Kabisa mkuu, inabidi ujitoe haswa
Umegusa jambo la msingi sana. Kujiajiri si mbadala wa ajira kwa kila mtu. Ni busara mtu akaanza kujenga biashara akiwa bado ana kipato cha uhakika, biashara ikishasimama ndipo afanye uamuzi wa kuhamia kabisa. Vinginevyo, wengi hujikuta wanarudi kuajiriwa si kwa sababu hawakuwa na uwezo, bali kwa sababu biashara inahitaji mtaji, muda na uvumilivu mkubwa kuliko wengi wanavyodhani.Watu wengi ninao wajua, waliacha kazi kujiajiri badae wakasanda, wakarudi makazini. 😊
Mimi nimejiajiri, huwa sishauri mru aache kazi aje ajiajiri. Sana sana nitamwambia jiajiri ukiwa kazini.
Nakumbuka wakati wa sikukuu waanajeshi,polisi,wafanyakazi wa hospital walivyokijichekesha ili niwakopeshe dukaniHapa umeongopa.
Kujiajiri kunahitaji nidhamu kubwa zaidi ya nidhamu ya mwajiriwa.
Kujiajiri unawaza maradufu....unaumia maradufu.
Chochote unachokigusa unaona si chako ni cha biashara. Lkn ukiajiriwa kile unacholipwa una uhuru nacho.
Na ndiomaama unaona walioajiriwa wanaishi maisha yenye unafuu kuliko aliejiajiri.
Faida ya kujiajiri ni kwamba unapombambana kukuza biashara na asset zinaongezeka bila wewe kutambua, mwisho wa siku unajikuta tu kumbe milionea.
Naona Mkuu unanisema Mimi hapaUnauza duka, genge, winga, Machinga, Saloon, na kazi kama hizo.
Huko siyo kujiajiri.
Hizo ni SUVIRVAL SKILLS.
Unapambana tu USIFE NJAA.
Ukiugua wiki 2, tu unakula MTAJI biashara inakufa.
Dogo alileta usomi na usasa mwingi ndo maana 😃😃😃Tatizo watu wengi wanadhani kila mtu anaweza kufanya biashara,kuna dogo mmoja alimaliza chuo sasa baba yake alikuwa na duka kubwa sana la hardware dogo akakabidhiwa mikoba aisee mara akaanza kugawa vipeperushi mara sijui nini aisee ndani ya miezi 7 tu duka likaganda tu ikabidi mzee wake arudi kuokoa jahazi
Biashara sio kwa ajili ya kila mtuDogo alileta usomi na usasa mwingi ndo maana 😃😃😃