Waarabu wana mafanikio gani tangu waanze kufuzu Kombe la Dunia

Waarabu wana mafanikio gani tangu waanze kufuzu Kombe la Dunia

alaf kwa nn ata wasingepambanishwa wenyew kwa wenyew ila wapunguze tim za kiarabu uko mf Misri vs Tunisia au Algeria vs Morocco alf game zao ukiondoa Misri wote wanamalizia nyumban kwao.

Kwani waarabu wakituwakilisha kuna tatizo gani? Huwa tunapenda sana kulalamika tunabaguliwa na wazungu, sasa hiki kinachotokea kwa mleta mada na wafuasi wake ni dhahiri wabaguzi.
 
Rekodi za Nigeria, Ghana,Cameroon na senegal zinaeleweka kombe la dunia huwa wanatufutia aibu

Je, hawa waarabu wanarekod yeyote nzuri? Wakienda kombe la dunia? Wameshawahi kuvuka hata makundi?

Kwanini wamefanikiwa soka la africa lkn wakivuka mpaka wa bara wanakuwa kama timu za ndondo?
Kwa nini uwaze mambo ya waarabu badala ya kuwaza timu yetu ya Taifa Stars!
 
Wao ndio wanainflunce upangaji wa ratiba makao makuu ya shirikisho yapo misri wanajua sana kuchezesha

Unateseka sana,,,furaha yangu pia waarabu wakichomoza, wala sitaumia. Ila kuna wengine mfano wako wanaumia na kuteseka 😁 Mungu awabariki waarabu, tunawapenda sana kama tunavyo wapenda wengine.
 
2014 Algeria ilifika 16 bora. Akaenda 90 na Germany droo . Akaenda 120 ndio wakafungwa. Huku wakiwa kwenye mfungo wa Ramadhani. Ujerumani hiyo iliipiga 7-1 baadaye. Ikaenda ikachukua kombe

Mleta mada ana lake jambo sio kwa chuki hizo. Na asipojiangalia na kudhibiti hasira/chuki zake atapata presha aise
 
afu acha maswali ya kibaguzi unavouliza warabu taja taifa huska Iran,Saudi Arabia, Oman ,wote ni warabu

Hapa huwa wananiacha njia panda mkuu 😁 anashindwaje kutaja jina la nchi mpaka aseme waarabu!😁 mfano wakutane S.Afrika na Saudi Arabia, huwezi kukuta waarabu au wazungu wanasema waafrika wamefungwa na Saudia Arabia. Ila huku sasa 😱

Twendelee kukemea Ubaguzi
 
Tukubali kuwa waarabu ni mizigo wanaaibisha africa

Huna hoja,, wadau wanajitahidi kuleta statistics, wewe umekalia kuwaponda tuu. Ubaguzi utakumaliza kijana. Wewe na huyu ndugu yako permanides badilikeni, acheni ubaguzi na udini.

Msije mkasema "udini umeingiaje hapa" lakini wadau tulionao humu, wanaelewa nini maana ya mpira na wamejibu kwa hoja za msingi, so bado hawakujuweni kama ninyi ni wabaguzi na wadini.
 
Co wew kitendo Cha warabu kutofika robo fainali ndio unaona hawana mafanikio ao warabu unaona hawana mafanikio ndio watakua wakishirikishi wako 2022 aligeria,egypty ,Tunisia,morroco jiande kuwatazama

Hofu yangu kubwa kwa huyu utah jazz na jamaa yake permanides wasijinyonge tu kwa kitakachotokea😁 kama wale wanaojiuwa kisa wivu wa mapenzi😁 ngoja tusubiri Millard ayo atuletee taarifa za matukio mnamo siku ya juma4, baada ya mechi kumalizika😁
 
Munateseka sana na Waarabu, Ila hawa waarabu ni hatari sana, wanawanyoosha wabantu mpaka wanaishia kumwaga povu la chuki tu mitandaoni.

Kwa kifupi tu kati ya timu 5 zinazokwenda world cup 4 zitakua ni za kiarabu.
Katika timu 8 ambazo zitacheza robo fainali ya CAF champion league msimu huu 6 ni za kiarabu
Katika timu 8 ambazo zitacheza robo fainali ya CAF Confederation msimu huu 5 zinatarajiwa kuwa ni Za kiarabu

SO wamatumbwi acha waendelea kumwaga povu tu

Wataelewa somo, wee subiri tu
 
Leo tukiwa sehemu tumejadili hii mada. Naikuta tena hapa.
Tukazungumzia Egypt inavyokuwa mdobwedo hata akikutana na nduguze Saud Arabia.
Kwani Egypt sio Afrika? Au upoyoyo wako unakufanya ufikiri Afrika ni ya Wabantu tu? Hao Saudi Arabia kwa maana ya Wabantu basi ni nduguzo zaidi ya Wamisri. Wamisri ndugu zao wa Karibu sana hapa Tanzania ni Wajaluo na kama hao "Nilo hamites".
 
Hivi kuna tofauti gani ya perfomance kwenye World Cup kwa nchi za Africa?

Unaonekana hujui kitu.. kwa kukusaidia tu nimekuwekea timu zilizoshiriki kutoka Africa.

Cameroon: Wameshiriki mara 7.. Ukiacha kufika Robo fainali mwaka 1990 waliposhiriki kwa mara ya kwanza, hawajawahi kuvuka makundi tena.

Nigeria: Wameshiriki mara 6 , wamevuka makundi mara mbili tu.


Ivory Coast: Hawajawahi kuvuka makundi.

Senegal: Wamevuka makundi mara moja tu

Morocco: Wamevuka makundi mara mbili.

Algeria: Wamevuka makundi mara mbili.

Ghana: Wamevuka makundi mara mbili.

Egypt: Wameshiriki kombe la Dunia mara mbili tu, hawajawahi kuvuka makundi.

South Africa: Wameshiriki mara mbili. Hawajawahi kuvuka makundi.

Tunisia: Hawajawahi kuvuka makundi.

Angola: Wameshiriki mara moja, hawakuvuka makundi.

Togo: Wameshiriki mara moja, hawakuvuka makundi.

Zaire: Wameshiriki mara moja tu., hawakuvuka makundi. Walifungwa goli 9-0 na Yugoslavia mwaka 1974.


Nchi nyingi za Africa hufanya vizuri mara ya kwanza wanaposhiriki Cameroon, Senegal walifika hatua ya Robo Fainali mara yao ya kwanza kushiriki i.e 1990 na 2002 respectively.
..
.
Attention: Fanya masahihisho hapo kwa Cameroon, walishiriki kombe la dunia mara ya kwanza mwaka 1982 na hawakuvuka hatua ya makundi lakini waliposhiriki kwa mara ya pili mwaka 1990 ndio wakafika robo fainali na kutolewa na England.
 
Kwani Egypt sio Afrika? Au upoyoyo wako unakufanya ufikiri Afrika ni ya Wabantu tu? Hao Saudi Arabia kwa maana ya Wabantu basi ni nduguzo zaidi ya Wamisri. Wamisri ndugu zao wa Karibu sana hapa Tanzania ni Wajaluo na kama hao "Nilo hamites".
Hii sio kweli, wajaluo hawana ukaribu wowote na waarabu wa Misri. Wakati waarabu wa Misri ni Semitic, wajaluo wao ni Nilotic asili yao ikiwa ni jimbo la Bahar El Ghazal ambayo leo iko kaskazini magharibi mwa South Sudan.
 
Back
Top Bottom