Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Hapo majuzi nchi tano za kiarabu ziliahidi kusimamia mpango wa kuijenga Gaza kwa gharama ya dola bilioni 53.Ni jambo zuri sana lakini ni maamuzi ya kizembe sana.
Wakati ahadi hiyo ikitolewa ilishapita wiiki 2 Israel ikiwa imezuia mahitaji yote kuingia Gaza tena katka mwezi mtukufu wa Ramadhani.Si kuzuia vyakula tu,bali Israel imeendelea kupiga maeneo tofauti ya Gaza na kuua watu kadhaa ikiwa ni uvunjifu wa mkataba wa kusitisha vita wa wazi wazi.
Uvunjwaji wa majengo karibu yote ya Gaza usingetokea iwapo tangu mwanzo nchi za kiarabu zingeamua kuizuia Israel kivitendo kwa namna moja au nyengine.
Kama ni ujirani au haja ya kuwa na amani na jirani basi hata Mexico na Canada pia zinapenda jambo hilo lakini wanapoona heshima na maslahi yao yanakandamizwa na jirani yao ,Marekani basi na wao wameamua kupigana kiume na sera za Trump
Kwa kuacha madhila kwa wapalestina kuendelea kila siku hata baada ya mikataba ya amani kunatoa tafsiri gani kwa nchi za kiarabu.