Watanzania wengi wana tatizo la kutoweza ku focus kwenye hoja na dhana, na kutaka ku focus kwenye watu na natukio.
Kuna msemo kwamba, small minds discuss people, average minds discuss events, great minds discuss ideas. Sisi tunekomaa sana kwenye small minds na average minds.
Ndiyo maana Mwalimu Nyerere alivyiends Kilimanjaro Hotel kujadiki sifa za mgombea urais, waandishi wakaanza kuongelea watu, hususan Mrema, Nyerere akawaambia sijaja hapa kujadili mtu, ninekuja kujadiki sifa za urais.
Ndiyo maana uzinduzi wa kitabu cha Mkapa badala ya kujikita kwenye uchambuzi wa dhana za msingi alizokulia na kuzeekea rais Mkapa, kama msuguano kati ya Azimio la Arusha alilokulia Mkapa na ubinafsishaji wa mashirika ya umma alioufanya uzeeni, uandishi umeenda kuongelea watu na matukio, habari za Magufuli kupeea sumu.