Jipambanie, ongeza thamani yako kwa juhudi na maarifa, wasipoitambua thamani yako nenda katafute malisho pengine !
Besides baada ya kuhitimu chuo miaka kadhaa nyuma kabla sitapata direction, kuna sehemu nilikuwa najishikiza, ni sekta binafsi,,unafanya kazi kama punda, masaa mengi hakuna cha overtime wala nini,,,unapelekeshwa kama kichaa, kazi imejaa machawa, ndg zao na maboss hata ambao hawana uzoefu na kazi husika wamechazwa wengi nao wanataka waabudiwe, mshahara Mbuzi na mnalipwa mda mwingine hadi tar 10 , nafasi niliyokuwepo nilikuwa na ahueni ya mshahara, niliacha kazi nikaondoka kila mtu aliniona kichaa, lakini moyoni nilikuwa najua yanayonisibu,,,, ! Amua fanya maamuzi sahihi, ushauri usiache kazi kabla ya kupata kazi, mm niliacha kabla ya kupata kazi lakini usiniige!