Waandishi wa hababari wamekuwa wabaguzi kuripoti habari za uvunjifu wa haki za binadamu. Ila wao yakiwakuta ndio midomo juu

Idugunde

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2020
Posts
6,404
Reaction score
6,969
Kuna habari inatembea kwenye mitandao ya kijamii kuwa mwandishi wa gazeti la mwananchi huko Zanzibar amepigwa na kudhalilishwa na wana usalama huko Zanzibar. Inadaiwa maafande wa KMKM walimvamia na kumpa kichapo kisha kumtesa na kumlazimisha avunje simu yake aliyotumia kuwapiga picha wakati wakifurusha wamachinga maeneo ya Darajani Zanzibar.

Lakini hawa watu wanatabia mbaya sana kama ni raia wa kawaida amepatwa na madhara kama haya hawawezi kuripoti kama wakiripoti ni kwa shingo upande sana.

Hii tabia ya kujipendelea nyie tu huwa ni uzembe usiofaa kabisa. Na kinyume na maadili ya kazi yenu
 
Ila si kosa Lao jamani kumbuka kipindi cha nyuma kabla ya hii miaka mitano iliyopita.....walikuwa na uhuru wa kureport kwakweli acheni HERODE aende zake
 
Lakini angalao Waandishi wa Zanzibar walikuwa wanajitutumua kuliko hawa wa Tanganyika waliokuwa wameufyata Mkia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…