Waandishi wa Habari waliotembelea bandari Dubai

Kuna watanzania wanatakiwa kuwekwa kwenye list ya maadui wa taifa, ukianza na Samia na Mbarawa, anayefuatia ni huyo mzee Balile, mwanaume mpuuzi anayejipendekeza kwa mwanamke ilimradi ajaze tumbo.
labda mamaako
 
CCM ni chama Cha hovyo sana, yaani unantumia Msukuma na Kibajaji kudrive issue sensitive Kama ya Bandari??, Bora hata Magufuli aliwatumia kina Prof Kabudi wakadanganya wakaeleweka.
Wtz ukiwasikiliza kwenye rooms za club house utacheka nakuona tuna ujinga mwingi, eti tunauliza Bunge likiidhinisha huo mkataba inakuwaje?. Binafsi ningesema kila jimbo litamke Kama Bunge litapitisha huu upuuzi basi mbunge afie ndani kwake choma kila kitu iwe starting point ya mapinduzi... Tumezid maneno bila vitendo, tumekalia siasa za chadema na CCM hata kwenye Mambo ya kitaifa.
 
Hakuna dua inayoweza kupigwa
na kisha wabunge wote wenye nia mbaya na nchi wakatangulia?
Hasa wa CCM
 
Hakuna Mwandishi tapeli Kama balile! Ukimsikiliza unaweza kudhani huyu ndio mtu! Likn ukimfuatilia Ni mtu hatari Sana.
Maulidi wa-KANGA anamzidi huyo, msome vizuri kwanini kila kitu kikitokea hakihusu michezo anapelekwa wa kwanza, aende kupush agenda, wanajua ana influence na foloweers wengi, naamini sasa watu wata mu- unfollow.
 
Watu wanashindana kujenga mahoteli waachie fursa huku hakuna wakuwagusa Wala kuwahoji hata ingekuwa wewe mambo yangekuwa hayo hayo!
 
Na Bashir Yakub, WAKILI

1.. WAANDISHI WA HABARI WALIOTEMBELEA BANDARI DUBAI.

Watanzania wapuuzeni sana hawa. Mtu ambaye amelipiwa tiketi ya ndege, amelipiwa malazi ya karibia wiki mbili Dubai, ametembezwa bandari za Dubai, amelipwa na posho juu mpaka anarudi hawezi kuwa na akili yake. Sio mtu huru huyu na si wa kutegemea katika maoni. Akili imeporwa na ndio kawaida ya mnyonyaji.

Mnyonyaji huwa hashughuliki na walio wengi, hushughulika na walio wachache lakini wenye sauti, na hapo huwa amemaliza dakika zake 90 za uwanjani.

Kaka yangu DEODATUS BALILE ni mwandishi ninayemheshimu sana. Bahati mbaya naye ameingia katika huu mtego. Tumsamehe huenda akarejea, Tour ya Dubai sio kitu cha kumuacha mtu salama.

Aliyewapeleka Dubai ndiye anayetaka kuwekeza na ndiye mwenyeji wao huko. Hivi mnadhani anaweza kuwatembeza maeneo yenye changamoto. Mnadhani anaweza kuwapa data maeneo aliyokwama. Mna akili nyinyi mnarudi hapa kutwambia eti mmeona msichana mdogo anabonyeza kompyuta kontena inajishusha yenyewe, nyie watu, nyie watu.

Nani kati yenu alienda Dubai na hadidu za rejea za maeneo maalum na akaomba na akaoneshwa vile inavyostahili. Naapa, mlichokiona kwa macho na kwa data ndicho mwekezaji alichopanga muone, si chini wala zaidi. Hakuna chenu mlichojipangia kuona mkaoneshwa labda kama kilikuwa chanya kwa mwekezaji.

Watanzania muwapuuze hawa si watu huru tena. Maoni yao yamehodhiwa na "DUBAI TOUR".

Mnyonyaji kabla ya kufanya hila lazima awapate baadhi ya waandishi wa habari, wanasiasa, na watu maarufu katika jamii. Kwahiyo msishangae hivi karibuni mtawaona , wasanii na watu wengine maarufu katika hili. Hii ndio ada ya mnyonyaji. Iko hivyo tangu miaka na mikaka.

Tuwaepuke madalali wa rasilimali zetu.

Yumkini tumewajua tuwakatae kwa nguvu zote. Watachagua kumrudishia mwekezaji posho zake au kutimiza walichomuahidi ambacho tunasema hakiwezekani.

2. NI KITU GANI AMBACHO HATUWEZI KUFANYA WENYEWE.

Ukisoma ule mkataba una mambo mengi lakini makubwa ni mawili tu, UBORESHAJI na UENDESHAJI. Tumeshindwa nini katika haya. Tumeshindwa kuboresha ama kuendesha.

Lipi ambalo tukiweka nia hatuwezi kulifanya. Hawa wadubai wana uwezo gani wa akili ambao hatuna. Ugonjwa wetu ni mmoja tu UVIVU.

Mtu mvivu atakuwa na shamba kubwa, anao uwezo wa kutafuta mbegu, madawa, akalima na akapata mazao na faida kubwa.

Lakini kwasababu hataki kujisumbua , hataki kusimamia, atakodisha shamba lile kwa mkataba ili yeye awe analetewa hela yake tu kila msimu bila usumbufu wowote.Huyu ndiye mtu mvivu.

Aliyekodisha shamba atalima, arapalilia, atapata usumbufu,atapata mazao, atauza , atapata hela ya kutosha, kisha amlipe mwenye shamba 10% ya mkataba yeye achukue 90%.

Mtu mvivu hataki kusimamia, mtu mvivu hataki kupambana na changamoto, mtu mvivu hataki kuumiza akili,mtu mvivu sio mbunifu,mtu mvivu yuko tayari apate kidogo sana lakini ambacho kimekuja kwa ulaini kabisa. Uvivu ni ugonjwa lakini yafaa uwe Jinai pia.

Kama sisi tumeshindwa kuendesha bandari anayekuja ataendeshaje. Atatumia malaika kuendesha ?. Tunachoacha kufanya ndio hichohicho anakuja kufanya. Ndio, tunaacha kuendesha anakuja kuendesha. Wao wana vichwa vingapi, wana akili ngapi wana nini kitu maalum ambacho hatuna.UVIVU tu

Kama teknolojia, basi hii inauzwa. Tuingie kandarasi tupatiwe teknolojia ya kisasa. Ufanisi hauwezi kuja haraka lakini tukiweka malengo tunafika. Mwekezaji mwenyewe haleti manufaa hapohapo naye atakupa malengo, atakwambia baada ya miaka kadhaa ya mkataba ndio mambo yataanza kuwa mazuri.

Malengo tunayokwepa kuweka ndiyo hayohayo anayoweka tunayempa bandari. Shida yetu ni nini. Akili yetu huwa tunaweka wapi.

Tunasumbuliwa na madalali, tufanye kila njia tuwaepuke.

3.MWEKEZAJI ANA MIGOGORO YA BANDARI KILA SEHEMU DUNIANI.

Huyu huyu Mwekezaji DP World ana migogoro ya kimkataba karibia kila sehemu duniani katika mahakama ya Kimataifa ya Migogoro ya Uwekezaji ICSID.

Ana mgogoro wa Bandari na Brazil wa mwaka 2014.
Ana mgogoro na Uruguay wa mwaka 2016.
Ana mgogoro Argentina wa Mwaka 2018.
Ana mgogoro na Pdkistan wa Mwaka 2020 nk ,nk.

Migogoro yote hii ipo ICSID na yote ni mikataba ya bandari. Nani kamleta huku kwetu tena. Nini mnataka na huyu mwekezaji.

Hatujamaliza hata maumivu ya mkataba wa TICTS mnakuja na hiki kidudu mtu tena. Hatutakubali.

4.NANI AMELETA WAZO HILI.

Bila shaka sio Tanzania ni mwekezaji mwenyewe. Hakuna shaka sio wazo letu ni la mwekezaji. Aliyechumbia ni niwekezaji na tunacheza ngoma yake. Kwahiyo viongozi hamna haja ya kushupaza sana misuli ili kuonekana mna maono saaaana, hamna kitu, halijawahi kuwa wazo lenu hili. Sio wazo lenu.

Na ushahidi ni kuwa, kawaida wazo lingeanzia kwetu tungetangaza Tenda wakajitokeza washindani ambaye angeshinda angeingia mkataba.

Hamshangai jambo hili halina tenda!!!, Ni kwasababu mwenyewe amekuja na wazo lake mija kwa moja na hivyo huwezi kumshindanisha.

Nataka kusema nini hapa, huyu amekuja kutafuta oppurtunity na si kuisaidia Tanzania. Amekuja kutafuta ukwasi. Naona viongozi wengi mnaongea kana kwamba sasa ndio wakati wa kufaidika,huyu mtu ni mzuri sana, ataisaidia nchi, atainua uchumi, ataleta maendeleo, ajira zitamwagika nk.

Hamjifunzi tuu, ni mwekezaji gani tokea mmeanza kuwapokea wawekezaji, kuanzia wale wa migodini nk. amewahi kuwafikisha katika hayo. Ni yupi tangu sera za Mkapa za Ubinafsishaji ziingie.

Mwekezaji ni mfanyabiashara anaangalia faida yake period.

Ni hivi, hakuna mwekezaji anaweza kuendeleza nchi yako. Mtu pekee wa kuendeleza nchi yako ni wewe mwenyewe. Umeshindwa wewe na nchi imeshindwa, umefanikiwa wewe na nchi imefanikiwa.

Tuache UVIVU tusimamie bandari yetu. Bandari inahitaji usimamizi tu na si vinginevyo, na mwekezaji hatafanya kingine chochote zaidi ya kusimamia.

Tuna nini sisi vichwani.
Hili ni andiko Bora zaidi hapa jf,hakika Mungu asimame nasi huyu mama ameamua kuwauzia warabu nchi yetu,Si punde tutakuwa landlocked country.
 
Hivi bandari ya Dubai inasimamiwa na hawa DP?
Kwa nini wasingewapeleka na kwingineko hata huko Brazil?
Hapo kuna jambo.
Dunia ya leo kukataa wawekezaji ni mawazo mgando...
Tatizo si wawekezaji ila tunanufaikaje na uwekezaji wao...hap ndio inabidi tukae sawa mikataba itunufaishe.
Rushwa wakati wa negotiation ndio inatufanya tupate hasara kwa hiyo tatizo liko kwetu na si wawekezaji.
Dunia ya leo ukisubiri tender itangazwe ndio ushindanie hutafanya biashara ni lazima uoneshe mteja ana changamoto gani na namna utampa suluhisho kwa hiyo ni juu ya mteja kuwa makini kuangalia ananufaikaje.
Kwa kifupi bandari imetushinda na tunahitaji mwekezaji serious ila tatizo ni viongizi wetu ambao wanataka asilimia zao sababu utakuta hizo terms hata mwekezaji hakuaj nazo ila watu waliziingiza wapate chao.
Hivi kweli bila rushwa mtu utakubali kipengele cha mkataba kutovunjwa hata kama mwekezaji kazingua?
Halafu eti ndio wanajiita wazalendo hii nchi inahitaji maaamuzi magumu kubadili upuuzo huu.
 
Back
Top Bottom