Waandishi wa Habari muwe na akiba ya maneno, kufurahisha watawala kutawadhalilisha

Waandishi wa Habari muwe na akiba ya maneno, kufurahisha watawala kutawadhalilisha

Nchi hii ngumu sana.


View attachment 2104148

Inawezekana kabisa watanzania waliotukanwa, kudhalilishwa, kusingiziwa, kubaghazwa na mengineyo mengi ndiyo wenye mapenzi ya dhati kwa taifa lao.

Ukweli unaweza kuchelewa tu, lakini ikifika muda wake, huibuka na kujisemea wenyewe.

Leo ni huyu dada lakini kuna siku tutajua faida ya LISSU katika Taifa hili. Ni muda tu.
Wakuu ni mapema sana kushangilia, kuna mdau aliweka uzi wa namna nchi inapokuwa kwenye kipindi cha tahadhari inapotokea rais aliyeko madarakani akafa. Kwa Tanzania kifo cha Dkt Magufuli kimeambatana na kundi fulani kufurahia tena wazi wazi, sasa huwezi jua wenye nchi wanaacha ili kila msaliti ajianike then wafanye yao na kuwaua wasaliti wote na nchi kurudi kwenye mstari. Kwa hiyo kipindi hiki ukipewq nafasi usishangilie unaweza jikuna upo kwenye 18 ya wenye nchi.
 
Lisu
Fatma a.k.a Shangazi yetu kipenzi.
Maria Sarungi.
Mangi Kimambi
Kigogo.
Hawa watu ni wazalendo halisi Kwa Taifa hili.
Muda wote Wamelipigania Taifa hili bila kujali maslahi ya kibinafsi au kivyama au kisiasa au kiuchumi.

Mungu ndiye anayeweka watawala na viongozi katika nchi ili watawale Kwa haki.
Wakipuuza haki basi Mungu ataendelea kutenda miujiza na kuwashusha chini waliojikweza na kuwainua waliodhalilishwa.

CCM na watawala wenye kujiona miungu wasipojali haki Kwa wananchi wote bila kujali vyama,jinsia, dini,kabila n.k basi wajue kabisa kabla ya kumalizika Kwa muongo huu Lisu atainuliwa na Mungu na atakua juu bila kutegemewa. Rushwa ,Kununua watu, kutisha watu, kuweka propaganda za kila namna bila kutenda haki na kusimamia kweli na uhuru wa watu wema na ulinzi wa watu na Mali zao itakua ni kitanzi kikubwa Kwa CCM na serikali yake.
 
Huu Ujumbe kuhusu Lissu ufike pande zote

Maana kwa miaka ile enzi ya Jakaya kama kuna mwanaChadema ungemwambia eti ipo siku Dr Slaa atafanya kazi kwenye Serikali ya CCM basi angekupiga hata na mayai viza
Wana Ccm na wana Cdm ni mtu na ndugu yake wote ni wachumia tumbo tu.

Siwezi kuidanganya nafsi yangu kwenda eti kupoteza muda kupiga kura nikimchagua kiongozi wa Ccm ama Cdm, kwamba nina imani nao, nitakuwa ninajisaliti mwenyewe!

Lisu na Mbowe walinistaafisha uanachama baada ya kula matapishi yao ya kumuuzia ugombea uRais Lowasa kwa vipande vya fedha kwa maslahi yao binafsi, tangia wakati huo ninakiamgalia Cdm na viongozi wake kama ni kundi la wahuni tu.

Ninasema na ninarudia tena kuwa waTz tumechoshwa na siasa za propaganda na matamshi ya chuki na kejeli kila siku badala ya sera.

Hupelekea kujiuliza: au Cdm ni mamluki wa Ccm walio maalumu kwa ajili ya kuhadaa raia na kuvuruga upinzani nchini kama alivyofanya Mrema Lyatonga?

Kwanini mnakuwa hambadiliki?

Tunaomba mumuweke ama ajitokeze kiongozi mwingine mpya wa upinzani tutakayempima kwa hoja zake, kwamba huyu atatuvusha na kutupeleka kuleTz tuitakayo, huyo tutampatia kura zetu zote bila kujali rangi ya bendera ya chama chake na jambo hili lifanyike mapema iwezekanavyo.

Lakini sura zikiwa ni hizi hizi za upinzani za leo, Lisu sijui Mbowe, sijui Lipumba, sijui Zitto ni kupoteza wakati kufikiri mmojawapo kati ya hao anaweza akatuletea maendeleo ya mabadiliko ya maana tuyatakayo zaidi ya migogoro na chuki tu.

Ni lini mtaacha kuendelea kujisafisha kwa tope mlilolivagaa 2015 kutusaliti washabiki na wapenzi wenu wa mageuzi na kuanza kuhubiri mikakati na sera za maana zitakazotushawishi?

Tumechoka, embu wekeni sura mpya.

Kwa nyie hapana imetosha sasa.
 
Nchi hii ngumu sana.


View attachment 2104148

Inawezekana kabisa watanzania waliotukanwa, kudhalilishwa, kusingiziwa, kubaghazwa na mengineyo mengi ndiyo wenye mapenzi ya dhati kwa taifa lao.

Ukweli unaweza kuchelewa tu, lakini ikifika muda wake, huibuka na kujisemea wenyewe.

Leo ni huyu dada lakini kuna siku tutajua faida ya LISSU katika Taifa hili. Ni muda tu.

Du mkuu umeconclude kimahaba. Hakuna connection kabisa na Lissu. Taifa Hili Lissu hawezi kutuongoza. Atakuwa dikteta wa hali ya juu sana. Kwake the end justifies the means.
 
Haya yaliyoandikwa na hili gazeti pro-ccm waliwaaminisha Watanzania kwa nguvu kubwa hadi majukwaani.

Lakini jambo la ajabu leo Zuhra Yunus (Adui namba 4) anateuliwa kuwa Msemaji wa ofisi kuu zaidi yaani Ikulu.

Jee siku Bob Amsterdam akiteuliwa kuwa balozi wetu wa Utalii huko Ulaya tutashangaa?

CCM ni waongo na wasahaulifu hakuna mfano na tunapaswa kuwapuuza.

patrickolesosopi-___CZcFIosN4Zq___-.jpg
 
Hizi zilikuwa kampeni za uchaguzi wa 2020...hayo yalishapita, hizi ni zama mpya.
 
Haya yaliyoandikwa na hili gazeti pro-ccm waliwaaminisha Watanzania kwa nguvu kubwa hadi majukwaani.
Lakini jambo la ajabu leo Zuhra Yunus (Adui namba 4) anateuliwa kuwa Msemaji wa ofisi kuu zaidi yaani Ikulu.
Jee siku Bob Amsterdam akiteuliwa kuwa balozi wetu wa Utalii huko Ulaya tutashangaa?
CCM ni waongo na wasahaulifu hakuna mfano na tunapaswa kuwapuuza
View attachment 2104729
Shida pia walio mzunguka Mama hawako makini. Tusipo amka na kupiga kelele Mama ana kuja kuwa hatari kuliko JPM. By the way mnajua asili yake.
 
Back
Top Bottom