Waandishi Clouds 360 wamshukia kama mwewe wakili Msando kwa kupotosha kuwa Arusha hali ni mbaya kwa Corona

Hivi kule Clouds TV na radio kuna Waandishi wa habari Nguli?? Labda wazuri wapo lakini siyo hivyo unavyo taka kutuaminisha.
 
Hawa na msando wote wanatengeneza drama kututoa kwenye reli. Serikali inatakiwa kutoa taarifa na waandishi wanatakiwa kutafuta habari kuibua hoja, wote hawafanyi wanachotakiwa kufanya.
Wasitupotezee muda.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo Msando ni rafiki na viongozi wa CCM hivyo alivyosema hakukurupuka, hao "waandishi wako nguli" ndio hawajielewi, watakuwa wanajipendekeza tu, au hawajui kufanya uchunguzi.

Wale wapiga miziki ndo unawaita nguli!.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ngoma naye ni mwandishi NGULI ? mleta mada ni ngumbalu kweli kweli
 
Hoja yako ilikuwa nzuri sn ila umeinajisi kwa kusema hao wa kina sasali na Hassan Ngoma eti ni Nguli
 
Wao clouds waendelee kukaa kusubiri habari ndo waitangaze lakini Msando anawasihi watoke wakatafute habari. Anayesubiri habari ndo atangaze hawezi kuwa mwanahabari.
 
wamekurupuka ,next time mtu kabla ajaongea inabidi afikiri
 
Wewe unasemaje kuhusu hali ya Corona bwashee?!
 
Waandishi wa habari za kiuchunguzi sijui kama wapo, Risk ni kubwa alikuwepo JM, Na Kabendera. Na nje kuna kina Kashogi. Hawataki ku take risk, wanataka upande ambao upo soft wanasubiri serikali itangaze then wao wafuate. Wanaogopa kutafuta ukweli au ku balance story.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wao clouds waendelee kukaa kusubiri habari ndo waitangaze lakini Msando anawasihi watoke wakatafute habari. Anayesubiri habari ndo atangaze hawezi kuwa mwanahabari.
Hata hiyo ya Msando wamesubiri, kwanini wawe wa kwanza na si serikali. Wajibu hoja ya Msando, watoke ofisini waende field, au wanaogopa Corona [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…