Wanaotusaliti Afrika ni Wasomi na wanasiasa.
Mpaka Leo Tanzania kuna Malaria lakini miaka zaidi ya 30 kuna madaktari wanafanya tafiti na miradi ya malaria kwa mabilioni ya fedha.
Dawa ya haya yote ni kudhibiti haya maduka binafsi ya dawa ili yasiwe mawakala wa mabeberu ya kusambaza dawa.
Kuweka mkataba na watafiti wa miradi hiyo.
Kuacha tabia ya wataalam wa afya kutumia miradi kama sehemu ya kujitajirisha .
Inabidi sasa kuanza Kuwalipa wale wanaofanya utafiti Mara baada ya kukamilisha tafiti zao na kutoa matokeo chanya yenye tija kwa jamii.
Haiwezekani miaka zaidi ya 30 bado kuna mbu Tanzania.
Watu wanawaza eti miradi ya kutokomeza malaria badala ya kutokomeza Mbu.
Wataalam wetu wa afya wanafeli sana kwa sababu ya ubinafsi.
Leo hii ni vijana wa mitaani tu wanaounda vikundi vya kunyunyiza na kupuliza dawa za kutokomeza mbu; hawa ndio kidogo wamefanikiwa kupunguza mbu japo wanatumia tafiti duni na vifaa duni kwa gharama ndogo.
Sasa tujiulize wataalam wetu wako wapi? Wataalam walioshindwa kutokomeza mbu mpaka sasa ! Watawezaje kutokomeza Chinise Virus aina ya Covid 19?
Hawa wataalam wetu watatusaliti hata kwa mbinu nyingine pale tu mifuko yao itakapotunishwa na mapesa kutoka kwa mabeberu.
Zika haijapatiwa jibu mpaka sasa.
Homa ya ini bado inatamkwa kama mradi.
Ukimwi bado ni fimbo ya mabeberu .
Mabusha bado hawajatuambia hasa yanatokana na kitu gani na kwa nini hawamalizi chanzo cha tatizo.
Kuna magonjwa mengi ni tatizo sana lakini yanatumika kama miradi ya watu kuneemeka badala ya kumaliza tatizo.
Sent using
Jamii Forums mobile app