Huu Ujumbe kuhusu Lissu ufike pande zote
Maana kwa miaka ile enzi ya Jakaya kama kuna mwanaChadema ungemwambia eti ipo siku Dr Slaa atafanya kazi kwenye Serikali ya CCM basi angekupiga hata na mayai viza
Wana Ccm na wana Cdm ni mtu na ndugu yake wote ni wachumia tumbo tu.
Siwezi kuidanganya nafsi yangu kwenda eti kupoteza muda kupiga kura nikimchagua kiongozi wa Ccm ama Cdm, kwamba nina imani nao, nitakuwa ninajisaliti mwenyewe!
Lisu na Mbowe walinistaafisha uanachama baada ya kula matapishi yao ya kumuuzia ugombea uRais Lowasa kwa vipande vya fedha kwa maslahi yao binafsi, tangia wakati huo ninakiamgalia Cdm na viongozi wake kama ni kundi la wahuni tu.
Ninasema na ninarudia tena kuwa waTz tumechoshwa na siasa za propaganda na matamshi ya chuki na kejeli kila siku badala ya sera.
Hupelekea kujiuliza: au Cdm ni mamluki wa Ccm walio maalumu kwa ajili ya kuhadaa raia na kuvuruga upinzani nchini kama alivyofanya Mrema Lyatonga?
Kwanini mnakuwa hambadiliki?
Tunaomba mumuweke ama ajitokeze kiongozi mwingine mpya wa upinzani tutakayempima kwa hoja zake, kwamba huyu atatuvusha na kutupeleka kuleTz tuitakayo, huyo tutampatia kura zetu zote bila kujali rangi ya bendera ya chama chake na jambo hili lifanyike mapema iwezekanavyo.
Lakini sura zikiwa ni hizi hizi za upinzani za leo, Lisu sijui Mbowe, sijui Lipumba, sijui Zitto ni kupoteza wakati kufikiri mmojawapo kati ya hao anaweza akatuletea maendeleo ya mabadiliko ya maana tuyatakayo zaidi ya migogoro na chuki tu.
Ni lini mtaacha kuendelea kujisafisha kwa tope mlilolivagaa 2015 kutusaliti washabiki na wapenzi wenu wa mageuzi na kuanza kuhubiri mikakati na sera za maana zitakazotushawishi?
Tumechoka, embu wekeni sura mpya.
Kwa nyie hapana imetosha sasa.