Waafrika tulipotoshwa kuhusu Chifu Mangungo wa Msovero sio mjinga, Watanzania tuiombe familia yake msamaha na tumuenzi kama shujaa wa uwekezaji

Waafrika tulipotoshwa kuhusu Chifu Mangungo wa Msovero sio mjinga, Watanzania tuiombe familia yake msamaha na tumuenzi kama shujaa wa uwekezaji

Tukiruhusu fikra huru tuna sababu za msingi za kuhoji ujinga wa Chief Mangungo kama historia inavyodai.

Tunahitaji kuheshimu maamuzi ya Mangungo na labda kumuweka kwenye kundi la mashujaa waliochagua amani na sio vita..Kuchagua amani sio ujinga.

Historia imewapa ushujaa viongozi waliopambana na kumwaga damu na wengine kujiua kabla ya kushikwa na wakoloni kama Mkwawa, Isike, Abushiri, Bwana kheri, Makung'anya, Mangi Meli, Mangi sina, na Kinjekitile Ngwale. Huku ikiwanyima ushujaa viongozi waliochagua amani na diplomasia kama Mangungo na Rumanyika....zaidi Mangungo ati alisaini mkataba wa kilaghai.

Kwanini tunatakiwa kumjadili upya Mangungo?

Mangungo alikuwa muwazi...Mkataba na Carl Peters ulisainiwa mchana kweupe mbele ya mashahidi wa pande zote na mkalimani aliyeongea kiswahili ambacho upande wa Mangungo ulikielewa...sasa vitabu vingi vya historia yetu vinasema Mangungo alisaini mkataba asioelewa maana yake na kwa lugha ya kigeni ambayo hakuielewa...Kuna upotoshaji hapa au utafiti hafifu.

Baada ya Carl Peters kurudi kutoka Ujerumani akiwa ameiunda GEACO na ukoloni kuanza, mangungo na watu wake hawa kuanzisha vita kupinga ukoloni kwa muda huo. Hii ina maana kwamba baadhi ya makubaliano yalitimizwa ikiwamo ujenzi wa miundo mbinu na huduma nyingine za kijamii hata kama interest kubwa ilikuwa kwa mkoloni...Kama Mangungo angestuka kuona makubaliano hayatekelezwi basi ni wazi angeanzisha mapigano kama walivyofanya Samori Toure wa Mandika na Lobengula wa Washona wa Zimbabwe...hawa waliingia makubaliano baadae wakagundua dhuluma na kuanzisha vita.

Mkondo aliouchukua Mangungo ni kama ule aliouchukua Nyerere wakati wa kudai uhuru...Mangungo alitumia diplomasia, hakutaka bloodshed kama Nyerere alivyofanya. Wakati kina Mwai Kibaki, Ahmed Sekou Toure, Samu Nujoma, Eduado Mondlane, Samora Machel nk wakidai uhuru kwa nguvu, Julius Nyerere alichagua diplomasia na hakutaka bloodshed. Tunamuitaje Mangungo mjinga hapa?

Tofauti ni zama tu lakini content ya mkataba wa Mangungo na mikataba mingi ya sasa ni yaleyale...Mangungo alisaini kuukubali ukoloni, viongozi wa sasa wanasaini kuukubali Ukoloni mamboleo.

Guevara Jr
Mangungo ni kiongozi bora sana kuwahi kutokea. Kwa zama zake . Sema mtunzi wa kitabu ndio anaweza kumtengeza staa aonekane vip
 
Naona wataka kurudi tena kwenye historia ya hila za wakoloni barani Afrika ili tu kuweza kututawala.

Ukumbuke wakoloni walikuwa na njia tatu za kutaka kuitawala Afrika - kutumia majasusi kama akina Carl Peters, kugombania na kisha kuamua kukaa Berlin Conference na mwisho kuanzisha utawala wa kikoloni barani Afrika.

Hii ya mwisho ya kuanzisha rssmi ukoloni Afrika isingefanikiwa bila akina Carl Peters kusafisha njia na kuketi kule Berlin Conference.

Ukumbuke utawala wa kikoloni ule wa wajerumani ulikuwa ni kati ya mwaka 1880 na 1900, lakini walipoanzisha makampuni kama GEA, mashamba makubwa na uchumi wa kijerumani na pia kupambana na wenyeji walokuwa wakipinga ukoloni, tayari walikuwa wamefanikiwa kuwalaghai hao viongozi ambao ndo walokuwa wa mwanzao kuwaruhusu hao wakoloni.

Pia wazungumzia diplomasia ya hayati Nyerere katika kushirikiana na wakoloni hii ilikuwa ni katika azma ileile ya kuwaondoa hawa kuitawala Afrika na hizi resistance zisingeweza kufanikiwa kama kusingekuwa na nia ya dhati ya kutaka kujitawala wenyewe.

Ila usipotoshe kuwa Chifu Mangungo alitumia diplomasia kwa kukubali ulaghai wa Carl Peters na kusaini mkataba ambao haukuwa na uhalali wowote, tena baada ya kukubali vijizawadi.

Hili ni somo zuri ambao Mwanafunzi Mtoro kalileta tujadili kwa makini.
 
hata atende mema kumzidi Musa bado kuna siku atafumba. Macho.
Halafu weye Babu Msagara una tatizo la kudumu daamuni...Nani alikwambia Musa alifumba macho??...wewe kama utafumba siyo woote watafumba!......sisi tutaendelea kuishi ktk ulimwengu mwingine!

unaelewaje fungu la ........''ili kila amwaminiye apate uzima wa Milele?.......
Hapa hatupo kulinganisha awamu ya tano na ya sita.
Babu umedandia uzi, rudia tena ukasome ndo ujue kwa nini nimelinganisha na uongozi wa sasa! au umelewa??
Unaonekana unakazi maalumu hapa JF???

Geuka nyuma angalia kwenye ubao .Kama jina lako sio la kwanza pia haliwezi kuwa la mwisho.
Afu weee Babu ntakupiga ngumi ujue?? nani asiyejua kazi ni msingi wa Maendeleo??..........jina na mie wapi na wapi?? CHIFU MANGUNGO ALIKUWA chief mzembe sana! tunachekwa huko nje ya nchi! mpaka leo!

Hana tofauti na Kambona , Babu, ntuntemeke sanga! sijui haya maeneo yana shida gani yaani ni mtindo wakutoa viongozi vilaza tyuuuuu! mpaka leo! mnakulaga nini nyie kenge!
 
Naona wataka kurudi tena kwenye historia ya hila za wakoloni barani Afrika ili tu kuweza kututawala.

Ukumbuke wakoloni walikuwa na njia tatu za kutaka kuitawala Afrika - kutumia majasusi kama akina Carl Peters, kugombania na kisha kuamua kukaa Berlin Conference na mwisho kuanzisha utawala wa kikoloni barani Afrika.

Hii ya mwisho ya kuanzisha rssmi ukoloni Afrika isingefanikiwa bila akina Carl Peters kusafisha njia na kuketi kule Berlin Conference.

Ukumbuke utawala wa kikoloni ule wa wajerumani ulikuwa ni kati ya mwaka 1880 na 1900, lakini walipoanzisha makampuni kama GEA, mashamba makubwa na uchumi wa kijerumani na pia kupambana na wenyeji walokuwa wakipinga ukoloni, tayari walikuwa wamefanikiwa kuwalaghai hao viongozi ambao ndo walokuwa wa mwanzao kuwaruhusu hao wakoloni.

Pia wazungumzia diplomasia ya hayati Nyerere katika kushirikiana na wakoloni hii ilikuwa ni katika azma ileile ya kuwaondoa hawa kuitawala Afrika na hizi resistance zisingeweza kufanikiwa kama kusingekuwa na nia ya dhati ya kutaka kujitawala wenyewe.

Ila usipotoshe kuwa Chifu Mangungo alitumia diplomasia kwa kukubali ulaghai wa Carl Peters na kusaini mkataba ambaop haukuwa na uhalali wowote, tena baada ya kukubali vijizawadi.

Hili ni somo zuri ambao Mwanafunzi Mtoro kalileta tujadili kwa makini.
Ancient Egypt ilitawala Atlantidas yoote ni wamisri wakazi wake, Ulaya yooote hiyo usiwaone wajanja vile lkn walikuwa chini ya Mweusi Wa Misri pure!! mpaka kuleee USA ya leo!!

Wana sayansi wooote km Archimedes, Dalton, nk walisomea Misri! ....lkn alicho kifanya Mzungu alifuta kumbukumbu zooote za kinyonge za kutawaliwa na watu weusi!..kwa faida za vizazi vyao! na

kamwe weusi hamtayajua haya Makuu yenu kwa sababu mkijua tuuu.... mtakuwa hamkamatiki tena kwa kiburi bin jeuri........hii ni siri isipokuwa sisi wachache tu, twajua...!

Ebu fikiria tu, utakapo jua kuwa wewe ulikuwa kitukuu cha Farao Ramse...aliye shindana na Mungu si utapanda watu vichwani weye??
 
Mbona mzee Mohamed Said akiwaambia hata hao machifu wenu mashujaa kina Mkwawa na Songea mbano. Walikuwa waislam mnambishia wakati kila kitu kinajionesha kwamba waarabu walishirikiana na machifu katika biashara na mambo ya kiimani.

Kabishane na wengine
 
Halafu weye Babu Msagara una tatizo la kudumu daamuni...Nani alikwambia Musa alifumba macho??...wewe kama utafumba siyo woote watafumba!......sisi tutaendelea kuishi ktk ulimwengu mwingine!

unaelewaje fungu la ........''ili kila amwaminiye apate uzima wa Milele?.......

Babu umedandia uzi, rudia tena ukasome ndo ujue kwa nini nimelinganisha na uongozi wa sasa! au umelewa??

Afu weee Babu ntakupiga ngumi ujue?? nani asiyejua kazi ni msingi wa Maendeleo??..........jina na mie wapi na wapi?? CHIFU MANGUNGO ALIKUWA chief mzembe sana! tunachekwa huko nje ya nchi! mpaka leo!

Hana tofauti na Kambona , Babu, ntuntemeke sanga! sijui haya maeneo yana shida gani yaani ni mtindo wakutoa viongozi vilaza tyuuuuu! mpaka leo! mnakulaga nini nyie kenge!
Yani Kambona alikuwa kilaza? Are you serious?
 
Yani Kambona alikuwa kilaza? Are you serious?
Eeee! Bana weee!! sijakosea kabisa sasa km siyo kilaza, katusaidia nini humu Tanzania! Africa??!!....leo hii vitukuu vyake vinasafiri kutoka Bambabey mpaka Tarime kwa Lami tupU ambayo hakushiriki kuijenga!! Muzee!.............

hana la kukumbukwa msaliti yule! yaani kwa sababu ni babu yako baaaasi...........fikiria mtu aliye tukimbia maatizo yetu, tukamuimba weee!! bila hata kujisikia aibu! alirudi?? angekomaa na sisi humu tuone!!

Hata Mtakatifu nyerere alifungwa na Mkoloni, Alikumbana na hatare ya kupinduliwa kabisaaa, naMapinduzi jua kabisa kile ni kifooooo!! na alikuwa na uwezo wa kukimbia nchi tena akaishi huko vizuri tu.......

lkn kidume cha Mara kile kikasema noooo! ntafia humu humu,........ Haya huyoooo kaachia ngazi akaitwa kwa kuombwaaa na Mabepari njoo huku Uswiss uishi!! aka sema nooooooooo!
 
Ancient Egypt ilitawala Atlantidas yoote ni wamisri wakazi wake, Ulaya yooote hiyo usiwaone wajanja vile lkn walikuwa chini ya Mweusi Wa Misri pure!! mpaka kuleee USA ya leo!!

Wana sayansi wooote km Archimedes, Dalton, nk walisomea Misri! ....lkn alicho kifanya Mzungu alifuta kumbukumbu zooote za kinyonge za kutawaliwa na watu weusi!..kwa faida za vizazi vyao! na

kamwe weusi hamtayajua haya Makuu yenu kwa sababu mkijua tuuu.... mtakuwa hamkamatiki tena kwa kiburi bin jeuri........hii ni siri isipokuwa sisi wachache tu, twajua...!

Ebu fikiria tu, utakapo jua kuwa wewe ulikuwa kitukuu cha Farao Ramse...aliye shindana na Mungu si utapanda watu vichwani weye??
Tia neno kwenye mada mkuu, hizi porojo zingine ni kwa mada ingine.

Twamwongelea Chifu Mangungo kwamba kusaini mkataba wa kilaghai alopewa na Carl Peters ilikuwa ni udhaifu, au ujinga (kutofahamu kusoma na kuandika) ama kutojitambua au ilikuwa ni njia mojawapo ya kuvuta uwekezaji wa kikoloni kama anavyodai Mwanafunzi Mtoro.
 
Chifu mangungo hakuwa mjinga, watanzania tulipotoshwa, tunapaswa kuiomba familia yake msamaha

Kwa miaka mingi sana chifu mangungo ameendelea kuonekana kama mfano wa kiongozi mjinga hasa pale linapotokea swala la mikataba. Lakini je Mangungo alikuwa mjinga kweli?

Chifu mangungo ni nani?

Naomba ninukuu kidogo kipande cha historia fupi kuhusu chifu Mangungo kutoka katika uzi wa ndugu humu Jf KILABA

"Mangungo simultaneously for all his people and Dr. Peters for alt his present and future associates hereby concluded a treaty of Eternal Friendship.

Mangungo offers all his territory with all its civil appurtenances to Dr. Karl Peters, as the representative of the Society for German Colonization, for the exclusive and universal utilization for German colonization.

Dr. Karl Peters, in the name of the Society for German Colonization declares his willingness to take over the territory of the Sultan Mangungo with all rights for German Colonization subject to any existing suzerainty of Mwenyi Sagara.

In pursuance thereof, Sultan Mangungo hereby cedes all the territory of Msovero, belonging to him by inheritance or otherwise for all time, to Dr. Karl Peters, making over to him at the same time all his rights.

Dr. Karl Peters in the name of the Society for German Colonization undertakes to give special...attention to Msovero when colonizing Usagara.

This treaty has been communicated to the Sultan Mangungo by the interpreter Ramzan in a clear manner and has been signed by both sides, with the observation of the formalities valid in Usagara the Sultan on direct enquiry having declared that he was not in anyway dependent upon the Sultan of Zanzibar, and that he did not even know the existence of the latter.

Sgd. Dr. KARL PETERS
Sgd. MANGUNGO

This contract has been executed legally and made valid for all time before a great number of witnesses, we testify herewith:
Kwagakinga (mark);
Sultan Mangungo’s son of Golola (mark);
Sultan Mangungo’s second son of Draman (mark);
Graf Pfeil August Otto;
Mark of the intepreter Ramazan etc.
Dr. Karl Juhlke.
Msovero Usagara November 29, 1884.

Kwa tafsiri isiyo rasmi, kwa Kiswahili unasomeka hivi:
Mangungo, Sultan wa Msovero katika Mwenyisagara, na Dk. Karl Peters. Mangungo sambamba na watu wake wote na Dk. Peters kwa niaba yake na washirika wake wengine wajao kwa pamoja wanaweka mkataba wa Urafiki wa Kudumu.

Mangungo amekubali kutoa himaya yake yote pamoja na watu wake na hadhi yake kwa Dk. Karl Peters, kama mwakilishi wa Umoja wa Ukoloni wa Kijerumani (Society for German Colonization), kwa ajili ya matumizi ya moja kwa moja ya koloni la Kijerumani.

Dk. Karl Peters, kwa niaba ya jina la Umoja wa Ukoloni wa Ujermani anatangaza dhamira yake ya kuitwaa himaya yote ya Sultan Mangungo na haki zote kwa ajili ya Koloni la Ujerumani inayohusisha kila kona na amali za Mwenyi Sagara.

Katika kutekeleza hilo, Sultan Mangungo anakabidhi himaya yote ya Msovero, inayomilikiwa na yeye mwenyewe kwa urithi au kwa namna yoyote ile kwa nyakati zote, kwa Dk. Karl Peters, na wakati huo huo kumkabidhi haki zake zote.

Dk. Karl Peters kwa niaba ya Umoja wa Ukoloni wa Kijerumani anakusudia kuweka mkazo maalum kwa eneo la Msovero wakati wa kuitawala Usagara.

Mkataba huu umewasilishwa kwa Sultan Mangungo na mkalimani Ramzan katika dhana ya wazi kabisa na umesainiwa na pande zote, kwa kuzingatia taratibu zilizopo katika Usagara, Sultan baada ya kuhojiwa moja kwa moja alikiri kwamba hakuwa na ushirika ama kutegemea kwa namna yoyote Sultan wa Zanzibar, na kwamba hakuwa hata akimfahamu.

Imesainiwa. Dk. KARL PETERS
Imesainiwa. MANGUNGO

Mkataba huu umefanyika kihalali kabisa na umehuishwa kwa nyakati zote mbele za mashahidi wengi, ambao tunakiri hapa:
Kwagakinga (dole gumba);
Golola mtoto wa Sultan Mangungo (dole gumba);
Draman mtoto wa pili wa Sultan Mangungo (dole gumba);
Graf Pfeil August Otto.
Dole gumba la mkalimani Ramazan etc.
Dk. Karl Juhlke.
Msovero Usagara Novemba 29, 1884.

KWANINI MANGUNGO ALIONEKANA MJINGA?

Historia ilipoandikwa baada ya kupata uhuru , iliwahesabu watu wote waliopambana na wazungu kama mashujaa mfano Mkwawa. Bila kujali utawala wa hao machifu kama ulikuwa wa haki au laa. Historia haikutazama watawala hawa machifu kama watu walio pambania madaraka yao bali inawahesabu kama mashujaa kwa kuwa ilipambana tu mzungu.

Baada ya uhuru watu walisoma hadithi kama "KIBANGA AMPIGA MKOLONI". waliosoma kwa kipindi hicho walimuona Kibanga kama shujaa kwa kumpiga mzungu ( mkoloni). Lakini je Kibanga wa mwaka 1960 bado ni shujaa leo hii au ataonekana anafukuza "WAWEKEZAJI" ?

Kwahiyo kama KIBANGA alionekana shujaa kwa kumpinga mkoloni kipindi cha kutaka kujitawala ni wazi historia yoyote iliyoandikwa kwa kipindi hiko ingemtazama mtu yeyote yule aliyeshirikiana na wakoloni kipindi wanaingia Afrika kama mtu mjinga na msaliti kwa jamii yake.

KWANINI NASEMA MANGUNGO SIO MJINGA?

Kilichotokea kati ya Mangungo na machifu wengine waliopigana na wazungu ni uelewa tu. Mangungo aliona mbali ambapo wengine hawakuona kwa kipindi kile. MANGUNGO aliwaona wazungu kama wawekezaji mapema sana kuliko machifu wenzake. Kile alichokifanya Mangungo kuwaona wazungu kama wawekezaji ndio hiki tunakiona leo na sisi kuwa wazungu wanauwezo wa kuwekeza katika nchi zetu za kiafrika na uchumi ukakua.

JE MANGUNGO ALIAHIDIWA NINI KWA WAZUNGU?

Binafsi naamini tofauti na mkataba wa kuichukua ardhi na kiutawala tunaoambiwa kuwa ndio huo MANGUNGO alisaini lakini inaonesha wazi kwamba Mangungo alielezwa kuwa kama wazungu watalichukua eneo basi watakuja na mamba yafuatayo ;

mashine ( matreka) za kilimo kama treka nk

Ujenzi wa hospital za kisasa kwa (kipindi hicho)

Ujenzi wa shule

Ujenzi wa maghala ya kuhifadhia chakula

Ujenzi wa barabara

Ujenzi wa mabwawa ya kuzalisha umeme

Ujenzi wa reli ya kisasa kwa wakati huo

Ujenzi wa madaraja katika maeneo yasiyopitika kipindi cha masika

Upatikanaji wa huduma za maji safi .

Je upi unaweza kuwa uthibitisho wa hizo ahadi hadi kupelekea MANGUNGO kukubali?

Ukilitazama vizuri hilo eneo la Msovero ambalo ndio inaelezwa kuchukua eneo kubwa la KILOSA ya leo utagundua yafuatayo.

Maeneo mengi ya wilaya hiyo yana mashamba makubwa ya mkonge yaliyolimwa na mwekezaji wa Mangungo. Kuanzia Msowero ya leo , Gairo, Kimamba, Ludewa, Kilosa mjini ya leo, Chanzuru, Kivungu, Zombo , Mikumi, Kilangali , Malangali ,Ngaite, Melela Mvomero inayopakana na kilosa , ILONGA had maeneo ya dumila nk

Hayo ni maeneo machache sana yanayoonesha mwekezaji alitekeleza kweli ahadi yake ya kuinua kilimo.

Maeneo ya Kilosa mengi yalijegwa hospital. Mfano hospital ya Kilosa , Kimamba , vituo vya afya kama maeneo ya Ludewa , Mkata , na vingine ambavyo vilijegwa na wajerumani . Hivyo vitu havikuwepo kabla ya mkataba wa MANGUNGO.

Uwepo wa barabara kama ya kutoka Kilosa hadi Mikumi kupitia Zombo, barabara ya kutoka Kilosa hadi Morogoro mjini kupitia Mkata na ile kupitia Ludewa ni ushahidi tosha kuwa mwekezaji alifanya yale aliyoahidi mbele ya chifu Mangungo.

Uwepo wa njia ya reli inayopita tokea Morogoro mjini pale kichangani na kupita maeneo kama Mkata, Kimamba, Kilosa mjini ya sasa, Mkadage huko hadi Pwaga na kuingia Mpwapwa hii inaonedha jinsi gani mkataba wa chifu Mangungo na machifu wa kiluguru na wa kizingua ulizaa matunda kwa maeneo yao kiuwekezaji.

Uwepo wa shule ya KIZUNGUZI (kizu boys)

Ajira kwa vijana Uwepo wa huduma za malazi kwa wafanyakazi. Ajira ilipatikana kwa manamba japo mshahara haukuwa mkubwa lakini ukibadili thamani ya mshahara wa kipindi hicho unafanana na baadhi ya mishahara ya baadhi ya watu wanaolipwa hivi leo. Si kwamba hata hivi leo watu hawalalamiki udogo wa mishahara.

Nyumba za watumishi zilijegwa kila kwenye stesheni , kwenye kila kituo chao cha kukusanyia mikonge mfano Kimamba, ludewa , Chanzuru Msiwero , Kivungu nk. Hapa inaonesha ni jinsi gani mkataba aliosaini abwana mangungo haukuwa mbaya kama tunavyoaminishana leo hii.

Bado kama hayo hayatoshi ukipita maeneo ya Ilonga utaona jinsi wajerumani walivyopaendeleza katika kilimo na vituo vya utafiti wa kilimo walijenga ( hapa mtanikosoa kama walijenga wajerumani au waingereza).

Kwa wale watu walio bahatika kuishi Sagara ya zamani au Kilosa ya leo wanaweza kuwa mashahidi . Mji wa kilosa wa leo unaoneka ni mji uliokuwa wa kifahari enzi ya wawekezaji wa Mangungo ( ambao waliitwa wakoloni hapo awali) kabla ya kubadilishwa jina tena na kuitwa wawekezaji kama alivyowaita Mangungo na kizazi cha sasa . Kilosa ulikuwa mji kimbilio la wageni toka mikoa mbali mbali Tanzania. Usifikiri katika "engo" ya manamba kupata mchanganyiko wa kabila katika eneo la kilosa bali hata huduma ziliwavuta vijana wa zamani kwenda kuishi Kilosa.

Je kunyonywa kiuchumi ndio kunatufanya tumuone Mangungo alikuwa mjinga?

Binafsi namuona Bwana Mangungo kama kiongozi aliyeuona uwekezaji tangu mapema. Kwani kama kuhusu kunyonywa bado hadi leo kama taifa bado tuna mikataba mingi ya kinyonyaji isiyoacha alama kwa taifa kuliko ile ya msovero iliyoacha hata reli ,magofu ya nyumba na hospital.
Wapo watakaosema ujinga wa Mangungo ni kuiachia ardhi kwa wazungu kulima pamba na mikonge huku wenyeji kuishi kwa njaa. Binafsi naamini kwa nyakati hizo kulikuwa na watu wachache sana wenye uwezo wa kulima mamia ya ekari kama wawekezaji. Wengi walilima kujikimu kwani ni miaka zaidi ya 70s sasa tangu Mzungu atuachie ardhi yetu lakini kuna maeneo tangu kuumbwa kwa dunia hayajawahi kulimwa na wazawa. Vijana wanashinda kwenye vituo vya kubeti huku redio zikihamasisha nguvu ya buku katika kushinda kamali. Kwa mawazo kama hayo hatuoni kama bwana Mangungo aluoba mbali kuingia mikataba na wawekezaji?

Wapo watakaosema ujinga ni kuwa alisaini bila kuelewa chochote . Binafsi naona si kweli, kwani kama ni kweli Mangungo alisaini kitu asichoelewa historia ingeonesha kutokea mgogoro baina ya mwekezaji na Mangungo. Katika hali ya kawaida mtu akwambie muingie makubaliano ya kulichukua eneo lako lote la ardi na kiutawala na ukakubali bila kumuuliza shughuri atakazofanyia eneo lako. Pili, mkata ulisainiwa kisha Karl na wenzake wakaondoka kurudi Ujerumani . Kama wangekuwa ni walaghai basi pale waliporudi kutekeleza uwekezaji wao lazima pangetokea ugomvi na kutoelewana. Maana katika hali ya kawaida ukimpa mtu eneo alime au akae alafu ghafla unamwona anakuja na fundi wake wanajenga nyumba , hospitali, reli bila kwenda kuwahoji.

MANGUNGO ALIKUWA KIONGOZI MWANADIPLOMASIA

Kwajinsi sasa jamii ya Kiafrika inavyomsifu kiongozi mwenye mahusiano mazuri na wazungu kama kiongozi bora na mwanadiplomasia basi ni wazi Mangungo alikuwa nguli zaidi kama mwanadiplomasia wa mwanzoni kabisa.

NINI WITO WANGU KWA JAMII

Niwakati sasa wa jamii yetu kubadili mtazamo juu ya chifu Mangungo kwa kumchukulia kama kiongozi mjinga na kumwona kama kiongozi wa mwanzoni kuhamasisha uwekezaji nchini. Kumwona Mangungo kama kiongozi mjinga kumeifanya hata familia yake isijulikane leo hii ksma zinavyojulikana familia za ma chifu wengine. Kwakuwa sasa viongozi wetu wamerudi kule kule kuwapokea wazungu na kufanya nao shughuri za maendeleo kama ujenzi wa miundombinu ya maji , barabara, reli, hospitali, na shule jambo ambalo hata Mangungo ndilo alilifanya kwa ustadi basi hatuna budi kumuenzi Mangungo kama mwasisi wa uwekezaji nchini.
Natamani sasa hata familia yake iliyobaki tuiombe msamaha kama taifa kwakuwa tulilewa mvinyo wa uhuru kiasi ya kuwaona waliopinga kushirikiana na wazungu kuwa ndio MASHUJAA.

Nawasaliim
GREAT THINKER ,binafsi kwa bandiko hili Mangungo aombwe msamaha kule alipo na yoyote aliyemtumia kama reference ya mikataba mibovu.
 
Mi nilishindwa kumjibu mana niliona kaja kama mwalimu wa history na anataka tujadili mambo kama anavyoyafundisha yeye huko shuleni.
Labda maswali yangu yalikuwa magumu sana na yangevuruga narrative yako kwa hiyo umeona mwl wa historia ndio kichaka cha kujificha. Rudi kajibu maswali yangu. Mimi sio mwalimu wa historia.

Nimenukuu ulichokiandika na nikahoji kama unavyohoji. Unfortunately unaona una haki ya kuhoji historia ya vitabuni ila for some reason unadhani hoja zako hazitakiwi kuhojiwa, else anayehoji atakuwa mwalimu wa historia!
 
Tia neno kwenye mada mkuu, hizi porojo zingine ni kwa mada ingine.

Twamwongelea Chifu Mangungo kwamba kusaini mkataba wa kilaghai alopewa na Carl Peters ilikuwa ni udhaifu, au ujinga (kutofahamu kusoma na kuandika) ama kutojitambua au ilikuwa ni njia mojawapo ya kuvuta uwekezaji wa kikoloni kama anavyodai Mwanafunzi Mtoro.
Mbona mzee Mohamed Said akiwaambia hata hao machifu wenu mashujaa kina Mkwawa na Songea mbano. Walikuwa waislam mnambishia wakati kila kitu kinajionesha kwamba waarabu walishirikiana na machifu katika biashara na mambo ya kiimani.

Kabishane na wengine
wale hawambishii Mzee mohamed bali wana muelimisha! kuwa Uislamu ulikuwa ni Dini ya kitumwa hata watemi nguri na akina mkwawa waaliukataa! lkn kuupeleleza uislamu ili kuujua siyo kuwa sasa umekuwa Mwislamu!
 
GREAT THINKER ,binafsi kwa bandiko hili Mangungo aombwe msamaha kule alipo na yoyote aliyemtumia kama reference ya mikataba mibovu.
Si Chifu Mangungo pekee ambae alitia saini mikataba ya kilaghai kwa niaba ya wananchi wake na maeneo yote waloyamiliki.

Wapo machifu wengine nilowataja hapo juu ambao nao baadae walipojitambua kama yule wa Shona na Ndebele wakaamua kupigana na akina Cecil Rhodes kurudhisha ardhi zao.

Ardhi ya kabila ya Wandebele ilisheheni dhahabu kama ilivyokuwa kwa kabila la Washona na wakoloni wa kiiingereza walipogundua hiyo rasilimali wakamsainisha mikataba ya kilaghai (wale washirika wa Rhodes) Lobengula tena wakifahamu kuwa baba yake Msilikazi alikufa lakini Lobengula hakubaini ulghai huo hadi alipogundua Waingereza watangaza kumiliki eneo la migodi na ndipo vita ilipoanza.

Hii ni historia ambayo ipo na ni vizuri tukaijadili kwa makini kuhusu udhaifu wa viongozi wa wakati huo.
 
wale hawambishii Mzee mohamed bali wana muelimisha! kuwa Uislamu ulikuwa ni Dini ya kitumwa hata watemi nguri na akina mkwawa waaliukataa! lkn kuupeleleza uislamu ili kuujua siyo kuwa sasa umekuwa Mwislamu!
Sawa hizo ni mada zingine turudi mada kuu
 
Tia neno kwenye mada mkuu, hizi porojo zingine ni kwa mada ingine.

Twamwongelea Chifu Mangungo kwamba kusaini mkataba wa kilaghai alopewa na Carl Peters ilikuwa ni udhaifu, au ujinga (kutofahamu kusoma na kuandika) ama kutojitambua au ilikuwa ni njia mojawapo ya kuvuta uwekezaji wa kikoloni kama anavyodai Mwanafunzi Mtoro.
siyo poroja mkuu baba!! Bali ni kuonyesha kwamba sisi weusi tulikuwa hatari sana kuliko kina karl peters hao, na tulifanya makubwa zaidi!!ya wao!! na bado tuna weza ...... lkn wanataka tujione sisi ni madhaifuuuuu!

wanatkuza watu dhaifu km kina chifu mangungo wa msovero ambao walikuwa upande wao! yaani vibaraka lkn sisi hatuwafanyi vibaraka km mfano wa kuigwa
 
wale hawambishii Mzee mohamed bali wana muelimisha! kuwa Uislamu ulikuwa ni Dini ya kitumwa hata watemi nguri na akina mkwawa waaliukataa! lkn kuupeleleza uislamu ili kuujua siyo kuwa sasa umekuwa Mwislamu!
Mkuu, tusitoke nje ya mada tunaiharibu.
 
Labda maswali yangu yalikuwa magumu sana na yangevuruga narrative yako kwa hiyo umeona mwl wa historia ndio kichaka cha kujificha. Rudi kajibu maswali yangu. Mimi sio mwalimu wa historia.

Nimenukuu ulichokiandika na nikahoji kama unavyohoji. Unfortunately unaona una haki ya kuhoji historia ya vitabuni ila for some reason unadhani hoja zako hazitakiwi kuhojiwa, else anayehoji atakuwa mwalimu wa historia!
Samahani kama jibu langu lilikukwaza mkuu. Kuhusu swali lako jibu sina. Swali lako lipo juu ya uwezo wangu kulijibu.
 
siyo poroja mkuu baba!! Bali ni kuonyesha kwamba sisi weusi tulikuwa hatari sana kuliko kina karl peters hao, na tulifanya makubwa zaidi!!ya wao!! na bado tuna weza ...... lkn wanataka tujione sisi ni madhaifuuuuu!

wanatkuza watu dhaifu km kina chifu mangungo wa msovero ambao walikuwa upande wao! yaani vibaraka lkn sisi hatuwafanyi vibaraka km mfano wa kuigwa
Hiyo ya kwamba sisi watu weusi akili tunazo hiyo haina ubishi na hadi kesho sisi ni tishio kwa hawa jamaa.

Lakini je sisi ni werevu?

Walotushinda wenzetu wote wazungu waloijenga Ulaya na waarabu waloijenga Dubai kwenye jangwa ni akili au werevu?
 
Si Chifu Mangungo pekee ambae alitia saini mikataba ya kilaghai kwa niaba ya wananchi wake na maeneo yote waloyamiliki.
Hatutaki hayooo!! hao waliotia mikataba kama hiyo ya kilaghai ni wengi tu, lakini walijua kujitetea upyaaa na kwa nguvu zote na mikataba ikafa mazimaaa!!

pale walipo gundua wamelaghaiwa mfano ni chief Malumbo wa Majita, na Majinge wa Musoma nk. huwezi kuja na kajikaratasi halafu unidanganye eti ni Mkataba,.......Hata leo!..fanya ivo uone!! ivi wewe kijana kabila gani weye!!

Richa ya maeneo hayo kuwa na dhahabu nyingi na vipusaa/watumwa, lkn Wazungu/waarabu hawakutia pua zao hovyo kuree! heee!.. eti na kikaratasi unaropoka eti ni mkataba........

walichofanywa kuree Mara ...walikuwa wanazingirwa na kuchomwa moto LIVE, then wanakula nyama zao hadharani hasa makalio yaliyo nona! kule hata utumwa ilikuwa ni mtihani!

Mkurya mmoja tu alikuwa anapiga Battalion nzima ya mzungu tena akiwa na panga/rungu tu!...ndo maana wakaenda kubembeleza wanajeshi kule wkt wa vita ya II.
 
Lakini je sisi ni welevu?

Walotushinda wenzetu wote wazungu waloijenga Ulaya na waarabu waloijenga Dubai kwenye jangwa ni akili au welevu?
Naona sasa unaanza kunielewa safi sana! ..sisi ni werevu kupita maelezo na asikudanganye mtu wazungu... waarabu wanatuogopa mno! ndo maana wanatumia nguvu nyingi kutuua

.........walioijenga Ulaya yoote .USA yoote. Dubai yako hiyo ni watumwa weusi tii!kifupi mitaifa yenye nguvu Duniani ilijengwa na watumwa weusi tuu tena!

Kutoka Africa! jiulize tu kwa nini, wauza watumwa wali Target Africa tu zaidi!! wakt kwingine kooote kuna watu?? hata alexander ali--target AFRICA kwa nini?...ubora wa Rasilimali watu...

OK! turudi kwenye mada!
 
Back
Top Bottom