Abubakar Karsan
Member
- Oct 27, 2019
- 62
- 45
Nimesoma kwa makini sana hoja zote zinazozungumzia utendaji kazi wa waandishi wa habari,asanteni nyote hii ni feedback nzuri sana kwetu na tutajaribu kila njia ili tuyafanyie kazi yale yaliyo ndani na uwezo wetu
Hata hivyo nina machache nataka kuongea hapa
1.Waandishi wa habari hawamiliki vyombo vya habari,ni wafanyakazi tu na tena zaidi ya hapo hawana mamlaka ya habari gani itoke na ipi isitoke,mamlaka hayo wanayo wamiliki
2.Baadhi ya wamiliki huamua habari ziandikweje ili kutowaudhi wenye mamlaka za kisiasa au kiuchumi
3.Wamiliki kwa upande wao wanadai wanatishwa kiychumi kuwa wakiandika habari zinazokosoa mamlaka,wananyimwa matangazo kwa maksudi na hatimaye wanashindwa kuendesha vyombo vyao
4.Waandishi wa habari pia wanatishwa na kudhuriwa kwa kuandika habari za ukweli na hii nyote mnaona,sasa mkumbuke hakuna habari inayozidi uhai wa mwandishi wa habari
4.Hatuwezi kabisa kuwalinganisha waandishi wa habari wanaofanya kazi na mashirika kama bbc na hawa wa kwetu wanaofanya kazi kwenye vyombo kama tanzania daima,kwani kuna tofauti kubwa sana,kimaslahi,kimuundo,kisera na kiusalama
Wakatabahu