Ondoa nneo kipaji
Kwa namna fulani naamini kwa mbaaali.
Hii kuamini kwangu kwa mbaali inanifanya nisitie maanani suala la kipaji kwa sababu kufanya hivyo kutanifanya nikifeli mara moja nichukue kama hiyo ni excuse kwamba " aaah labda sio kipaji changu"
Lakini tukija katika suala la kipaji hakuna kipimo maalumu kwamba ukifikia kutumia nguvu hii kutafuta jambo fulani basi ujue hiko ni kioaji chako.
Ama ukifikia kiwango fulani cha nguvu kutafuta jambo fulsni basi jua hilo jambo sio kipaji chako bali umefosi.
Hii kwangu inakataa.
Wengi wanachopima ni namna watu wanavyofanya.
Mfano kuna mtoto atatengeneza gari la udongo kwa muda wa dakika kumi.
Mwingine atatengeneza gari hilo hilo kwa lisaa limoja.
Hapa utasema huyu wa dakika 10 ni kipaji chake kwa sababu hajatumia nguvu.
Lakini akitokea mwingine akatengeneza kwa dakika 5 utasema huyu hajatumia nguuvu kama wadakika 10 yule ama yule wa lisaa limoja.
Hivyo hapa utaona kuwa uliyemdhani mwanzo ana kipaji kwa kutumia nguvu ndogo kumbe kuna ambaye katumia nguvu ndogo zaidi yake
Na huyu ambaye unadhani hana kipaji kwa kutumia lisaa limoja kuna mtu pia atakuwa amemzidi hivyo kwa mantiki hiyo ni sahihi kusema hata huyu wa lisaa limoja pia ana kipaji kwa sababu wapo wanaotumia nguvu nyingi zaidi yake.
Hii ndo point yangu mkuu
Azarel upo lakini mkuu ?