Waarabu na wazungu waliondoa dini zetu za asili ili tuabudu Nyota/Mwezi na Sanamu za bikra maria

Waarabu na wazungu waliondoa dini zetu za asili ili tuabudu Nyota/Mwezi na Sanamu za bikra maria

Unahusianisha Dini na Science hapa umechemka

Science haina dini babu

China ndo nchi inayoongoza kwa upagani lakini ndio inaongoza kwa science na technologia
We ndo umechemka mzee.... Hivi unadhani dini ni kwenda kanisani au msikitini pekee!!!

Dini ni mfumo mzima wa maisha ya mtu kwanzia anavyoamka mpk atavyorudi kulala.
Hayo mambo ya kuwaita wachina wapagani unayajua wewe wao wanadini yao (Kama wew unavyowaona wapagani na wewe wanakuona mpagani maana haufati taratibu za dini yao)

Science na dini vipo hapa kwa hapa.... Huwezi vitenganisha sababu vyote mlengwa wao n binaadam

Mungu mwenyew alimtengenezea Adam nguo baada kujigundua yupo uchi.... Process ya kuchukua malighafi akazichakata zikatoa product mpya ambayo ni nguo, kwa lugha nyepesi huo tunaita n utendaji wa kiwanda

Pale haukufanyika muujiza bali ilitumika sayansi (kumfunza mwanaadam ajue kujistiri kwa mapambo ya nguo)
 
labda kwene kabila lenu!
Ikumbukwe kila kabila lilikua na namna yake ya kuabudu
 
kiongozi mi siongei bla bla
 

Attachments

  • FED0EB37-7B45-47C6-8086-44AC46B7081D.jpeg
    FED0EB37-7B45-47C6-8086-44AC46B7081D.jpeg
    37.4 KB · Views: 2
Mnapenda Kweli kulinganisha Uisilamu na kila kitu kinachofanywa na wakristo,

Uisilamu hauna mahusiano yoyote na symbol ya nyota na mwezi bali ni Symbol tu ya Taifa La Ottoman, Si Quran wala si hadithi zinataka hizo symbol kuwa part ya Imani.
sasa kama ni ottoman mnaiweka kwene misikito ya nn??
Na mnavoendaga kubusu kimondo?? si ndo kuabudu jiwe
 
Kiafrika hazikuwa na mambo ya ajabu ajabu kwa umri wangu nimekua nikishuhudia babu zangu wakifanya rituals mbalimbali hazikushirikisha uvunjifu wa haki za watu.

Matambiko mengi ya Kiafrika especially Tanzania hayahusishi ukatili kwa binadamu,bahati mbaya sana kizazi chetu hakijarithishwa mambo ya mila za Kiafrika tumerithi dini za wageni.
Hii ni revisionism tu, huyo babu yako tayari alishaathirika na Mila za Dini kwa maelfu ya miaka.

Tafuta Vitabu vya Ibn Batuta mtu pekee ambaye kaitembelea Africa kipindi hiko hata wazungu hawajakuja, ni jambo la kawaida kwa Dini za Asili Chief akifa azikwe na msichana Bikra, Mila za Kutoa kafara watu zilikuwepo, kuoana ndugu baba na mtoto, dada na kaka Etc.

Kuna mambo mengi mno mpaka hao waojiita Atheist wanayafanya ila ni Mila ambazo zimeletwa na Dini, kifupi civilization ya sasa kwa kiasi kikubwa ni Dini ndio imeeka.
 
sasa kama ni ottoman mnaiweka kwene misikito ya nn??
Na mnavoendaga kubusu kimondo?? si ndo kuabudu jiwe
Kuna misikiti wanaweka kuna misikiti hamna ni optional na huswali kuelekea Nyota ama mwezi.

Pia kubusu kitu ni tofauti na kukisujudia ama kukiabudu ama kukiomba msaada, hakuna muisilamu ama kitu chochote kwenye dini kwamba ukiliomba dua hilo jiwe litakutimizia matakwa yako.

Ni utofauti kabisa na wanoomba sanamu la yesu, Bikra Maria ama waabudu masananmu wengine
 
Kiafrika hazikuwa na mambo ya ajabu ajabu kwa umri wangu nimekua nikishuhudia babu zangu wakifanya rituals mbalimbali hazikushirikisha uvunjifu wa haki za watu.

Matambiko mengi ya Kiafrika especially Tanzania hayahusishi ukatili kwa binadamu,bahati mbaya sana kizazi chetu hakijarithishwa mambo ya mila za Kiafrika tumerithi dini za wageni.
Labda hakukuwa na kafara, sijui, sina uhakika.

Lakini tuliishi kama wanyama....

Mfano tu kwa sisi wachaga ilikuwa ukipata homa dawa unatemewa mate mara 80, halafu mwisho unatemewa kwenye matundu ya pua, kisha yanapulizwa yafike kichwani...

Jando yetu(ngasi) ilikuwa ni lazima mtu mmoja afe. Mnaambiwa mumuue mnaemuona ni dhaifu au amelemaa. Huo ndo kama mtihani wa mwisho...
 
unachoongelea hata hukijui

mbona hakuna uhusiano kati ya matambiko na kuishi kwa tabu
Nimezaliwa maeneo ambayo mpaka miaka ya 90-2000 walikua wana mambo ya uchifu, ilikua tabu kwa wakazi wa pale hasa wafanyabiashara, kulikua na imani za ajabu ajabu kuwafavour hao machifu na kuwatisha raia.
 
Back
Top Bottom