Parabolic
JF-Expert Member
- Dec 3, 2013
- 2,922
- 3,252
DAR. Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka Dar es Salaam (DART) umeingia mkataba wa miaka 12 na kampuni binafsi ya usafirishaji ya Emirates National Group (ENG) kutoka Abu Dhabi kuendesha mfumo wa BRT jijini Dar es Salaam.
Soma pia: Mabasi mwendokasi
Mkataba huo ulisainiwa rasmi Ijumaa, ukiashiria hatua muhimu katika jitihada za serikali kuboresha huduma za usafiri wa umma katika jiji la kibiashara.Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa DART, Dk. Athumani Kihamia, ENG itachukua uendeshaji wa awamu ya kwanza ya mradi wa BRT na kuleta mabasi mapya 177 yatakayoongeza ufanisi na upatikanaji wa huduma jijini.
Mchakato huo ulianza mwaka 2017 kupitia mfumo wa ubia kati ya sekta ya umma na binafsi (PPP), lakini ulipata changamoto za kimajadiliano kuhusu viwango vya nauli na mifumo ya usuluhishi.Mnamo 2020, serikali ilitangaza zabuni upya ambapo kampuni 40 ziliwasilisha maombi, na ENG ikaibuka mshindi. Hatimaye, mchakato huo sasa umekamilika kwa kutiwa saini kwa mkataba rasmi wa utekelezaji.
Chanzo: Habari Leo