Waandishi wa habari wa Tanzania, Hoja kuu ya Mkapa ilikuwa nini?

Waandishi wa habari wa Tanzania, Hoja kuu ya Mkapa ilikuwa nini?

Nimesoma kwa makini sana hoja zote zinazozungumzia utendaji kazi wa waandishi wa habari,asanteni nyote hii ni feedback nzuri sana kwetu na tutajaribu kila njia ili tuyafanyie kazi yale yaliyo ndani na uwezo wetu
Hata hivyo nina machache nataka kuongea hapa
1.Waandishi wa habari hawamiliki vyombo vya habari,ni wafanyakazi tu na tena zaidi ya hapo hawana mamlaka ya habari gani itoke na ipi isitoke,mamlaka hayo wanayo wamiliki
2.Baadhi ya wamiliki huamua habari ziandikweje ili kutowaudhi wenye mamlaka za kisiasa au kiuchumi
3.Wamiliki kwa upande wao wanadai wanatishwa kiychumi kuwa wakiandika habari zinazokosoa mamlaka,wananyimwa matangazo kwa maksudi na hatimaye wanashindwa kuendesha vyombo vyao
4.Waandishi wa habari pia wanatishwa na kudhuriwa kwa kuandika habari za ukweli na hii nyote mnaona,sasa mkumbuke hakuna habari inayozidi uhai wa mwandishi wa habari
4.Hatuwezi kabisa kuwalinganisha waandishi wa habari wanaofanya kazi na mashirika kama bbc na hawa wa kwetu wanaofanya kazi kwenye vyombo kama tanzania daima,kwani kuna tofauti kubwa sana,kimaslahi,kimuundo,kisera na kiusalama
Wakatabahu
 
Acha dharau! Wewe umethubutu lipi katika kuipigania nchi yako! Hebu paza sauti kukosoa yanayotokea chini ya Serikali ya awamu ya tano! Maana wewe una level ya PHD achana na hao waliofeli kidatu cha nne.
 
Nimesoma kwa makini sana hoja zote zinazozungumzia utendaji kazi wa waandishi wa habari,asanteni nyote hii ni feedback nzuri sana kwetu na tutajaribu kila njia ili tuyafanyie kazi yale yaliyo ndani na uwezo wetu
Hata hivyo nina machache nataka kuongea hapa
1.Waandishi wa habari hawamiliki vyombo vya habari,ni wafanyakazi tu na tena zaidi ya hapo hawana mamlaka ya habari gani itoke na ipi isitoke,mamlaka hayo wanayo wamiliki
2.Baadhi ya wamiliki huamua habari ziandikweje ili kutowaudhi wenye mamlaka za kisiasa au kiuchumi
3.Wamiliki kwa upande wao wanadai wanatishwa kiychumi kuwa wakiandika habari zinazokosoa mamlaka,wananyimwa matangazo kwa maksudi na hatimaye wanashindwa kuendesha vyombo vyao
4.Waandishi wa habari pia wanatishwa na kudhuriwa kwa kuandika habari za ukweli na hii nyote mnaona,sasa mkumbuke hakuna habari inayozidi uhai wa mwandishi wa habari
4.Hatuwezi kabisa kuwalinganisha waandishi wa habari wanaofanya kazi na mashirika kama bbc na hawa wa kwetu wanaofanya kazi kwenye vyombo kama tanzania daima,kwani kuna tofauti kubwa sana,kimaslahi,kimuundo,kisera na kiusalama
Wakatabahu
Hapo ndio tunataka, maana kwenye mifumo ya kileo ya uendeshaji serikali kuna muhimili wa NNE, wana habari!

Muhumili ukitishwa better public ijue! Hizo ndio sacrifices za professionalisms, kama Muhandisi anavyo risk kwenye majengo au manyaya ya umeme mwandishi ana risk kwenye ukweli na uwazi!
 
Alijua weaknesses za waandiji akajitahidi kudrift attention na akafanikiwa kwasababu ya ukanjanja wa waandishi wetu!
Kwa hiyo ulitaka akae kimya tu licha ya ukweli kuwa alitaka kuuwawa?. Huoni uhusiano kati ya njama za kutaka kumuua na uongozi wa Mkapa?.

Unawakejeli waandishi wa habari halafu na wewe unajenga hoja nyepesi zenye kustahili kukejeliwa!!.
 
Umeelewa hoja? Umeelewa Hata ulichokiandika?
 
Unawazungumzia Waandishi wepi? Wakina Pascal Mayalla, Jackton Manyerere, Sam Mahela au wepi?
Hakuna watu wa Hovyo kama Waandishi wa Tanzania. Na Ndiyo maana sikilizi Taarifa za Habari za Tanzania wala magazeti Maana wanaandika kama Hata shule hawajaenda. Hawana Msaada kwa Jamii ya Tanzania.
Nilowapuuuza Kabisa na Kuwaona hopeless pale Waliposhindwa Kusimamia Msimamo wao kwa Kumgomea Nyamitako badala yake wao ndiyo wakaanza kujipendekeza. Waandishi wa Tanzania Makanjaja tu labda Mzee Ulingwe pekee.
Wanashindwa hata kumpigania Eric Kabendera ambaye wanajua anashikiliwa rumande kinyume cha sheria kwa makala za uchunguzi dhidi ya utawala wa awamu ya 5.
 
Wanashindwa hata kumpigania Eric Kabendera ambaye wanajua anashikiliwa rumande kinyume cha sheria kwa makala za uchunguzi dhidi ya utawala wa awamu ya 5.
Hatuna Waandishi wa Habari Tanzania, tuna Makanjanja tu.
 
Kwa hiyo ulitaka akae kimya tu licha ya ukweli kuwa alitaka kuuwawa?. Huoni uhusiano kati ya njama za kutaka kumuua na uongozi wa Mkapa?.

Unawakejeli waandishi wa habari halafu na wewe unajenga hoja nyepesi zenye kustahili kukejeliwa!!.
Kwa tabia za alizonazo Jiwe kuanzia ngazi ya familia alikozaliwa, kwenye familia yake mwenyewe, shule alizosoma na mtaani alikoishi, inasadikiwa ni mtu mnoko sana na mgumu kuishi naye. Matukio ya kutaka kuuliwa kwa tabia za kinoko hayakwepeki. Naungana na waliosema kuwa kuwekewa kwake sumu mwaka 2005 haikupaswa kuwa habari kubwa kwenye magazeti kwa kuwa kwa tabia zake hilo ni jambo la kawaida.
 
Wasalaam,

Kuna tatizo la kimsingi la waandishi wetu wa habari, huenda ni kwa utashi, au uoga au muono pofu.

Hoja ya Bwana Mkapa Jana imesulubishwa na kijihoja Cha kutakiwa kuuwawa kwa bwana mmoja! Nadhani waandishi walitakiwa ku -capitalize kwenye hoja za mleta hoja lakini wengi wao wameacha hoja za msingi wamehamia kwenye habari za sumu! Kwa mtazamo wangu mpewa sumu na hasira zake na %ya uvumilivu wake nahisi mtoasumu huenda angekuwa ameletewa kifaru kipite juu yake! Just a joke!

Waandishi wameacha hoja zilizoletwa kuhusu jinsi gani New CCM wanashindwa kujua kuwa kwasasa kuna vyama vya kushindana navyo kwa hoja, wanadhani kuna koroni sugu linalotakiwa kung'olewa kwa mtutu, kiasi cha kuingiza vyombo vya usalama kukilinda!

Waandishi wameshindwa hata kupembua hoja nono kama je kwanini wajeshi wakapewaa teuzi za kisiasa katika kipindi hiki cha mfumo wa vyama vingi ambapo mtangulizi wa Raisi aliyepo alishatutoa huko tayari, je hawana datakuwa kuna wanajeshi na mapolisi wamepewa teuzi za kisiasa kama uDC au uRC au nyingine zinazofungamana na hizo?

Wanaelewa maudhui ya Bwana Mkapa kama ilikuwa ni wakeup call, kuliamsha taifa kurekebisha mapungufu badala yake kwa ukichwa panzi!
Nchini hapa mwandishi akifa ulimwengu ndobasi tena, ukitaka utamu wa kitabu hicho tafuta Tanzania daima,mana ulimwengu alifanya kazi namkapa wanajuana mno
 
Duu hii ni bonge la point tuna waandishi vichwa panzi mpaka wanaboa, na msingi wa tatizo lao ni ukosefu wa elimu
Na hata walipoambiwa wakasome wawe na digrii mwitikio wake ni mdogo sana,hapo kuna shida ya elimu.
 
Huoni kuwa hata walioenda kwenye hafla ya uzinduzi wa kitabu hicho walidivert attention kwa kuingiza mambo ya sumu ?

Kulikuwa na haja gani rais Magufuli kusema alinyweshwa sumu wakati anaweza kukaa kimya for 15 years ?

Hakuwa na mambo mengine zaidi ya kujiongelea yeye binafsi na ulaji wa sumu?
Ni kutokana na kuwa na shule tia maji tia maji
Hiyo ni hoja ya siku nyingine ila kwa Leo tunawaongelea waandishi wanapo divert attention bila kujua!!
 
Kweli kabisa, Radio njaa njaa nyingi tu na vigazeti uchwara tangu juzi zinacheza clip ya sumu tu......wamesahau maudhui mazima ya kitabu ya Mzee Ben hasa kwenye Demokrasia hasa mauaji ya Zanzibar.....Pia CCM kuiba hela za Tanesco benki kuu na kutumia kwenye uchaguzi.
 
Huoni kuwa hata walioenda kwenye hafla ya uzinduzi wa kitabu hicho walidivert attention kwa kuingiza mambo ya sumu ?

Kulikuwa na haja gani rais Magufuli kusema alinyweshwa sumu wakati anaweza kukaa kimya for 15 years ?

Hakuwa na mambo mengine zaidi ya kujiongelea yeye binafsi na ulaji wa sumu?
Ni kutokana na kuwa na shule tia maji tia maji
Okay umeelewa hoja sasa, is either alifanya maksudi kwa kujua kuwa content za kitabu zinamsuta Kwa asubuhi pimia kubwa, akajua weaknesses za wandishi wetu!

Ila waandishi Wazalendo walitakiwa wausome mchezo mapema kuliko kuwaachia waandishi "wazarendo" waharibu event nzima
 
Mnawaonea waandishi wa habari kutoa stress zenu tu.
Hapa Tanzania ni kada ipi ambayo unaweza kusema watu wake wana weledi mkubwa katika majukumu yao?

1 Mbona wanafunzi wanasoma mpaka darasa la saba wanataka hawajui kusoma na kuandika ?

2 Mbona kuna madaktari wengi tu anaacha hadi mikasi kwenye matumbo ya watu na wengine wanatoa diagnosis wrong kwa wagonjwa?

3 Mbona maengineer wetu wanajenga majengo baada ya wiki mbili jengo zima linapasuka pasuka halafu wanatuambia kuwa ni expansion joints tu ?

4 Hebu angalia hayo maprofesa yanayoteuliwa wengi wao wanabahatisha bahatisha na kujikombakomba kwa wateuzi wao kiasi cha kusahau hata misingi ya taaluma zao ?

5 Ukiangalia hapa JF kundi kubwa wanajf hawajui kuandika tu je huko kwenye kada zao wanabungua bongo kweli ?

Tusiwaonee waandishi hapa nchini hakuna kada ambayo unaweza kusema hii iko vizuri, sababu kubwa elimu yetu yenyewe tia maji tia maji tu.
Hata viongozi wetu wakubwa hawana elimu ya kuongoza.Sasa sijui tutang'ata wapi maana naona hii embe imeoza kila upande.
 
Wewe unamuona yule mzee anayeongoza kuita wenzake wapumbavu anakuja kulia lia kwa kitabu anayoyalilia alikuwa na mamlaka ya kuyabadilisha.
Hata viongozi wetu wakubwa hawana elimu ya kuongoza.Sasa sijui tutang'ata wapi maana naona hii embe imeoza kila upande.
 
Kwenye hii hoja yako naona gazeti la MWANANCHI linapigwa sana vita na vijana hapa Lumumba sababu lenyewe kila siku linachambua hoja moja kutoka kwenye kitabu suala la sumu wamelitupia mbali
 
Mkapa kwenye kitabu chake anasema Alipata Daraja la Kwanza ( Division 1) ya juu na Walifaulu 3 tu kati ya Wanafunzi 51 kutoka St. Francis (Pugu Sec) kwenda Makelele kusomea uandishi wa habari.
Hapana, mkapa hakusomea uandishi wa habari makerere.

Makerere alikwenda kusoma "shahada ya lugha, sarufi na fonetiki ya kiingereza"

Baadae sana baada ya kwenda serikali ndio akapelekwa mafunzoni kusomea uandishi wa habari.
 
Back
Top Bottom