Ukijiingiza kwenye information war ya identity crisis, kunakuwa na facts na wanaopinga facts kwa sababu yabidentity.
Kwenye saikolojia kuna kitu kinaitwa "cognitive dissonance". Hii hali hutokea pale mtu anapoonabukweli unapingana na imani yake, lakini anaendelea kushikilia imani yake na kupingana na ukweli.
Kwa mfano, mtu anatoka Mwenge Dar es salaam, anataka kwenda Kariakoo Dar es salaam. Lakini badala ya kuelekea kusini, anaelekea kaskazini, anapita Lugalo, anapita Kawe, anapita Tangi Bovu, anapita Africana, anapita Tegeta, anaanza kuona kama anakoenda siko, lakini anajipa moyo kwamba anaelekea upande sawa, soko la Kariakoo liko mnele kidogo tu hapo, after all, ameshasafirinumbali mrefu sana, lazima soko litakuwa karibu.
Kumbe anaelekea upande tofauti na kila anavyozidi kusafiri ndivyo anavyozidi kuliacha soko la Kariakoo mbali zaidi.
Watu wengi wanapinga ripoti za BBC kwanza bila hata kuangalia hizo video. Wanapinga kwa "identity war" tu. Ni kama mtu akimshambulia baba yako na kumuita mjinga, unaweza kupigana naye bila kujali kwamba alichosema ni kweli au la.
Hawa watu wengi wanaona baba yao TB Joshua kashambuliwa, wanaishambukia BBC. Identity war tu.
Ukifuatilia zile video, wale watu walivyoongea, walivyo wengi, walivyotoka nchi nyingi, mpaka mtoto wa TB Joshua alivyosema, jinsi TB Joshua alivyokuwa ana fake mirackes tangu zamani tunavyojua, jinsi alivyokuwa mtu wa kutafuta shortcuts mpaka akajenga ghorofa lililoanguka, jinsi alivyozuia waokoaji wasiokoe watu, jinsi wafuasi wake wa karibu walivyokubali madudu aliyoyafanya, jinsi mpaka serikali ya Nigeria ikivyokubali TB Joshua kajenga jumba kiholela.
Utaona kuwa only a fanatic fighting identity war with cognitive dissonance would defend TB Joshua.
This is identity war fueled by cognitibe dissonance.
TB Joshua tulimjua ni tapeli siku nyingi tu, kabla BBC hawajammulika.
BBC wamejazia nyama tu kwenye skeleton kwa expose yao.