Waarabuni wa Dubai waomba zabuni ya kuendesha Mabasi ya Mwendokasi

Napongeza maamuzi ya serikali kuwapa wawekezaji huu mradi ,

Napendekeza mashirika mengine yapewe wawekezaji wenye sifa na uwezo bila kujali ni wa NDANI au wa nje
Kila siku tunalalamika HUDUMA mbovu za mwendokasi
Ikiwezekana Kila mwekezaji apewe router yake ili kuongeza ushindani
 
Hivi hii Serikali yetu inaweza kufanya kitu gani hasa?
Leo nimegundua pengine hujui unachotaka au unachosimamia

Natamani yasiwe ndo mawazo ya chama Chako
Maana kitaonekana chama kisichokua kinachotaka au Kusimamia kwenye nchi
 
Hamna kitu ndugu yangu.Utashangaa hizo Kampuni wanazisema ni za Watanzania ni za hao vigogo. Watapambana wachukue hiyo tender halafu waturudishe kulekule
Kama ni za watanzania na Zina vigezo na uwezo kwanini wasipewe tender ?
Unajitambua kweli wewe kipi unasimamia ?
 
Hongera mkuu kwa mawazo chanya kabisa
Serikali iachane na Biashara ni kupoteza Kodi zetu bure
 
Reactions: Tsh
Tanesco na TTCL mbona hazibinafusishwi?
Hayo ni moja ya mashirika yanajiendesha kwa hasara kubwa
Kuna kipindi ilikadiriwa Tanesco inajiendesha kwa hasara ya shilingi million 400
Ushasikia Tena line za Ttcl
Serikali kujiingiza kwenye Biashara ni ukichaa
 
INGAwa sikuungi mkono hoja zako zote Ila umeongea point
 
nashauri wampe yeyote mwenye uwezo,hata kama ni mwarabu,apewe. watu wanapata shida sana mwendo kasi, ukipita unawaona wamekaa kwenye stand wameshika tama wamekata tamaa kabisa, raia wanapata shida, leteni mwekezaji haraka tena mwenye uwezo na experience ya nje.
 
Umeongea hoja nzito mkuu,
Naona
Bado hutujaweza kuundaa watu wenye uwezo wa kuendesha miradi mikubwa na maono makubwa
Ila kuliko mradi ufe wapewe wenye uwezo watanzania wakijipanga
 
Kwa asili binadamu wengi ni wabinafsi Sana na hili tatizo kwa watanzania ni kubwa zaidi
Jambo likishakuwa la umma hata Kama ana uwezo atafanya hujuma
Ni wachache wanaoweza Kusimamia mradi unaoingiza faida ya mabilioni serikalini
Huku yeye akiambulia milioni 3 Hadi 5 za ukurugenzi
Hili ni moja ya tatizo kubwa la watanzania na la Taifa wanamwona MTU ambaye sio mpigaji ni mjinga na wapigaji ni wajanja
Very bad mentality in our Nation
 
Umeandika pumba!!
 
Tayari watu wa Dubai washapewa Hilo dili.
Soma guardian la leo 27.3.24
 
Ni tatizo halafu wakitoka hapo wanaenda mpa biashara mwekezaji uchwara kwa income losses za serikali.

Sisi watanzania tunadhani huko ulaya ni rahisi tu watu wanapewa hizo PPP contracts.



Fanya upuuzi uone fines za serikali


Huku nako kuna malipo ya kutumia hizo njia line tu ya dar Arusha unaweza lipa £200m kama maintance costs. Kwa serikali bado una target za faida hiyo mikataba inataka labda kwa miaka 8 ulipe serikali £3.3 billion kuendesha hiyo line (hayo ni mapato baada ya kodi ambayo na kodi yenyewe unalipa), wafanyakazi wanachukuliwa kama waajiriwa wa serikali pension plan yao lazima ulipe serikali.

Hayo mambo ya PPP sio rahisi kama watanzania wanavyochukulia kuna fines za kuchelewesha huduma pia au under investments. Masharti yake ni balaa kujiingiza huko uwe na utaalamu kweli kweli wa hiyo biashara vinginevyo utajuta.

Tanzania tunadhani na wenyewe huko wanapewa tu sandakalawe kama serikali ya Tanzania inavyogawa mtu anatoa $500m anapewa sehemu kubwa ya bandari kwa miaka 30 dah wataacha kuigombea hiyo UDART kwa akili hizo. Ili kufanikisha hilo zoezi lao anatolewa mtu mwenye uelewa wa finance kama Kakoko wanaenda weka mkurugenzi ambae ukimsikiliza yule hata akili ya kuendesha duka kubwa hana iwe bandari.

Ndio maana wenye akili zao huko serikalini washajichokea wanaona bora liende tu.
 
Huko Chadema mnahitaji kupigwa msasa. Kuna kitu kinaitwa (PPP) yani Public - Private Partnership.
Chadema bado watoto wadogo sana kushika nchi they are still hopeless

Hawajapata watu sahihi.Wilbold Slaa na Lowasa na Sumaye walau walikuwa vizuri walijua mambo fulani lakini Chadema walishindwa kuwafuga hiyo mifugo kwenye zizi lao la mifugo

Hayo unayoongea kwa Chadema iliyobaki ni rocket science somo gumu kwao kuelewa
 
Wangetafuta foreigner aongez

umenena vema ni miaka 26 tokea mkapa aifungue nchi kwa kuleta waekezaji tuwe wa kweli hakuna cha maana walichofanya
Wawekezaji hawana shida. Viongozi wakiwa na uchungu na taifa lao,hata muwekezaji atawaheshimu.
BRT si ya jana tu. Anza na mshahara wa raia abaefanya kazi kwa mhindi.
Anakuja mhindi,anavikwa cheo cha supervisor,hata kinachofanyika mazingira hayo,hakijui. Mshahara wake, $15,000 na kuendelea. Mbongo,fundi wa mashine za kiwanda, yeye analipwa Tshs 300,000. Hii pesa,atapewa kwa mafungu,kwa mkono wa kushoto(wenye imani zao wanajua mana yake). Miaka 10 na zaidi anafanya kazi,lakini hata kodi tu,hapati. Achana na yeye kujenga. Mnyonge ananyongwa,na haki hapewi.
Ukiongea tu,unatukanwa Tunina
Ni hizo contracts,muwekezaji anaejielewa, akishajua nchi haina msimamo,haji. Bora Kim Jong Un. Hivi,inaingia akilini,mbunge alipwe na mambo mengine kwenye Milioni 25. Mwalimu wake,laki 2!!! Mwingine,anafia hospitli,kwa kukosa dawa.
Jirani analala njaa,watoto wake gata nguo hawana. Mbunge anaseleleka na na kodi za walala hoi. Vitu vingine ni aibu.
Muwekezaji mwingine,anafika ofisini,form 4 tena division 0, anampokea na earphones,akichat whatsapp,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…