Ni kweli huko nje tunabaguliwa sana na hata kutupiwa maganda ya ndizi. Lakini msiba mkubwa zaidi ni yale tunayotendeana sisi kwa sisi. Hatujaliani. Ubinafsi wa kinyama. Ni kila mtu na tumbo lake, familia yake na marafiki zake.
Fisadi mmoja anapoamua kukwapua mabilioni (na sasa tunaambiwa mpaka matrilioni ya shilingi) huku wananchi wenzake hawawezi kumudu hata mlo mmoja kwa siku; na wanaweza hata kukata roho kwa kukosa dawa ya kununua Aspirin huwa ni nini kama siyo unyani wetu na ubinafsi wa kihayawani? Kwa nini tunashangaa tukibaguliwa na hawa wazungu kama sisi kwa sisi tunatendeana unyama huu?
Halafu angalia tunavyojidharau. Utamaduni wetu hatuna. Dini zote za kuletewa. Lugha hali kadhalika. Hata rangi hii nyeusi kusema kweli hatuitaki. Yaani tupo tupo tu kama wasindikizaji hapa duniani.
Hili la kubaguliwa huko nje mimi wala halinishangazi (wala kunihuzunisha) kivile [emoji51]
View attachment 2762699