Waambieni vijana wenu wanaosoma kuwa hakuna u-genious bila juhudi binafsi

Hakuna ugenius.

Mlikuwa wavivu na wazembe tu.
Ama kuna concept wanazo ambazo zinawarahisishia wao kuelewa maudhui yaliyopo ama wanachofundishhwa.
Ama walishasomaga hizo mada kitambo ila wanajifanya kama hawajasoma vile.

Hujawahi kusikia mtu kavushwa darasa mkuu!!

kuna watu wamebarikiwa
 
1:10
 
Hujawahi kusikia mtu kavushwa darasa mkuu!!

kuna watu wamebarikiwa
Huyu haelewi kwa nini kuna IQ test, hajui kwamba kuna slow learners na fast learners. Kuna training moja nilisoma na wazungu nilipokuwa majuu, aiseee huwezi amini namna wanavyofundishwa ni kana kwamba hicho wanachofundishwa walishakielewa mapema, yaani kwa slow learners waliojaa kwa jamii ya watu weusi kipindi kinaweza kuisha na hujaelewa chochote...
 
Wenzio wameandaliwa sio walikurupuka tu kuwafundisha hivyo vitu.

Hii kitu IQ test naona bado sijapata muda wa kuiamini saaana
 
Wenzio wameandaliwa sio walikurupuka tu kuwafundisha hivyo vitu.

Hii kitu IQ test naona bado sijapata muda wa kuyafatilia
 
slow learners na fast learners
Hii haiji tu burebure.inategemea na mtoto kakulia mazingira gani,kalelewaje,muingiliano na watu ukoje.

Kuna matukio mengi ambayo watoto wanayaexperience katika maisha kiasi kwamba inakuwa rahisi kwake kuelewa masomo ya darasani.

Kuna watoto ambao utaona kama wanasikiliza lakini kumbe hajui kuituliza akili yake ikatulia akasikiliza jambo analofundishwa wewe utaona kama yuko pale kumbe akili yake inawaza mambo mengine kabisa,

huyu inaweza kuwa ni athari ya namna anavyolelewa pengine analelewa katika mazingira ambayo hajifunzi utulivu wa kutulia na jambo moja hivyo hata shuleni anashindwa kutuliza akili.

Huyu ukimfundisha atachelewa kuelewa kwa sababu akili yake haijatulia sehemu moja.
.
Kuna sababu nyingi za kimazingira ambazo tokea utotoni zinamsaidia mtoto kuwa bora huko mbeleni,ndio maana hao wazungu unaowatolea mfano wanawakazania watoto katika mambo mengi sana.
.
Wengine wanakuambia mpaka mtoto akiwa tumboni msomee vitabu au muimbie inasaidia,lakini mbongo anaona upuuzi na miujiza badae anakuja kusema ooh watu fulani majiniaz kumbe alidharau misingi imara ya kumkuza mtoto.
 

ni kweli mkuu tumetofautiana sana katika uwezo.
Juhudi ni muhimu katika kila kitu ila kiwango cha juhudi kinachowekwa na watu kupata matokeo katika jambo flani hutofautiana

watu wenye vipaji hawahangaiki sana na wakiweka juhudi kubwa lazma wafanye maajabu. Wakati mtu mwenye uwezo hafifu atachukua nguvu na muda mrefu kufanya kitu kile kile
 
Wait...don't u believe in talents/Blessings?

At times, some people got blessed with talents, they don't work hard like others to meet their goals, they capture easily

What's yo opinion on this?
 
Ondoa nneo kipaji
Wait...don't u believe in talents/Blessings?

At times, some people got blessed with talents, they don't work hard like others to meet their goals, they capture easily

What's yo opinion on this
Kwa namna fulani naamini kwa mbaaali.

Hii kuamini kwangu kwa mbaali inanifanya nisitie maanani suala la kipaji kwa sababu kufanya hivyo kutanifanya nikifeli mara moja nichukue kama hiyo ni excuse kwamba " aaah labda sio kipaji changu"

Lakini tukija katika suala la kipaji hakuna kipimo maalumu kwamba ukifikia kutumia nguvu hii kutafuta jambo fulani basi ujue hiko ni kioaji chako.

Ama ukifikia kiwango fulani cha nguvu kutafuta jambo fulsni basi jua hilo jambo sio kipaji chako bali umefosi.

Hii kwangu inakataa.

Wengi wanachopima ni namna watu wanavyofanya.

Mfano kuna mtoto atatengeneza gari la udongo kwa muda wa dakika kumi.

Mwingine atatengeneza gari hilo hilo kwa lisaa limoja.

Hapa utasema huyu wa dakika 10 ni kipaji chake kwa sababu hajatumia nguvu.

Lakini akitokea mwingine akatengeneza kwa dakika 5 utasema huyu hajatumia nguuvu kama wadakika 10 yule ama yule wa lisaa limoja.

Hivyo hapa utaona kuwa uliyemdhani mwanzo ana kipaji kwa kutumia nguvu ndogo kumbe kuna ambaye katumia nguvu ndogo zaidi yake

Na huyu ambaye unadhani hana kipaji kwa kutumia lisaa limoja kuna mtu pia atakuwa amemzidi hivyo kwa mantiki hiyo ni sahihi kusema hata huyu wa lisaa limoja pia ana kipaji kwa sababu wapo wanaotumia nguvu nyingi zaidi yake.


Hii ndo point yangu mkuu Azarel upo lakini mkuu ?
 

Nimekuelewa brother na ninakubaliana na yote unayoyasema haswa kwamba watu wanapima matokeo au kitu ulichokifanya na sio kitu unachoweza kukifanya ila hujakifanya. 100% correct

Kipaji kinaweza kuonekana katika wepesi lakini pia katika ubunifu au ubora wa kitu mnachokitoa

Hivi brother unataka kuniambia wapishi wazuri hutumia muda na viungo tofauti na wengine.. Kwa nini wengine wawe best chefs

Je, wabunifu wa nguo kwa nini wengine watoe kazi nzuri zaidi kuliko wengine.. is it all bout efforts !!

Je, kwa nini mafundi ujenzi wanaotumia vifaa sawa lakini kitu wanachotoa kikawa na ubora tofauti ??...

Naamini Juhudi ni muhimu sana katika kutoka chini kwenda juu ila kuna kiwango kukifikia unahitaji vyote viwili
 
Naam mkuu.

Suala la juhudi ndio linamata.

Kwa sababu ukiwachanganya watu wawili.

Mmoja ametengeneza fenicha nzuri kwa vifaa fulani,mwingine akatengeneza fenicha mbaya kwa macho yako lakaini kwa kutumia vifaa vile vile.

Hapa wewe utasema huyu alotengeza vizuri ana kipaji.

It's okey tufanye ana kipaji.

Lakini bila kuwepo huyu wa kumlinganisha nae na akampita usingewexa kusema huyu ntu ana kipaji kwa urahisi ,ingekuwa ngumu.

Lakini unasema fulani ana kipaji kwa sababu anafanya jambo bora zaidi ya mwingine.

Swali langu ni kuwa huyu aliyefanya jambo chini ya kiwango akikutana na mtu ambaye kafanya chini ya kiwango zaidi huoni kama huyu aliyefanya chini ya kiwango ataonekana ana kipaji kuzidi yule mwenzie ?
 
Mkuu, acha kujifariji. Kama wewe ulikuwa hufanyi vizuri darasani, anza kuwapeleka watoto wako shule za ICU (English media). Akili zinarithiwa kama vile unene, weupe na urefu. 'Haiwezekani' baba mweusi tii, mama mweusi tii katoto kazaliwe keupe peee! Ndivyo hivyo. Haiwezekani baba kilaza, mama kilaza azaliwe mtoto brilliant.
 

mkuu watu wanakijua kipaji wanapoona kitu "outstanding"

Mtu kama Joe Jackson alikuwa na watoto almost wote waimbaji, akawapa malezi na work ethics sawa lakini mtoto mdogo Michael Jackson ndiye akaja kuwa mkubwa king of pop "talent ilihusika"

kwa hiyo mtu kufanya kitu na mtu akaridhika inaweza kufanywa na mtu yoyote akiwa na efforts au talent kiasi kidogo (maana hata talent zimetofautiana levels)

ila mtu kufanya kitu hadi watu wakaona kama kitu kipya lazma kipaji na juhudi zitumike

somo kubwa nililolipata kwenye post yako ni kuwa usitegemee kipaji lazma utachelewa.. juhudi ni muhimu zaidi
 
Mkuu hakuna genious anayehangaika kupiga msuli hadi kuloweka miguu kwenye maji, labda genius wa mabox. Wakati wengine watakaa masaa 24 kuweza kuelewa, genius atatumia hardly nusu saa ku-digest na kuelewa the same content.....
Unazungumzia hawa mageniuos wanaomaliza topics zote baada ya kumaliza kidato cha nne wakiingia advance wanakuja kuwapumzikia wenzao ,wanaonekana hawasomi na wanaelewa haraka kumbe washasoma zamani, Huo sio ugenious mkuu wa nchi na watu wa namna hii kwenye mazingira halisi huwa ni ngumu kuwa inventive. Wanaweza wakafanya Kazi vzr lkn kutatua changamoto KWA kujiongeza nje ya scope ya walichosoma ni ngumu sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…