Waajiriwa wa sekta binafsi hatuna Afya ya akili

MeVSMe

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2024
Posts
270
Reaction score
425
Wana Jf mko poa? Aisee wale wenzangu namimi wa sekta binafsi, tuambizane kama nyie mna Afya ya akili makazini kwenu.

Picha linaanza unaingia ofisini saa2 unaondoka saa11, ni lazima sio matakwa tu.

Halafu mshahara wako ambayo ni haki Yako, unapata tarehe 37, 38, 39 sometimes mpaka hata tarehe 40, wenye D mbili tu ndo watanielewa.

Hivi Kwa namna hii utaipenda KAZI unayoifanya kweli? Na hapa Afya ya akili kazini ni uongo. Embu labda Mimi nakuwa too judgmental, wenzangu mnazingatia Nini ili kuwa attractive na KAZI zenu 😞😞.

Nahisi Kuna UMUHIMU Mkubwa sana wa kuhamasisha Afya ya akili makazini especially SEKTA BINAFS.
 
Wale WA sekta binafsi mko wapi????
 
Sekta binafsi bongo tunaigiza zaidi kuliko uhalisia..
Mtu hadi leo hata dalili za mishahara hakuna ila ndio utafanya nini unajiamsha asubui kwenda job kibishi bishi..
 
Kuna sekta binafsi unafanya kazi masaa machache hela kwa wakati ,nazingine masaa mengi hata 14 na hela wanatoa kwa wakati na nzuri .

Ni kupambana kutafuta green pasture .

Kumbuka sekta binafsi zinazoajiri watu wengi nizile zinategemea biashara iende sawa ndio wakulipe ,ikienda sio sawa nao wanaangushia mzigo chini. biashara sio rahisi na sio sekta binafsi zote zipo vizuri
 
Nakubaliana nawewe Mkuu, zipo sekta binafsi aisee very Professional,
Tunajua wanategemea biashara sawa, lakini ndo inakuja ule ubinadamu aisee. Yani mtu unaingia ofisini saa2 inafika saa3 usiku unaambiwa kama hujamaliza KAZI usiondoke. Halafu mshahara unapokea tarehe 38?????
 
Nilikuwa na Boss mmoja hata iyo saa 11 anataka uendelee kukaa ofisini apo geto ni Tegeta Ofisi sinza.
Mshahara tareh mpaka 50 ndio analipa sometime mnajua Ofisi imelipwa lkn anakuja na sababu kibao ili tu asiwalipe
Sitasahau yale Maisha.
Apo Afya ya akili sahau
 
Dah, Aisee, Sasa hongera kwako sasahivi umebaki kusema nilikuwa, Kuna wengine ndio maisha ya Kila siku
Na Hilo ndo linakera, yaani mnafanya kazi mnaona kabisa kampuni imeingiza hela ila hampewi hela uuuuwi

Ofisi zingine hazitoi hata mikataba, kudadeki, utadai mikataba we mpaka utakoma
 
Sekta binafsi ipo vizuri sana na utaona matunda yake kama kichwa chako kiko smart.

Ji 'brand' wajue bila wewe mambo hayaendi, utakopeshwa range, nyumba, na nje utasafiri sana; muhimu je kichwa chako kina madini.

Sekta binafsi haiitaji 'compliance' bali inahitaji 'output'/faida; kama unaweza kufanikisha hilo nenda sekta binafsi, kama huwezi ngojea hizo ajira za kugombania.​
 
Tuko hapa Mkuu, changamoto ni nyingi ila ndio tunavumilia.

Ukitaka kupata ahueni, ikubali hiyo hali huku ukitafuta kazi nyingine.
Muhimu, usiache kazi kabla ya kupata kazi. Na hakuna ofisi isiyo na changamoto, zinatofautiana tu.
Amini kwamba! Haya ni madini Mkubwa
SEMA safari ya utafutaji ni ndefu sana
 
Nakubali Mkuu,
Sasa hapo Kwa wahindi, πŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™Œ
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…