtoe Mangungo kwenye kundi la viongozi wajinga tumweke kwenye kundi la viongoz walio harakisha uwekezaji ( viongoz wajanja) au viongozi wa kiafrika wa leo tuwaweke kundi moja na Mangungo jambo ambalo watu wanapinga kwa kusema ukolon si sawa na uwekezaji wa leo.
Na ikumbukwe tukisema hakuna maendeleo bila wazungu kama alivyoamini mangungo na viongoz wa leo, maana yake wapigania uhuru ni kama waliwafukuza wawekezaji. Kwasababu viongoz wa leo wanapata tabu kuwarudisha wazungu kufanya jambo lilelile walilokuwa wanashirikiana na mangungo. Au labda tuseme viongozi wa leo wao wanaboresha kwenye vipengele alivyopigwa Mangungo
 
Mkuu hongera kwako kwa kuielikisha jamii, na hapo watu hawata kuelewa kwasababu walishaminishwa tofauti
 
Hapana mkuu, mtazamo tu kuwa miundombinu kurahisisha uzalishaji wake bali kuwahudumia wafanyakazi wake hata sasa ukienda Mtibwa kuna zahanati ndani ya kiwanda kwa jamii iliyopo ndani ndio hunufaika.
Kwamifano hai kuonesha kunufaika kwa wakazi wake watu wengi kutoka iringa walikuja wao kwa hiari yao kuja kufanya kazi na walipo rudi walirudi na majina ya huko km Ludewa, Mlangali na malangali
 
Shida ni kwamba kila walichokuwa wanakizalisha kilipelejwa Nje kwenda kutengeneza material ya kutumia. Vibarua wa Kiafrika walifanya kazi Kwa mazingira magumu na ujira mdogo. Kila walichokifanya ni Kwa manufaa Yao na sio Kwa mwafrica
Ulitaka wanufaike vipi zaidi ya Mshahara?
 
Mbona Nyerere bado anatukuzwa na madudu yake
 
Sio wapigania uhuru sema wachumia tumbo
 
Tukiruhusu fikra huru tuna sababu za msingi za kuhoji ujinga wa Chief Mangungo kama historia inavyodai.

Tunahitaji kuheshimu maamuzi ya Mangungo na labda kumuweka kwenye kundi la mashujaa waliochagua amani na sio vita..Kuchagua amani sio ujinga.

Historia imewapa ushujaa viongozi waliopambana na kumwaga damu na wengine kujiua kabla ya kushikwa na wakoloni kama Mkwawa, Isike, Abushiri, Bwana kheri, Makung'anya, Mangi Meli, Mangi sina, na Kinjekitile Ngwale. Huku ikiwanyima ushujaa viongozi waliochagua amani na diplomasia kama Mangungo na Rumanyika....zaidi Mangungo ati alisaini mkataba wa kilaghai.

Kwanini tunatakiwa kumjadili upya Mangungo?

Mangungo alikuwa muwazi...Mkataba na Carl Peters ulisainiwa mchana kweupe mbele ya mashahidi wa pande zote na mkalimani aliyeongea kiswahili ambacho upande wa Mangungo ulikielewa...sasa vitabu vingi vya historia yetu vinasema Mangungo alisaini mkataba asioelewa maana yake na kwa lugha ya kigeni ambayo hakuielewa...Kuna upotoshaji hapa au utafiti hafifu.

Baada ya Carl Peters kurudi kutoka Ujerumani akiwa ameiunda GEACO na ukoloni kuanza, mangungo na watu wake hawa kuanzisha vita kupinga ukoloni kwa muda huo. Hii ina maana kwamba baadhi ya makubaliano yalitimizwa ikiwamo ujenzi wa miundo mbinu na huduma nyingine za kijamii hata kama interest kubwa ilikuwa kwa mkoloni...Kama Mangungo angestuka kuona makubaliano hayatekelezwi basi ni wazi angeanzisha mapigano kama walivyofanya Samori Toure wa Mandika na Lobengula wa Washona wa Zimbabwe...hawa waliingia makubaliano baadae wakagundua dhuluma na kuanzisha vita.

Mkondo aliouchukua Mangungo ni kama ule aliouchukua Nyerere wakati wa kudai uhuru...Mangungo alitumia diplomasia, hakutaka bloodshed kama Nyerere alivyofanya. Wakati kina Mwai Kibaki, Ahmed Sekou Toure, Samu Nujoma, Eduado Mondlane, Samora Machel nk wakidai uhuru kwa nguvu, Julius Nyerere alichagua diplomasia na hakutaka bloodshed. Tunamuitaje Mangungo mjinga hapa?

Tofauti ni zama tu lakini content ya mkataba wa Mangungo na mikataba mingi ya sasa ni yaleyale...Mangungo alisaini kuukubali ukoloni, viongozi wa sasa wanasaini kuukubali Ukoloni mamboleo.


Guevara Jr
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…