Waandamanaji Nairobi wavamia jengo la Bunge baada ya kuwashinda nguvu polisi, yasemwa waandamanaji 10 wameuawa kwa kupigwa risasi halisi

Waandamanaji Nairobi wavamia jengo la Bunge baada ya kuwashinda nguvu polisi, yasemwa waandamanaji 10 wameuawa kwa kupigwa risasi halisi

Kwa hiyo ww huwezi jitolea kufa ukipigania haki??
Acha kupotosha watu. Binafsi toka nivunjwe mkono kwa kumpambania Dogo janja pale Arumeru kisha nikatelekezwa na CDM alafu baadaye jamaa yetu Nasari akahamia CCM haki ninayoigombania sasa ni "unyumba tu kwa Mama Manka". Hizo nyingine siwezi ingia mtaani.
 
Wake ya wameonesha njia.watanzania tuamke tuubgane tuwashughulikie Hawa vyura wanaojiamulia tu na mambo Yao ya hovyo yanayotughalimu maisha yetu.Na sisi tuandamane kuelekea bungeni na kulichoma moto Hilo jengo maana ndilo linaloasisi maovu yanayotusumbua wananchi.Tukiamua tu aweza na kuwafanya Hawa viziwi kusikia Kwa lazima.
 
Tukio hili laonyesha jinsi serikali ya Kenya ilivyoshindwa kulinda jengo la bunge jengo la kistratejia na shughuli za serikali nchini humo ukizingatia maandamano haya yamechukua siku 7.

Hivyo kulikuwa na muda wa kutosha kwa serikali kuchukua hatua za tahadhari na kuongeza ulinzi katika majengo ya serikali likiwemo hili jengo la Bunge.
Kwamba ingeongeza idadi kubwa kuliko idadi ya wananchi? Suala ni busara siyo nguvu...wananchi wakiamua ata ikulu wanaingia ata uongeze ndege vita na vifaru vingapi
 
Wameingia bungeni na kushusha Bendera zote ya Taifa, ya Bunge, ya Africa mashariki nk

Wameingia Canteen ya Bunge na kuvunja kila Kitu

Wameingia Studio za Bunge na kuharibu kila Kitu

Wameingia Ukumbi wa Mapumziko na Vikao vya Kamati na kuharibu kila Kitu

Je, Bunge la Kenya halijanajisiwa? 🐼

Nairobi
 
Young generation ya wakenya ni wasomi na wanatambua kuwa hizi kodi kwa bidhaa mbalimbali kama mkate na sabuni zitaleta matatizo kwa wazazi wao ambao watawalazimisha vijana kutumia pesa nyingi kununua mahitaji hayo ya msingi.

Raisi Ruto apaswa kuangalia kizazi hiki cha sasa.

Senagal vijana nao wameamua kumchagua raisi kijana ili angalau wawe na same level ya uelewa wanapompelekea shida zao.

Afrika Kusini vijana wasomi wameamua kuigawa ANC bungeni ili kuongeza uwajibikaji na kupunguza vitendo vha kifisadi ambavyo chama hicho kimekumbatia.

Sasa young Generation ya Tanzania wapaswa kufikiri kuachana na Uchawa na kulamba viatu na kufikiri kuhusu "future" ya nchi yao na vizazi vyao.

Its about capacity thinking my friend.
Ni kweli. Lakini vijana wa bongo muda wote wanajadili ''kula tunda kimasihara''. Anyway, watu wa aina hii wanaweza kugeuka ghafla na kuwa wabaya sana na kuchóma kila kitu.
 

View: https://twitter.com/Sirjeff_D/status/1805583153773359575?t=9cXvC78w6ldNEMPULcVzIg&s=19

Kenya wazembe sana Wameshindwa kuingiza Jeshi kuweka vizuizi maeneo yote wanayopita hao waandamanaji?

Hawajifunzi Kwa Cyril Ramaphosa alivyowasafisha? Hao ni bangi,wanachoma Bunge ndio finance. bill?

Kwamba jeshi ingewafanya nini waandamanaji? Kwa utahira wako unadhani wanajeshi wamefundishwa mafunzo ya namna ya kuzuia waandamanaji zaidi ya polisi?
Ungefika ata jeshini ungejidharau sana.
 
Kwamba ingeongeza idadi kubwa kuliko idadi ya wananchi? Suala ni busara siyo nguvu...wananchi wakiamua ata ikulu wanaingia ata uongeze ndege vita na vifaru vingapi
Hapana, kwenye nchi ambazo watu wajitambua majengo hayo huwekwa uzio wa mbao na madirisha hukingwa, makaravati na nyenzo zingine ili angalau kupunguza watu kusogea ndani ya parameters za maeneo yote nyeti.

Hali ikirudi kuwa shwari madude hayo huondolewa.

Look, waandamanaji wana haki ya msingi ya kuandamana don't get me wrong lakini kuna ripoti kuwa kuna waandamanaji wengine wameamua kuvunja maduka na kuanza kupora mali.

Ukifanya hivyo waondoa haki yako ya kuandamana na unakuwa ni mhalifu na si muandamanaji.
 
Kenya hadi polisi wamegawanyika kikabila na polisi wengi Jaluo ndio maana hawataki kutumia nguvu kubwa kudhibiti Jaluo wenzao wanaandamana

How comes barabara zinafungwa na waandamanaji? Tanzania Jeshi letu hakuna ukabila wangetwangwa kuhakikisha wanaondoka barabarani kupisha shughuli za kiuchumi kwenye barabara ziendelee

Kenya na Jeshi lao hopeless kabisa watatumbukiza Kenya kwenye vita za wenyewe Kwa wenyewe muda si mrefu

Watanzania tuliwasaidia mlipotwangana na ukabila wenu na kuzalisha wakimbizi WA Ndani Kikwete akaja kuwasaidia mnataka kuingia part two ya vita za ukabila wenu wapumbavu nyie muanze tena kutusumbua watanzania tuwaletee msuluhishi

Shenzi type nyie
Hakuna jeshi ,polisi wala kikaragosi yoyote anayeweza kuzuia watu wenye njaa kali na waliokata tamaa na wanahisi hawana cha kupoteza .
We ngoja tu hali ya maisha izidi kuwa tight hapa Bongo , tena wewe ndio utakuwa mstari wa mbele kwenye maandamano .
Kwa hali ya kiuchumi ilivyo mbaya duniani , serikali corrupt kama Tanzania zitakuwa exposed Tu na raia watafeel maumivu ya maamuzi mabovu na uongozi mbovu wa serikali zao .
Wewe unafikiri kule Srilanka kulikuwa hakuna jeshi wala polisi ?

Narudia : Corrupt countries zote zenye uongozi mbovu na matumizi mabovu ya rasilimali zitakuwa exposed ,Maana wananchi watafeel maumivu kama kodi kuongezeka ili kufidia malipo ya mikopo iliyokopwa kipuuzi bila kuleta impacts katika vipato vya watu .
 
Ajabu baadhi ya watanzania humu tuna zungumzia zaidi na kushangaa inakuwaje polisi Kenya washindwe kudhibiti waandamanaji. Au sababu kuna wajaluo na mambo kama hayo.

Ile hoja kuwa raia wanaongezewa kodi na serikali haijaonesha mkakati wowote wa kupunguza matumizi watu wala haiwahusu. Inasikitisha sana.

Ndiyo maana kuna simulizi nyingi kuwa ni rahisi kutawala Tanzania. Na sifa nyingi nyinginezo za kujifariji, utasikia nchi hii imebarikiwa, ipo chini ya uangalizi wa sijui fulani wa huko mbunguni nk.

Tanzania hii, Tanzania hii, watu tunao tembea tumelala fofofo.
 
Back
Top Bottom