Waandishi wa habari waache kuidhalilisha dini safi ya Uislam. Aliyeiba nguruwe sio "Imam" kwa maana alichokifanya ni kinyume na miongozo ya dini yake

Status
Not open for further replies.
Nadhani mleta taarifa hajakosea,cha kujiridhisha ni je hizi habari ni za kweli?
Viongozi wa dini si mapadre au wachungaji nyuzi zao zimerepotiwa humu mara nyingi na zinachukuliwa kama taarifa na kuanza kutafuta ukweli.
Pamoja na kuwa viongozi wa dini lakini nao ni binadamu na wala si miungu hivyo anayeleta taarifa iwe ya waislam au ya wakristo ichukuliwe kuwa ni taarifa cha msingi iwe na ukweli.Hakuna dini inayowatuma waumini wake kufanya uhalifa,ila tumeshuhudia wakifanya hivyo.
 
mjibu hoja nakupongeza , hii ni taabu ya kuwa na waandishi wasio waandishi. TAALUMA HII IMEVAMIWA . na biashara ya magazeti imekuwa ngumu kwa sasa kutokana na teknolojia. huyo muandishi uchara anatakiwa kujua KUNA UISLAMU , NA MUISLAMU.
 
Huyo mwanahabari ndio amedhalilisha nafasi ya kiongozi wa dini, na sasa Imam wote wataanza kuonekana kama wezi wa nguruwe.
Hiyo ya kusema imam kaiba nguruwe haiwezi kufanya imam wote waonekane ni wezi, ni sawa na mtu kusema mchungaji kafumaniwa guest haimaanishi wachungaji wote wana mipango ya kando kwamba wanaenda guest.
 
- Salum Yusuph adaiwa kuiba nguruwe. Au;

- Mtu mmoja adaiwa kuiba nguruwe
cheo au status ya mtu huwa inatangulia kabla ya jina la mlengwa
mf rais...., waziri mkuu....., mwalimu.....
imamu salum yusuph n.k, ukishapata cheo huwezi ukalitaja jina lako kwanza
imamu kama kaiba anatajwa kwa cheo chake kwanza .
 
Sawa boss, lakini si jambo jema kuchafua dini za wengine...
Binafsi sioni kama amechafua... yeye kaandika alichofanya huyo aliyeiba na huku akitaja aliwahi kuwa na nafasi katika jamii yake... NI SAWA NA YULE MWANDISHI WA KESHYA ALIYEANDIKA ... nanukuu... TANZANIA YAPATA SULUHU BAADA YA POMBE.... mwisho wakunukuu... Ukikurupuka na heading, unaweza panic sana...

SEMA TU WEWE UNATAKA KUTUAMINISHA KWAMBA MWANDISHI KACHAFUA UISLAM... Ni sawa na PADRE AKIFANYA UJINGA UNAPINGANA NA CHEO CHAKE, Kitatajwa alichokifanya, na cheo chake... !!! KAMA KWELI KAFANYA HIVYO, NA CHEO KWELI NI CHAKE AU ALIKUWA NACHO HUKO SIKU ZA NYUMA, MWANDISHI AMECHAFUAJE?
 
Watu wanamwambia "Kimetajwa cheo chake ili kuonesha kwamba kwa CHEO chake haifikiriwi anaweza kuiba"

Yeye anauliza "Al Shabab kwakua ni magaidi ndiyo kusema waislamu ni magaidi?"

Sasa kwani Al Shabab ni cheo jamani?
 
Wewe ndio umeikuza habari kama Yusuph angekuwa kaiba nguruwe angetajwa kama mwizi yoyote, wote tunajua nguruwe ni haramu kwa waislamu imamu kama kiongozi wa dini alitakiwa awe mfano kusimamia sheria na mafundisho ya dini.
Habari hii kuripotiwa ni taarifa kwa waislamu imamu wenu hafai kwa sababu sio mwislamu safi
 
Wewe wala siyo mkatoliki ni Muslim,huu ugaidi uliougusia kwa nn haupitii ktk dini zingine
 

Unaweza kuwa na dini lakini matendo yako yasiendane na dini
 
Aliyekuwa Waziri wa Fedha, Baziri Mramba Ahukumiwa kifungo cha Mwaka mmoja gerezani baada ya Kupatikana na hatia katika kesi iliyokuwa inamuandama.

Braza, nasoma maandiko yako mengi sana na mengi yamenielimisha kwa ukubwa sana. Sio kila kitu lazima ukifahamu au ukiandike au ukizungumze. Vingine kuwa na tabia ya kuviacha vipite. Siku zote sisi binadamu huwa tunatambuliwa kwa sifa zetu zinazotutanabaisha vyema mbele ya hadhira. Huyo kaandikwa Imam na sio Muislam kujumuisha udini wake japokuwa tunafahamu kuwa Imam ni moja kati ya Viongozi katika Uislam.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…