Agent Smith
Member
- Jul 2, 2026
- 62
- 140
Raia wamelishwa propaganda za wanasiasa. Hili suala la kuwa-demonize graduates wanaotafuta kazi na watu waliojariwa ilikua ni mbinu yao kukwepa lawama za kutengeneza uchumi unaozalisha ajira za kutosha. Wenye akili ndogo wameibeba agenda ya wanasiasa kama ilivyo.Kwa TZ, serikali ina waajiriwa kama laki 8.
Sekta binafsi, ina ajira zenye staha kama laki 2.
Nchi hii ina watu wenye uwezo wa kufanya kazi kama Milioni 30.
Lakini kutwa kucha, wanajdiliwa watu ambao ni kama Milioni 1 tu.
Na hivi vimotivesheni speaker vina njaa kali sana na madeni lukuki.
Mimi ajira yangu, nakagua biashara, nyingi zina njaaa kali saaana.
Mtu anauza duka na yeye anasema kajiajiri ana uhuru, uhuru gani hawezi hata kutoka. Nje ya Wilaya, muda wote ni hapo duka i kwake???
Huna PENSION
Huna Bima
Huna Likizo
Halafu unasema umejiajiri una uhuru, wakati wakipita Manispaa tu hapo kukudai SERVICE LEVY, unakimbia mpaka miguu inagonga CHOGO.
Kuna motivesheno spika mmoja hivi naskia alishawahi kuwa Tanzania one. Aliwaambia vijana wajiajiri halafu yeye mwenyewe kaomba ajira ya ubunge na kaipata. Sasa hivi ni waziri.