Waafrika walipelekwa utumwani Kwa nguvu, wanarudishwa tena nyumbani Kwa nguvu, Huu ni Mpango wa Mungu.

Waafrika walipelekwa utumwani Kwa nguvu, wanarudishwa tena nyumbani Kwa nguvu, Huu ni Mpango wa Mungu.

Rabbon

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2022
Posts
21,625
Reaction score
33,688
Hellow Afrika!!

Afrika na wanae wanapitishwa tena katika moto Ili kuwasaidia kurudi kuijenga Africa Yao tena,

Ni kama tu tai, akitaka kumfunza kifaranga chake kuruka, huondoa nyasi Ili miiba Imchome aruke na kuanza safari ya kujitegemea.

Wazungu wanatoka ulaya kuja kufanya KILIMO na kufungua makampuni Africa, kuchimba dhahabu ardhini,waafrika wanatelekeza utajiri ,wanazamia meli kwenda uzunguni kufaidi JASHO na utajiri wa wazungu walioupata Afrika na kurudisha nchini mwao, sasa kwanini waafrika wasijenge Nchi zao?

Kufutiwa misaada ya madawa, kufutiwa misaada na mikopo ni njia njema ingawa ni ngumu, itasaidia kuwafanya viongozi wa Afrika waache wizi wa Kodi za wananchi, matumizi ya anasa, na kutumia vyema raslimali zao kunufaisha Nchi zao.

Muda umetosha Waafrika mmepata Maarifa ya kutosha ughaibuni, fungueni kampuni mbalimbali , fanyeni tafsiri za kisomi Kwa Elimu na Maarifa mliyopata ughaibuni, ninafurahi mnaporudishwa nyumbani tena Kwa kufukuzwa maana hamkusoma alama za nyakati.

Kuna wakati Ili ufikie mafanikio Yako, ni muhimu ukataliwe, ufukuzwe KAZI, uteswe nk nk, sasa huu ni muda sahihi Mungu anataka kuiinua Africa ifikie viwango vya juu kiuchumi, kisiasa, kijamii nk nk

Mungu Mbariki Nabii wako Donald Trump.

Mungu tubariki Afrika,

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Karibuni 🙏
 
Viongozi wa Afrika Badala ya kununua madawa,

Wananunua bunduki Kwa mkopo Ili kuua wakosoaji wanaowaambia UKWELI juu ya RUSHWA na matumizi mabaya ya raslimali.

Sasa misaada inaenda kukoma.

Tusubiri
 
Naona ni kama vile umefurahi sana kwa mikakati ya Trump kurudisha nyumbani wahamiaji walioko Marekani.

Unajua kuwa wanaorudishwa ni wahamiaji haramu tu? Ni wale ambao wame-overstay visa zao mpaka zikamaliza muda wake na sasa wako huko illegally wanabangaiza tu. Kama uko legally, una Green Card au ulishachukua uraia kabisa Trump wala hakugusi.

Na kwa uzoefu wangu sidhani kama kuna Wabongo wengi ambao wako kule illegally; na hata kama wapo si wote watakamatwa na kurudishwa nyumbani.

➡️➡️➡️ Ishu ya diaspora kurudi ina changamoto zake maana ukirudi huku unachukuliwa kama adui wa mfumo na hata kupatiwa vibali utahenya sana wakati mzungu yeye anakuwa treated kama mungu-mtu; na mambo yake yatakwenda chap. Nawafahamu watu wazuri sana kwenye mambo ya IT waliojaribu kurudi na kutaka kuanzisha makampuni ya IT hapa lakini walikwama na kuamua kurudi walikotoka. Wivu. Roho mbaya. Rushwa. Unconducive business environment kwa wazawa na ishu zingine kibao. Wakati mwekezaji wa kigeni anatetemekewa balaa.

Naamini mazingira yakiboreshwa kukawa na fair playground, tunao duaspora wazuri sana ambao wanaweza kufanya makubwa kwa nchi yetu na vijana wake.
 
Watafukuzwa wengi zaidi hata wenye uraia,

Behind the scene, ni kufanya Africa ijijenge,

Mungu anataka kuisimamisha na kuitajirisha Afrika Kwa matumizi yake ya mbeleni, Kupeleka Nuru ya Injili Dunia nzima Kutokea Afrika.

Mimi naunga mkono Mpango huu.
 
Trump hana uwezo wa kuwafukuza wote. Hao illegal immigrants wapo kati ya milioni 11 hadi 20.

Pia wanahitajika kwa kazi wanazofanya.
 
Trump hana uwezo wa kuwafukuza wote. Hao illegal immigrants wapo kati ya milioni 11 hadi 20.

Pia wanahitajika kwa kazi wanazofanya.
Wataondoka maana muda umefika wa Hilo kutimia,

Afrika inaenda kujengwa Ili kuwa Taifa kubwa Moja lenye nguvu sana.

Makamo makuu ya Africa ni hapa kwetu.
 
Back
Top Bottom