Waandishi wa Habari waliotembelea bandari Dubai

Kitenge kama kweli anatumika,aache,ajitambue.
 
WATANZANIA TUNA MADUDU VICHWANI
 
"4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?"
 
Duh, Aisee!!
 
 


4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
 
Balile bhana!
 
Hizi chokochoko zilishindwa. Uwekezaji ukiwa mkubwa lazima uambatane na maumivu kwa baadhi ya wanaozoea kula pale bandarini.
 
Umiliki wetu upo pale pale hakuna wa kuweza kuchukua bandari yetu, tatizo ni roho za maskini zinazochanganyika na upungufu wa uelewa kuhusu kipi haswa kinachotarajiwa kufanyika.
 
Umeandika utumbo mtupu. Unafika muda wa Tanzania kuwa sehemu ya biashara pana za kidunia, haiwezi tena kujitenga kwa hofu ya kuibiwa.

Na kwa taarifa tu ni kwamba biashara pana ya DP World bado haijaanza, na walioingia huu mkataba wametazama mbali.

Ukisema mwanamke ni mvivu kumbuka kwamba pwani ya TZ ina urefu wa kilomita 1424 ambazo ni chanzo bora kabisa cha kukuzia uchumi iwapo tunajipanga kisayansi.

Tunazo rasilimali za kutufikisha uchumi wa kati juu, kuliko hapa tunapoendelea kukwama huku ujinga wetu ukiwa ni sehemu ya mkwamo wenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…