Ajabu baadhi ya watanzania humu tuna zungumzia zaidi na kushangaa inakuwaje polisi Kenya washindwe kudhibiti waandamanaji. Au sababu kuna wajaluo na mambo kama hayo.
Ile hoja kuwa raia wanaongezewa kodi na serikali haijaonesha mkakati wowote wa kupunguza matumizi watu wala haiwahusu. Inasikitisha sana.
Ndiyo maana kuna simulizi nyingi kuwa ni rahisi kutawala Tanzania. Na sifa nyingi nyinginezo za kujifariji, utasikia nchi hii imebarikiwa, ipo chini ya uangalizi wa sijui fulani wa huko mbunguni nk.
Tanzania hii, Tanzania hii, watu tunao tembea tumelala fofofo.