Waandishi wa Habari na Kupotea/Vifo vya Kutatanisha, Toka Katabalo, Saanane, Gwanda, Mwangosi, Isango. Ni Ama Tuombe Mungu Atunusuru ama...

Waandishi wa Habari na Kupotea/Vifo vya Kutatanisha, Toka Katabalo, Saanane, Gwanda, Mwangosi, Isango. Ni Ama Tuombe Mungu Atunusuru ama...

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,

Humu jukwaani tuko watu wa fani mbalimbali na miongoni mwao ni sisi watu wa fani ya habari.

Leo nimewakumbuka waandishi wa habari na kupotea/vifo vya kutatanisha, toka kwa Stan Katabalo, Ben Saanane, Azory Gwanda, Daudi Mwangosi, Josephat Isango, maajaliwa ya hatma za maisha yao, ni ama tuombe Mungu atunusuru na dhahama hizo, ama... (Ndio kama vile kilichomkuta Ben Saanane na Azory Gwanda, ni vanish into thin air hata unywele!)

Ukiwa ni mwandishi wa habari wa kawaida tuu au mtangazaji wa kawaida tuu, uandishi wa habari, ni kazi kama kazi nyingine yoyote, lakini ukiwa ni mwandishi wa habari za kiuchunguzi (IJ) au mtangazaji machachari unayehoji maswali magumu kama ya kwenye Kiti Moto, kiukweli wasomaji wako na watazamaji wako watakusifu sana kwa kazi nzuri, wewe ni mwandishi hodari, ni mwandishi jasiri huogopi mtu, ni mwandishi shujaa wa habari, ila majaaliwa ya maisha yako na familia yako ni ya mashaka sana na wengi wa waandishi wa type hii, huwa na mwisho mbaya ambao hauzungumziki!.

Tukianzia kwa mwandishi wa kwanza wa habari za uchunguzi nchini Tanzania, Stan Katabalo wa gazeti la Mfanyakazi aliyeibua kashfa ya Loliondo, alikufa kifo cha ghafla, japo alisifiwa sana kwa ushujaa na mpaka kesho jina lake bado linavuma kwenye list ya mashujaa wa habari Tanzania, lakini sijui kama kuna waandishi au vyama vya habari wanajua chanzo halisi cha kifo chake, au kaburi lake linafanana vipi ?, au kuitembelea familia yake kujua majaaliwa ya familia yake aliyoiacha huku nyuma baada ya kifo chake, yeye akiwa ndio baba mwenye nyumba?!.

Baada ya Stan Katabalo, alifuatia Kabendera Shinani akiripotia BBC, Kwa mujibu wa mwana jf huyu
Mnamkumbuka Kabendera Shinani? Naye aliuwawa kule BK kwa kina IWE na alikutwa anaelea ziwani. Wanasema naye alikuwa akifuatilia kashafa moja ya utekaji wa magari mkoani Kagera ambapo kigogo mmoja huko mkoani alikuwa anahusika!
genekai,

Kabendela shinani hakuuwawa na yeyote bali ali commit suicide kwa kujitupa ziwani na watu waliona kile kitendo.
Alitoka nyumbani asubuhi akiwa ndani ya gari yake. akaegesha gari bandarini, kulikuwa na meli ya MV Victoria imetia nanga pale Bukoba, akaingia ndani ya meli na kujitupa majini kwenye maji ya kina kirefu.

Issue yake ni kwamba yeye ni mzaliwa wa Kagera ambaye aliamia Rwanda akaoa huko na kuchukua uraia na kuishi huko. Baada ya ile genocide ya Rwanda alikimbia kurudi huku kama mkimbizi. Lakini kwa kuwa alijua yeye ni mzaliwa wa hapa aliishi nje ya makambi ya wakimbizi na bahati mbaya sana alianza kujiingiza kwenye mambo ya siasa.

Wakati huo huo akiwa Rwanda alikuwa mtangazaji wa redio pale Rwanda, na mwakilishi wa BBC pia pale Rwanda. Lakini pia inaaminika alikuwa rafiki sana wa marehemu rais Habyalimana. Baada ya kifo cha Habyalimana kulitokea machafuko yaliyosababishwa na umwagaji damu sana. Na yeye alikuwa mmoja kati ya watu waliochochea sana through propaganda (kumbuka anayofanya yule Kibonde wa clouds?) mauaji katika radio na baadhi ya wenziwe walikuwa wameshakamatwa na kupelekwa Rwanda na wengine walikuwa Arusha.

Kwa kujihusisha kwake na siasa hapa kulimzalishia maadui na wakafichua siri kuwa pamoja na kwamba yeye alikuwa mzaliwa wa Tanzania lakini alishakana tayari uraia wa Tanzania na kupewa uraia wa Rwanda na kwamba alishawahi kumiliki passport ya Rwanda. Hilo lilifanya watu wa uhamiaji waanze kumuhoji na kumfuatilia sana na kutaka kujua kwa nini hakuwa anaishi katika makambi ya wakimbizi na kwa nini aliwahi kuomba passport ya Tanzania kwenda nje bila kusema ukweli kuwa yeye si raia wa nchi hii? Jambo hili lilimtia hofu sana.

Kwa hofu kwamba wangeweza kumrudisha makambini au kumrudisha Rwanda au kumkabidhi kwa makachero wa Rwanda waliokuwa wanamtafuta at that time, aliona bora ajiue na hivyo akafanya kama alivyofanya. Ilikuwa ni kuogopa mkono wa serikali ya Rwanda.

No body killed him but he killed himself. Familia yake wengine walirudi Rwanda wengine bado wako hapa Tanzania.
The same applies to Azory Gwanda na Ben Saanane wetu humu JF, yamebaki majina na mabandiko tu humu jf, lakini hakuna ajuaye hatima yao ni nini kiliwakuta, lakini sisi wanajamii vikiwemo vyama vya habari, japo tuliwasifu sana wakati wakileta habari za moto moto, lakini baada ya kutoweka, hakuna tena anayejali wala kujua tuu majaaliwa ya familia zao!. Kutokana na kazi ya uandishi wa IJ kuwa ni kazi ya hatari sana!.

Waandishi wa habari za IJ wa nchi za wenzetu wanakuwa na bima za maisha!, just in case of anything, likitokea, the family survives, lakini sio hapa kwetu Bongo!, sijui mwandishi yeyote wa habari mwenye bima ya maisha Tanzania, ukimuondoa Erick Kabendera ambaye na yeye aliponea chupu chupu kupotezwa!. Salama yake ni alikuwa mtu well connected hivyo akachukua tahadhari zote, wakashindwa kumpotezea, wakabidi kumkamata na kumbambikizia kesi.

Nimelileta bandiko hili baada ya kumkumbuka mwandishi wa habari machachari Josephat Isango aliyefariki tarehe ya jana mwaka 2018, baada ya kuugua ghafla, hakuna media wala chama cha habari kilicho jishughulisha kubaini chanzo cha kuugua kwake ghafla na baada tuu ya maziko, sifa na pongezi zake zinaishia hapo makaburini kwa waandishi, vyama vya habari na vyama vya siasa kuweka mashada makubwa ya maua, kisha kusoma risala nzuri za kumsifu marehemu jinsi alivyokuwa mwandishi shujaa, na baada ya mazishi, then all ends up there and then!, ulikuja peke yako, unaondoka peke yako!, nobody cares hata tuu kufanya IJ ya what real happened to you na nini majaaliwa ya familia yake!.

Mimi nilifahamiana na Josephat Isango mwaka 2015 kwa kuunganishwa nae na mtangazaji nguli Angalieni Mpendu kupitia kipindi cha Jicho Letu Ndani Ya Habari cha Star TV.

Kisha tukaja kukutana Siku ya Uhuru wa Habari Morogoro, then Mwanza na kote huko Isango akihadithia jinsi anavyo windwa na wenye mamlaka, hatukuwajibika ipasavyo kumsaidia kwa jinsi ile ile media tulivyoshindwa kumsaidia mwandishi wa ITV, Adam Mwaibabile (Mwana) alikuja kuishia kutupwa jela kwa maonevu!.

Hadi kifo chake, sikupata kusikia Isango alikufa kwa nini au chanzo cha kifo chake kama ilivyo kwa Stan Katabalo, ila kiukweli sisi waandishi wa habari za uchunguzi na watangazaji wa maswali magumu, tuna wakati mgumu sana kwenye maisha yetu, afadhali ya wenzetu kama Ansbert Ngurumo na Erick Kabendera, wana pa kukimbilia!, sisi tusio na pa kukimbilia, tutabanana hapa hapa!.

Hivyo wanabodi, tunaposifiana humu kwa maswali magumu kama yale ya Ben Saanane, tusiishie kusifiana tuu humu bali tuangalie na hatma za maisha yetu ya sasa na ya baadae ya sisi na familia zetu, hivyo ikitokea mtu aliyekuwa very critical on the status quo, ghafla akageuka na kuunga mkono juhudi, akaanza kusifu na mapambio, nawaombeni sana muwaelewe watu wa aina hii ambao hawaangalii tuu leo yao au sasa yao, bali wanaangalia mbali zaidi kwa kuangazia kesho yao kwa kuimagine, mfano mimi ndio ningekuwa Ben Saanane, au Azory Gwanda, what would become of my family left behind?!.

Wandugu tuombeane sisi watu wa media tumalize salama vipindi vyetu vifupi vya maisha yetu hapa duniani na tuwe na hatma njema za maisha yetu na ikitokea yakakatishwa ghafla, kwa nguvu nyingine yoyote ambayo sio mpango wa Mungu, japo Mungu ataingilia kati kupitia kitu kinachoitwa karma, basi wale ambao ni rafiki zetu wa kweli na wa dhati wa kufa na kuzikana, tusiishie tuu pale kwenye mashada na risala za wasifu, bali angalau fuatilieni what real happened, japo karma always takes care of this, ila pia fuatilieni na majaaliwa ya familia zetu tulizo ziacha huku nyuma!.

RIP Wanahabari wote waliotangulia mbele ya haki na Mungu uwanusuru wale waliopotea bila sisi kujua hatma zao, na naamini kabisa bila shaka yoyote kuwa karma Itawashughulikia wahusika wa matukio hayo, huku sisi ambao bado tuko kwenye fani kiugumu ugumu, and we are still surviving, Mungu atujaalie moyo wa uvumilivu, ustahimilivu, na ufuatiliaji, tuwatembelee kujua majaaliwa ya familia zao.

Paskali
Baadhi ya mada za Isango
Naomba mjadala wa wazi na Zitto kuhusu usaliti ndani ya chama - JamiiForums

Je, ni sahihi kwa CHADEMA kumzika Josephat Isango kwa taratibu za chama? - JamiiForums

Waandishi wa habari kuvaa sare za vyama kama huyu Gerson? - JamiiForums

TANZIA: Mwandishi wa habari, Josephat Isango afariki dunia; Azikwa Kisasida, Singida - JamiiForumsé

Josephat Isango (Tanzania Daima) ashtakiwa, adaiwa mil.500 - JamiiForums

Josephat Isango, Mhariri wa Habari Tanzania Daima akamatwa na Polisi - JamiiForums

Josephat Isango: Natoa Shukrani kwa wote - JamiiForums

Tanzia: Josephat Issango afiwa na baba yake. - JamiiForums
 
Mkuu,

Mbona ushaanza kuweka wosia kwa kutizama waandishi wengine waliondokaje. Huenda kuna makala ipo njiiani ina sita kuiachia,kwa mtizamo wa chanya wa ku risk maisha yako.

Iachie tu hiyo makala. Tutaipokea tu, kuhusu ulinzi Mwombe Mungu tu.
 
Pascal, kuna kitu kimoja ambacho ni common kwa hawa waandishi uliowataja - wote eidha waliikosoa serikali au viongozi wa juu wa serikali. Kwa hiyo kupotea kwao hakuwezi kuwa ni random/incidental au accidental. Na kwamba ni incident zaidi ya moja, ina maana pia kuna system iliyowekwa rasmi kwa ajili ya kupotea watu wa namna hii.

That is the sad reality.
 
Pascal, kuna kitu kimoja ambacho ni common kwa hawa waandishi uliowataja - wote eidha waliikosoa serikali au viongozi wa juu wa serikali. Kwa hiyo kupotea kwao hakuwezi kuwa ni random/incidental au accidental. Na kwamba ni incident zaidi ya moja, ina maana pia kuna system iliyowekwa rasmi kwa ajili ya kupotea watu wa namna hii.

That is the sad reality.
Ukija utawala mwingine ukawakamata watu kama wanne hivi kila kitu kitajulikana. mmoja ameshatajwa na Marekani.. huyo atawataja wote
 
Pascal, kuna kitu kimoja ambacho ni common kwa hawa waandishi uliowataja - wote eidha waliikosoa serikali au viongozi wa juu wa serikali. Kwa hiyo kupotea kwao hakuwezi kuwa ni random/incidental au accidental. Na kwamba ni incident zaidi ya moja, ina maana pia kuna system iliyowekwa rasmi kwa ajili ya kupotea watu wa namna hii.

That is the sad reality.
Wamepotezwa sio kupotea mtu mzima anapotea vipi
 
Back
Top Bottom