Waasi wa M23 sasa waelekea mji wa Bukavu

Waasi wa M23 sasa waelekea mji wa Bukavu

Mpya Wakuu,

Kuna Documents zimekamatwa kwenye Kambi ya Jeshi la Kongo kumbe lengo lao lilikuwa ni kwenda moja kwa moja hadi Kigali.
Propaganda, victim playing..waende kigali na watu mmewavamia hapo walikua wametulia!
 
Sio violent for nothing sema ni watu wenye kupigania uhuru wao.

Angalia huko Kenya wameruhusiwa kubeba Silaha ili kulinda Mifugo yao.
Culture yao ya ufugaji ndiyo inafanya wawe violent. Na mara nyingine kuwa bullies. Tofauti na mkulima, mfugaji muda wote ni mtu mwenye mashaka na usalama wa mifugo yao. Anaweza kufanywa maskini ndani ya usiku mmoja tu. Pia na yeye anatakiwa awe tayari kuvamia kwenda kuiba mifugo. Jambo hili limewafanya kuwa violent. Sasa wakikutana na wakulima wapole wanawaonea na kuwatawala. Siyo kwamba wana akili au wanajua sana kutawala. Ni kwa sababu wakorofi.
 
Culture yao ya ufugaji ndiyo inafanya wawe violent. Na mara nyingine kuwa bullies. Tofauti na mkulima, mfugaji muda wote ni mtu mwenye mashaka na usalama wa mifugo yao. Anaweza kufanywa maskini ndani ya usiku mmoja tu. Pia na yeye anatakiwa awe tayari kuvamia kwenda kuiba mifugo. Jambo hili limewafanya kuwa violent. Sasa wakikutana na wakulima wapole wanawaonea na kuwatawala. Siyo kwamba wana akili au wanajua sana kutawala. Ni kwa sababu wakorofi.
Asante kwa majibu muruwa 🙏🏼
 
Kuna kitu nilikuwa sijui kumbe Wakiga wa Uganda na Kongo nao wana ethnicities za Tutsis na Hutu?!

Hili swala nilikuwa silijui kama usiku wa Giza aisee....
.
 
Habari njema ambazo ni nadra kuzikia kwenye huu mgogoro wa Mashariki mwa Kongo DRC, kuna habari kuwa sasa Wakimbizi waliokuwa wakiishi kwenye Makambi karibu na Mji wa Goma sasa wamerejea makwao UN inatakiwa ikawasiadie Amani imeshapatikana FLDR nao wamekimbilia msituni.
 
02 February 2025
Bukavu, Kivu ya Kusini
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

Naibu gavana wa Kivu ya Kusini Bw. Jean-Jacques Elakano Myewa azungumza mjini Baraka na raia wa jimbo la Kivu ya Kusini juu ya tishio la M23 (lugha ktk Video ni katika kiSwahili safi kwao mtazamaji)


View: https://m.youtube.com/watch?v=kJAvoyQ6ewA

Naibu gavana baada ya mapokezi mazito ikiwa ni mara yake ya kwanza kufika Tarawa ya Fizi mji wa Baraka katika mkoa wa Kivu ya Kusini atoa hotuba nzito kwa kiSwahili akiwa na ujumbe salamu za kutoka mji mkuu wa Jimbo hilo mji wa Bukavu na kusema yafuatayo ikiwemo tishio la M23 kuteka jimbo hilo


View: https://m.youtube.com/watch?v=JpQBFKbeVUQ
 
03 February 2025
Kisangani, DR Congo

Jean-Pierre Bemba atoa wito kwa vijana kuitetea ardhi takatifu ya Kongo

View: https://m.youtube.com/watch?v=NJvnh20bb5Q
Jean-Pierre Bemba baada ya kuhudumu kama Naibu Waziri Mkuu wa Ulinzi 2023 hadi 2024, alihamishwa hadi Naibu Waziri Mkuu wa Uchukuzi wa serikali ya rais Felix Tshisekedi ambayo sasa inatishiwa kuondolewa madarakani na kundi la M23
 
03 February 2025
Kisangani, DR Congo

Jean-Pierre Bemba atoa wito kwa vijana kuitetea ardhi takatifu ya Kongo

View: https://m.youtube.com/watch?v=NJvnh20bb5Q
Jean-Pierre Bemba baada ya kuhudumu kama Naibu Waziri Mkuu wa Ulinzi 2023 hadi 2024, alihamishwa hadi Naibu Waziri Mkuu wa Uchukuzi wa serikali ya rais Felix Tshisekedi ambayo sasa inatishiwa kuondolewa madarakani na kundi la M23

Huyu jamaa bado yupo? Wakongo wasikubali kufa ili wapiga mapesa kama hawa waendelee kula pesa.
 
4 February 2025
TUME ZA JESHI LA ULINZI LA RWANDA WATUMISHI WAPYA 531 WA OPERESHENI MAALUM | KIREHE, 30 JANUARI 2025


View: https://m.youtube.com/watch?v=fI1FhLkVAv8

Jeshi la Ulinzi la Rwanda (RDF) limehitimisha mafunzo ya askari 531 wa Kikosi Maalum cha Operesheni baada ya kumaliza miezi 11 ya mafunzo maalumu ya kivita katika Kituo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Nasho, Wilaya ya Kirehe.

Kundi la waliohitimu ni pamoja na Maafisa 46 na vyeo vingine 485. Sherehe ziliongozwa na Mkuu wa Majeshi wa Jeshi la Ulinzi la Rwanda Jenerali MK Mubarakh.


Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi wa RDF aliwapongeza wahitimu wapya waliopata mafunzo kwa kukamilisha kwa mafanikio kozi kali ya miezi 11 ya mafunzo maalum ya mapigano, wakionyesha uthabiti na kiapo chao wakati wote wa programu. Alibainisha kuwa ujuzi walioupa utaongeza ufanisi wao wa kiutendaji kwa kiasi kikubwa, akiwataka kutanguliza nidhamu kama thamani ya msingi ndani ya Jeshi la Ulinzi la Rwanda (RDF).

"Lazima uimarishe ari na ujuzi ulioonyesha wakati wa mafunzo wakati wowote unapoitwa kutetea uhuru wa nchi yetu.

Kuwa tayari kutekeleza misheni yoyote kama wafanyikazi wa Kikosi Maalum cha Operesheni." CDS iliwashukuru wakufunzi kwa kujitolea kwao katika kuwaendeleza askari wafunzwa kuwa askari wenye ujuzi walioandaliwa kwa ajili ya operesheni maalum

. Katika hafla hiyo, askari watatu bora walitambuliwa kwa mafanikio yao makubwa, huku Kapteni Sam Muzayirwa akitunukiwa tuzo ya mwanafunzi bora wa jumla. Luteni Moise Butati Gakwandi aliibuka wa pili, huku Nahemia Gakunde Kwibuka akipata nafasi ya tatu.

Katika kipindi cha miezi 11 ya Mafunzo Maalum ya Operesheni, washiriki walipewa ujuzi wa hali ya juu wa mbinu muhimu kwa ajili ya shughuli maalum, ikiwa ni pamoja na silaha nzito na ndogo, mapigano ya mkono kwa mkono, kuvuka mto na maji, usomaji wa ramani ya kijeshi, upelelezi, uhandisi wa mapigano, shughuli za upandaji mlima na helborne ( kuchupa toka helikopta), na huduma ya kwanza ya hali ya juu.

Ujuzi huu unalenga kuandaa vikosi vya RDF kutetea uadilifu wa eneo na kulinda uhuru wa kitaifa wa Rwanda.
Source : Jeshi la Ulinzi Rwanda
 
RAIA WA MAREKANI WASHAURIWA NA UBALOZI WA MAREKANI KINSHASA KUONDOKA

Mbali ya tangazo hilo kwa raia wake waliopo DR Congo pia ubalozi uliopo Kinshasa wachukua hatua kupunguza idadi ya wafanyakazi kwa kuwaondoa nchini Congo.

Ubalozi unawataka kuondoka kwa njia mbalimbali ikiwemo kutumia Mashirika ya ndege kwa kuwa uwanja wa Kimataita wa Ndege wa N’Djili bado unaendelea kufanya kazi kupokea ndege. Na pia ubalozi unasema kwa wale walio nje ya Kinshasa watumie njia za mipakani kuingia nchi jirani kwakuwa mipaka ya DR Congo bado ipo wazi haijafungwa.

Security Alert: Kinshasa, Democratic Republic of the Congo
By U.S. Embassy Kinshasa
5 MINUTE READ

February 3, 2025


Location: Kinshasa Democratic Republic of the Congo (DRC) 3 February 2025

Event: The U.S. Embassy in Kinshasa is further reducing the number of U.S. personnel working in the Embassy.
The Embassy advises U.S. citizens in the DRC to depart immediately via commercial means.

Due to the security situation in Kinshasa, the U.S. Embassy will not be conducting any visa interviews and will not be able to offer routine services for U.S. citizens.

Make sure that your and your family’s travel documents are in order and essential items are packed in bags that you can easily carry. We understand that border crossings remain open for transit and many flights are departing from N’Djili Airport in Kinshasa.
If you need emergency assistance, please contact the Consular Section at the phone numbers below.
Actions to Take:
  • Review your personal security plans and ensure your family has enough food and water should you need to stay home for several days.
  • Have essential items (clothing, medications, travel documents) packed in a bag that you can carry.
  • Have a personal emergency action plan that does not rely on U.S. government assistance.
  • Take advantage of commercial transportation options, should you wish to depart the area.
  • Avoid crowds and demonstrations.
  • Be aware of your surroundings.
  • Monitor local media for updates.
  • Keep a low profile.
Source : Ubalozi wa Marekani Kinshasa
 
Back
Top Bottom