Waandishi wa Habari waliotembelea bandari Dubai

Waandishi wa Habari waliotembelea bandari Dubai

Hawa waandishi wahabari lazima wanatoka Tbc na channel 10 . Hizi channels ni zakinafki bongo nzima cjawah ona.
Zinabagua vyama vingine, vinaficha ukweli Kwa wananchi like si kitu . yaani..
 
Kosa kubwa ni kuwa tuna raisi mwanamke,kiuhalisia wanawake wengi wanapenda sana utegemezi,wao jambo likiwa na changamoto kidogo tu ni wepesi wa kukimbia kutafuta msaada,Si ajabu mama zetu wanakopa kwenye vikoba na sehemu zingine kutatua changamoto za mavazi,kitchen party,kusuka nywele n.k wanawake hawapendi kupambana na changamoto na ndio maana Mungu alisema wawe wasaidizi tu maana alijua uwezo wao,Dunia imebadilika wanaume tumekuwa wasaidizi,ona taifa linazidi kupotea.
Ttcl na bandari kumetokea changamoto mama amekuwa mwepesi kuachia,Dunia hii hakuna jambo lisilokuwa na changamoto na lazima kuzikabili na ukishinda ndipo unaonekana shujaa,mi nadhani serikali nayo inachangamoto basi ibinafsishwe kama ubinafsishaji ndo suluhu.
Mama anatakiwa atambua hakuna mwekezaji mwenye malengo ya kukuza uchumi wetu badala ya uchumi wao,mi nadhani hata wasomi wengi ni weupe kichwani,shuleni tunasoma kabisa nature and character of capitalists,Cha kushangaza wapo wanashangilia tu eti wawekezaji wa bandari watatupatia fedha nyingi 10% ndo fedha nyingi?.pole Tanganyika umekosa msimamizi
 
Na Bashir Yakub, WAKILI

1.. WAANDISHI WA HABARI WALIOTEMBELEA BANDARI DUBAI.

Watanzania wapuuzeni sana hawa. Mtu ambaye amelipiwa tiketi ya ndege, amelipiwa malazi ya karibia wiki mbili Dubai, ametembezwa bandari za Dubai, amelipwa na posho juu mpaka anarudi hawezi kuwa na akili yake. Sio mtu huru huyu na si wa kutegemea katika maoni. Akili imeporwa na ndio kawaida ya mnyonyaji.

Mnyonyaji huwa hashughuliki na walio wengi, hushughulika na walio wachache lakini wenye sauti, na hapo huwa amemaliza dakika zake 90 za uwanjani.

Kaka yangu DEODATUS BALILE ni mwandishi ninayemheshimu sana. Bahati mbaya naye ameingia katika huu mtego. Tumsamehe huenda akarejea, Tour ya Dubai sio kitu cha kumuacha mtu salama.

Aliyewapeleka Dubai ndiye anayetaka kuwekeza na ndiye mwenyeji wao huko. Hivi mnadhani anaweza kuwatembeza maeneo yenye changamoto. Mnadhani anaweza kuwapa data maeneo aliyokwama. Mna akili nyinyi mnarudi hapa kutwambia eti mmeona msichana mdogo anabonyeza kompyuta kontena inajishusha yenyewe, nyie watu, nyie watu.

Nani kati yenu alienda Dubai na hadidu za rejea za maeneo maalum na akaomba na akaoneshwa vile inavyostahili. Naapa, mlichokiona kwa macho na kwa data ndicho mwekezaji alichopanga muone, si chini wala zaidi. Hakuna chenu mlichojipangia kuona mkaoneshwa labda kama kilikuwa chanya kwa mwekezaji.

Watanzania muwapuuze hawa si watu huru tena. Maoni yao yamehodhiwa na "DUBAI TOUR".

Mnyonyaji kabla ya kufanya hila lazima awapate baadhi ya waandishi wa habari, wanasiasa, na watu maarufu katika jamii. Kwahiyo msishangae hivi karibuni mtawaona , wasanii na watu wengine maarufu katika hili. Hii ndio ada ya mnyonyaji. Iko hivyo tangu miaka na mikaka.

Tuwaepuke madalali wa rasilimali zetu.

Yumkini tumewajua tuwakatae kwa nguvu zote. Watachagua kumrudishia mwekezaji posho zake au kutimiza walichomuahidi ambacho tunasema hakiwezekani.

2. NI KITU GANI AMBACHO HATUWEZI KUFANYA WENYEWE.

Ukisoma ule mkataba una mambo mengi lakini makubwa ni mawili tu, UBORESHAJI na UENDESHAJI. Tumeshindwa nini katika haya. Tumeshindwa kuboresha ama kuendesha.

Lipi ambalo tukiweka nia hatuwezi kulifanya. Hawa wadubai wana uwezo gani wa akili ambao hatuna. Ugonjwa wetu ni mmoja tu UVIVU.

Mtu mvivu atakuwa na shamba kubwa, anao uwezo wa kutafuta mbegu, madawa, akalima na akapata mazao na faida kubwa.

Lakini kwasababu hataki kujisumbua , hataki kusimamia, atakodisha shamba lile kwa mkataba ili yeye awe analetewa hela yake tu kila msimu bila usumbufu wowote.Huyu ndiye mtu mvivu.

Aliyekodisha shamba atalima, arapalilia, atapata usumbufu,atapata mazao, atauza , atapata hela ya kutosha, kisha amlipe mwenye shamba 10% ya mkataba yeye achukue 90%.

Mtu mvivu hataki kusimamia, mtu mvivu hataki kupambana na changamoto, mtu mvivu hataki kuumiza akili,mtu mvivu sio mbunifu,mtu mvivu yuko tayari apate kidogo sana lakini ambacho kimekuja kwa ulaini kabisa. Uvivu ni ugonjwa lakini yafaa uwe Jinai pia.

Kama sisi tumeshindwa kuendesha bandari anayekuja ataendeshaje. Atatumia malaika kuendesha ?. Tunachoacha kufanya ndio hichohicho anakuja kufanya. Ndio, tunaacha kuendesha anakuja kuendesha. Wao wana vichwa vingapi, wana akili ngapi wana nini kitu maalum ambacho hatuna.UVIVU tu

Kama teknolojia, basi hii inauzwa. Tuingie kandarasi tupatiwe teknolojia ya kisasa. Ufanisi hauwezi kuja haraka lakini tukiweka malengo tunafika. Mwekezaji mwenyewe haleti manufaa hapohapo naye atakupa malengo, atakwambia baada ya miaka kadhaa ya mkataba ndio mambo yataanza kuwa mazuri.

Malengo tunayokwepa kuweka ndiyo hayohayo anayoweka tunayempa bandari. Shida yetu ni nini. Akili yetu huwa tunaweka wapi.

Tunasumbuliwa na madalali, tufanye kila njia tuwaepuke.

3.MWEKEZAJI ANA MIGOGORO YA BANDARI KILA SEHEMU DUNIANI.

Huyu huyu Mwekezaji DP World ana migogoro ya kimkataba karibia kila sehemu duniani katika mahakama ya Kimataifa ya Migogoro ya Uwekezaji ICSID.

Ana mgogoro wa Bandari na Brazil wa mwaka 2014.
Ana mgogoro na Uruguay wa mwaka 2016.
Ana mgogoro Argentina wa Mwaka 2018.
Ana mgogoro na Pdkistan wa Mwaka 2020 nk ,nk.

Migogoro yote hii ipo ICSID na yote ni mikataba ya bandari. Nani kamleta huku kwetu tena. Nini mnataka na huyu mwekezaji.

Hatujamaliza hata maumivu ya mkataba wa TICTS mnakuja na hiki kidudu mtu tena. Hatutakubali.


4.NANI AMELETA WAZO HILI.

Bila shaka sio Tanzania ni mwekezaji mwenyewe. Hakuna shaka sio wazo letu ni la mwekezaji. Aliyechumbia ni niwekezaji na tunacheza ngoma yake. Kwahiyo viongozi hamna haja ya kushupaza sana misuli ili kuonekana mna maono saaaana, hamna kitu, halijawahi kuwa wazo lenu hili. Sio wazo lenu.

Na ushahidi ni kuwa, kawaida wazo lingeanzia kwetu tungetangaza Tenda wakajitokeza washindani ambaye angeshinda angeingia mkataba.

Hamshangai jambo hili halina tenda!!!, Ni kwasababu mwenyewe amekuja na wazo lake mija kwa moja na hivyo huwezi kumshindanisha.

Nataka kusema nini hapa, huyu amekuja kutafuta oppurtunity na si kuisaidia Tanzania. Amekuja kutafuta ukwasi. Naona viongozi wengi mnaongea kana kwamba sasa ndio wakati wa kufaidika,huyu mtu ni mzuri sana, ataisaidia nchi, atainua uchumi, ataleta maendeleo, ajira zitamwagika nk.

Hamjifunzi tuu, ni mwekezaji gani tokea mmeanza kuwapokea wawekezaji, kuanzia wale wa migodini nk. amewahi kuwafikisha katika hayo. Ni yupi tangu sera za Mkapa za Ubinafsishaji ziingie.

Mwekezaji ni mfanyabiashara anaangalia faida yake period.

Ni hivi, hakuna mwekezaji anaweza kuendeleza nchi yako. Mtu pekee wa kuendeleza nchi yako ni wewe mwenyewe. Umeshindwa wewe na nchi imeshindwa, umefanikiwa wewe na nchi imefanikiwa.

Tuache UVIVU tusimamie bandari yetu. Bandari inahitaji usimamizi tu na si vinginevyo, na mwekezaji hatafanya kingine chochote zaidi ya kusimamia.

Tuna nini sisi vichwani.
Bashir Yakub....wakili....dalali....[emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Hivi kaka yetu wakili Bashir Yakub anataka kutuambia kuwa kamarada sana kaka mkubwa Deodatus Balile ni "kuwadi" wa anachofanya kilicho tofauti na madalali "mawakili"?!!!! [emoji15][emoji15][emoji15][emoji1787][emoji1787]

Hivi huu ni UWEKEZAJI wa kwanza kufanywa nchini kwetu?!!!

Hivi wekezaji nyingine zote huwa hakuna kutambulisha nguvu ya mwekezaji huko ATOKAKO ?!!!

Wakili Bashir Yakub atutajie WAANDISHI WA HABARI waliokwenda nchini MISRI kabla ya ARAB CONTRACTORS hawajaanza kazi zao bwawa la uzalishaji umeme mwalimu Nyerere?!!!

Walikuwa ni WAANDISHI wangapi?!!!

Nani na nani ?!!!

Walikaa siku ngapi Misri?!!!

Ama hajui ?!!

Hawajui ?!!!

Hajataka kuwajua?!!

Hivi Waturuki Yerpi Merkez wa reli ya "SGR" hawakupeleka WAANDISHI wa habari UTURUKI?!!!

Mbona Wakili Bashir hakupata kuandika na kuchambua kama ambavyo anamchambua kamarada Deodatus Balile?!!!

Wakili "dalali" ana yake....ana yake nasema [emoji1787][emoji1787][emoji1787]

#SiempreJMT[emoji120]
 
Nilikuwa nafanya kazi kwenye bandari kavu moja, wakiingiza makontena 7 basi 2 au 3 hayalipiwi kodi. Na kampuni ni kampuni ambayo ina mkono wa wanasiasa waandamizi. Kwahiyo tatizo la bandari ni usimamizi tu. Viongozi wanapitisha konteina bila kulipa kodi. Ni ulafi wa wanasiasa wasiompenda kutosheka. Ndiyo wanaodholotesha utendaji wa bandari. Ugumu upo wapi? Ni pale kamati ya bunge inabidi isimamie utendaji wa bandari. Inashindwa kutokana nyuma ya pazia kuna wanasiasa waandamizi, ambao kwenye kamati za chama wenyewe ndiyo walioshika mpini. Sasa nani wakumvisha paka kengele? Ni utashi tu wa serikali kuongeza mapato bila kumpa mwekezaji inawekana, ila kupanga ni kuchagua. Tutumbue majibu ya bandari ili iwe tiba ya kudumu au tumpe wekezaji ili tukalibishe ukoloni mamboleo.
 
Hawa waarabu ni kuwatimua wote waliopo tanganyika
Huna uwezo huo....huna uthubutu huo....wako watanzania wenye asili ya kiarabu na wewe hobobo si raia wa daraja la juu kuwazidi wao....

Huna haki/nguvu/uthubutu wa kumpangia raia mwenzako....

#SiempreJMT[emoji120]
 
In Short list ni kubwa, watu wamepewa magari na nyumba, walipanda ndege first class kwenda Dubai na wamejengewa nyumba sehemu za Dar na mikoani kutokana na takwa la mtu;
Wamepewa fedha, wana baraka za kufanya hivyo;
Hiyo list ukitaka ingia kwenye pages zao, utaona wanavyopush hii agenda ya MANGUNGO WA MSOVERA.
Mtake msitake....

Mradi huooo....
 
Waarabu wamedhamiria kuiangamiza Tanzania
Wewe utakuwa mjinga....

Wawekezaji wa migodini ni WAZUNGU....hawajatuangamiza?!!!

Aje mwarabu ,mzungu ,mchina ,mhindi mwekundu....tutakacho sisi ni MAENDELEO makubwa zaidi ya WIZI UENDELEAO TPA......
 
Hakuna Mwandishi tapeli Kama balile! Ukimsikiliza unaweza kudhani huyu ndio mtu! Likn ukimfuatilia Ni mtu hatari Sana.
Argumentum ad hominem....

Bashir Yakub amekutajia "list" ya WAANDISHI waliopelekwa Misri na "ARAB CONTRACTORS"?!!! [emoji15][emoji15][emoji1787]
 
Hili ni andiko Bora zaidi hapa jf,hakika Mungu asimame nasi huyu mama ameamua kuwauzia warabu nchi yetu,Si punde tutakuwa landlocked country.
Imetengenezwa PROPAGANDA ya chuki dhidi ya mh.Rais SSH....wanajulikana walioko nyuma ya hayo.....ni ubaguzi tu....ni kukatwa tu "mirija " yao....kifupi si mapya.....

#SiempreJMT[emoji120]
 
Balile sijawahi kumuamini
....unamuamini mh.Mbowe tu....

Nakukumbusha kitu....

Mbona Chadema mlikuwa mnampenda kipindi kileee "CHA NGOME" kule Mbezi Beach wakati mh.Laigwanan ENL anawamwagia "manoti" tu ?!!![emoji1787][emoji1787]
 
Ni waarabu wangapi wamekuja kuwekeza kuchimba MADINI ?!!!!

Wengi ni WAZUNGU....

Toka tupate uhuru....hadi alipokuja hayati JPM...nchi ilikuwa inapata "mrahaba"- dividend 3%....sasa sijui MASHIMO YETU yanayojaa maji amesababisha MWARABU ama MZUNGU?!!!

Ukimuona mtu anaongelea "racism" katika masuala ya uwekezaji....mbatize ubini....ZAMWAMWA ZAMWAMWA ZAMWAMWA [emoji1787][emoji1787]
 
Back
Top Bottom