Waajiriwa wengi wanauonea wivu uhuru wa waliojiajiri, lakini hawajui gharama ya huo uhuru

Kabisa mkuu, inabidi ujitoe haswa

Watu wengi ninao wajua, waliacha kazi kujiajiri badae wakasanda, wakarudi makazini. 😊
Mimi nimejiajiri, huwa sishauri mru aache kazi aje ajiajiri. Sana sana nitamwambia jiajiri ukiwa kazini.
 
Watu wengi ninao wajua, waliacha kazi kujiajiri badae wakasanda, wakarudi makazini. 😊
Mimi nimejiajiri, huwa sishauri mru aache kazi aje ajiajiri. Sana sana nitamwambia jiajiri ukiwa kazini.
Umegusa jambo la msingi sana. Kujiajiri si mbadala wa ajira kwa kila mtu. Ni busara mtu akaanza kujenga biashara akiwa bado ana kipato cha uhakika, biashara ikishasimama ndipo afanye uamuzi wa kuhamia kabisa. Vinginevyo, wengi hujikuta wanarudi kuajiriwa si kwa sababu hawakuwa na uwezo, bali kwa sababu biashara inahitaji mtaji, muda na uvumilivu mkubwa kuliko wengi wanavyodhani.
 
Nakumbuka wakati wa sikukuu waanajeshi,polisi,wafanyakazi wa hospital walivyokijichekesha ili niwakopeshe dukani
 
Tatizo watu wengi wanadhani kila mtu anaweza kufanya biashara,kuna dogo mmoja alimaliza chuo sasa baba yake alikuwa na duka kubwa sana la hardware dogo akakabidhiwa mikoba aisee mara akaanza kugawa vipeperushi mara sijui nini aisee ndani ya miezi 7 tu duka likaganda tu ikabidi mzee wake arudi kuokoa jahazi
 
Unauza duka, genge, winga, Machinga, Saloon, na kazi kama hizo.

Huko siyo kujiajiri.

Hizo ni SUVIRVAL SKILLS.

Unapambana tu USIFE NJAA.

Ukiugua wiki 2, tu unakula MTAJI biashara inakufa.
Naona Mkuu unanisema Mimi hapa
 
Dogo alileta usomi na usasa mwingi ndo maana πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ
 
Kuwa msomaji sometimes ni burudani tosha.
 
Kitu kibaya zaidi kwenye kujiajiri ni ile presha ya kutojua kesho itakuwaje.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…