Waandishi wa habari mkoa wa Mara hawatoi taarifa za matukio mengi kwa wakati! Sababu ni nini?

Waandishi wa habari mkoa wa Mara hawatoi taarifa za matukio mengi kwa wakati! Sababu ni nini?

Lanlady

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2019
Posts
1,836
Reaction score
6,303
Kuna baadhi ya matukio yamekuwa yakitendeka mikoani, ambayo taarifa zake hazitolewi kwa wakati au kutokutolewa kabisa.

Kuna tukio la kukatwa mapanga hadi kuuawa kwa mwalimu wa shule ya sekondari kata ya masaba, wolaya ya Butiama ila hadi leo hakuna taarifa iliyotolewa na vyombo vya habari kukemea ukatili huu!

Ingekuwa mwalimu ameua, amebaka au kufanya tukio lolote la kihalifu, bila shaka tungeshasikia kila mahali!

Waandishi wa habari mko wapi? Ukatili kwa baadhi ya walimu mkoa wa Mara umekuwa ukifanyika mara kwa mara! Matukio ni mengi lakini hayatolewi taarifa. Tusaidiane!
 
Nazani hawajaipata mkuu.

Lakini Mara kukatana mapanga imekuwa ni kawaida,huenda waandishi wameacha au wamepunguza kutoa ripoti za hayo matukio.

Anyway, karibu hapa nyasho nikuchukulie hata togwa kuna mnada walau upunguze joto.
 
Wanaachaje kuipata wakati mdogo mtu yupo hospital ya mkoa ya Mara hivyo nivitu vya muhimu kuvijua
 
Wanaachaje kuipata wakati mdogo mtu yupo hospital ya mkoa ya Mara hivyo nivitu vya muhimu kuvijua
Walikuwa wawili kaka yake amefariki amebaki mdogo mtu hivi inawezekanaje sisi tuliopo mbali tunajua Ila wao wako karibu wanashindwa au hawaruhusiwi kuhoji mtu mkoani Mara maana ukiangalia hata taarifa za mkoa zipo chache
 
Hivi sahvi kuna waandishi wa habari kweli.

Maana habari nyingi za umbea,wanamuita mandonga studio.

Mondi konde kajala kafanya nn wamuhoji.

Au ulitaka walete habari zipi

Ova
 
Kuna baadhi ya matukio yamekuwa yakitendeka mikoani, ambayo taarifa zake hazitolewi kwa wakati au kutokutolewa kabisa...
Tanzania hakuna waandishi wa habari bali kuna wachovu wanaochumia tumbo. Watu wengi wenye porojo na ambao walikuwa hawana kazi wamekimbilia huko ili kupata kula yao.

Wanajiua wenyewe kwa sababu siku hizi kuna social media na chema chajiuza kibaya chajitembeza.

Wewe badala ya kulalamika ungeweza kabisa kuanzisha thread kuhusi hili tukio, uelezee kwa kina.
 
JF ni uwanja wa taarifa, wasipozitangaza wao, humu utazikuta...
 
Back
Top Bottom