Waasi wa M23 Wamedhibiti mji wa Bunagana uliopo Mpakani mwa DRC na Rwanda

Mkuu pia kumbuka nchi kupigana Vita vingi sio kwamba ndo wananguvu Sana kuliko wengine, kwa kweli Ni fact kusema kwamba wanapata uzoefu so wanaelewa njia mzjri za kushida Vita na Nini kitakufanya ushidwe vita.
Kumbuka marekani wapo kwenye Vita kwa miaka mingi Sana ila sinauwakika Kama Kuna vita wamewahi kushida kwa uwezo wao wenyewe wakiwa pekeao, kumbuka Iraq walikuwa UK, France na USA na ndo maana walishidwa na walitumia njia ya kumbana kiunchumi asiuze mafuta hakose pesa za siraha ndo wakampiga. Sasa ukija kwa South Korea Mara ya mwisho kupigana Ni 1959 kwenye vita vya Korea Kama sijakosea mwaka, ndo Vita hivyo to walivyopigana Sasa kwa sababu hip Unaweza kusema wapo weak kabisa coz wamepigana Vita kidogo.
Ukija kwa India wamepigana kashimir miaka ya 70 huko Sasa utasema coz yapita miaka zaidi ya 40 hawajapigna , sawa na japani wamepigana Vita vya 2 vya dunia Sina uhakika Kama Kuna vingine wamepigana tangu 1945, so kwa hio hawajapigana mda Sasa inamaana wapo weak. Sawa na south africa sijajua Vita wapigana na Nani. Sasa waweza kusema kuwa wote hao hawataweza Vita.
Kumbuka wamepigana mda mrefu Sana na Sasa dunia imepandilika mpaka kwenye technology ya kivita Ni bola kuliko zamani. Na kumbuka magenerali wa kipindi hicho hawapo kazini Sasa.

Mimi naamini jeshi kuwa imara Ni MAFUNZO hasa na UZALENDO pamoja na KUJITUMA kwa Askari.
Pia VIFAA vinasaidia Sana na wavijue kuvitumia kwa usahihi.
pia MBINU nzazo husaidia namoja na NIDHAMU. Uzoefu nao Ni muhimu pia.
zitto junior Proved
 
Kenya wana silaha nyingi za kisasa na training kali kuliko inavyodhaniwa na wabongo. Na hivi karibuni wamefanya mission ya kisasa kuliko JWTZ. Ukitazama hata maonesho yao ya mwezi huu unaona silaha mpya na relatively modern kuliko sisi.

Wana artillery, APC, tanks, MRAP na helicopters za kisasa na nyingi kuliko sisi
 
Msikilize Sultan Makenga hapa👇

hahahahha Sultan Makenga....No different whether is Makenga, Laurent Nkunda or Bosco they are all from next side past kivu and they have their own route aka free safe passage to home probably over weekend or when called for the meeting and instruction from big brother....

its the project, making DRC chaotic for our beneffit and your existance.....dont touch the dial, things will turn into you..

There is big reserve of oil in Virunga national Park, whatch out....

The Bad thing of DRC, the kinshasa top dogs dominate all the wealth of Katanga and area of congo river, Kisangani, No one cares for their homeland.....may be, the fifth generation will awake and fight for their homeland..
 
JAMANI wangapi njoo hapa maramoja wa kupuliza zitto junior T14 Armata Count Capone Proved

Vifaru ( battle tanks) kwa dunia ya Sasa kukiweka Frontline kwenye mapambano ya kivita Ni rahisi Sana kuaribia maana dunia ya Sasa imeendela Sana kwa technology kuna ant tanks missile ambayo Ni rahisi Sana kuiaribu kifaru, askri wa urusi nchini Ukraine wengi wamekufa kwenye vifaru maana wamepoteza tanks 460+ , nimekumbuka pia uturuki kule Syria na vifaru vya Aina ya leopard kutoka ugerumani ambavyo vinasifia Sana kuwa Ni bola vingi biriaribia kule adi ugerumani wakashangaa.
Hii imekaaje kwenu wadau.
 
Story yako inatufudisha kitu,ila amini mkuu hao m23 hizo vurugu zote siku akiondoka kagame in power ndio zitakua mwisho na watakua wacongo watiifu kabisa kwenye nchi yao
 
Tank kuwa mzuri kwa Sasa wansema lazima uwe na system itakayo haribu missile KITU ambacho Ni ndumu kuwa nayo wachache wamejalibu jaribu ila sio Sana ipo hi ya Israel wanasema Ni mzuri kidogo.
 
Askari wa DRC hawana nidhamu hivyo kuifanya Kongo kuwa na jeshi dhaifu sawa na Nigeria ambalo ni taifa lenye nguvu kifedha lkn jeshi dhaifu sana kutokana na matabaka yao.
 
Kwa hiyo DRC wote na nchi za Afrika mashariki ni wajinga kasoro wewe?
 

unajua chochote kuhusu banyamulenge waliomsaidia Kabira kuingia madarakani...

Unafahamu chochote baada ya vita walipotakiwa kurudi kwao nini walifanya maeneo ya Kivu...?...

Unajua chochote juu ya bodiguard Rashidi na Kifo cha Kabira Senior..?..
Unajua chochote juu ya kabira Junior..

Unafahamu chochote kuhusu Lairent Nkunda, Sultan Makenga na Bosco Ntaganda? unafahamu historia zao?....
 
Haya mambo ya Bahima empire conspiracy or sijui Kivu agenda ni upuuzi kwa wale wasiolewa au wakabila na hakuna kitu kama hicho ndio maana huoni SADCC au Africa Kusini maana wanajua kinachoendelea, interest ya Rwanda ni FDLR (wahutu wenye siasa kali waliokimbilia Congo baada ya kushindwa vita) wamepiga kambi Congo kwa nia ya kuvamia Rwanda na kibaya wameenda na ideology yao ya genocide kuua watusi wa Congo (Banyamulenge) na ndio maana M23 ambao ni Banyamulenge nao wako vitani maana stupid Congolese wanafikiri Banyamulenge sio raia wa Congo, kitu kingine utajiri wa Congo kama shamba la bibi kuna makundi yapo pale kwa interest ya huo utajiri tuu na wanajua kama kuna amani pesa haitakuwepo tena, mnasikia M23 tuu lakini kuna makundi zaidi ya 20 yanapigana ndani ya Congo, Rwanda inatumika tuu na media kuonyesha chaos lakini really players wako huko wamejichimbia na majeshi yao migodini na wana mpaka viwanja vya ndege wanachimba na kubeba madini kila siku, na viongozi wengi sana wa Congo wanafaidika na hii chaos na hawataki iishe
 
Ukweli mchungu* RWANDA ni nchi ndogo yenye makeke sana .RWANDA inatamani kuwa taifa kubwa na lenye ushawishi kuliko mataifa yote EA . Kwa maana hiyo wanajijenga sana kwa kuwa na silaha za kisasa na kujikita katika technolojia na mafunzo ya ujasusi.

Kauli ya siku za karibuni kutoka kwa Kagame-Alisema yeye ni mdogo kwa maana ya eneo kijiografia ila ukimchokoza hutagusa ardhi yake vita itapiganwa kwako na ana vifaa na vijana wa kufanya hiyo kazi.Hofu na udhaifu wa Kagame ni kwamba kijamii imegawanyika hivyo ni rahisi kushindwa vita . Hutu vs Tutsi.

Mojawapo ya mafanikio ya kijeshi ya RWANDA ni kuweza kuwakabili magaidi waliokuwa wametamba msumbiji
 
Tanzania haitoi vitu hadharani. Tutakuonesha SMG na SAR tu . Utajua mwenyewe ukija
 
Tanzania haitoi vitu hadharani. Tutakuonesha SMG na SAR tu . Utajua mwenyewe ukija
Wewe na nani. Unajuaje kwamba sijui silaha zilizopo Tanzania? Silaha sio maparachichi kwamba utayaficha kwenye gunia. Russia, Ukraine, Syria, China, US wajulikane wana silaha gani wewe hapa nchi inayojengewa vyoo na IMF usijulikane?
 
Huwezi achana na vifaru kwa namna yoyote ile. Hilo suala nimelieleza kwenye uzi live wa Ukraine, kila silaha ina silaha dhidi yake na sifa ya silaha ambayo ni anti-XXX lazima iwe ya gharama ndogo na rahisi kuliko inachoenda kuharibu, huwezi mchinja ng'ombe ili umlishe nguruwe.

Leopalds zilizoharibiwa kule Syria ni version ya zamani ambayo siyo modification. Na kifaru siku zote kinaenda na infantry, sio kama Urusi mwanzoni walivyoingia Kyiv na misururu ya vifaru vikiwa peke yake. Nilieleza mara nyingi kwenye uzi ule, lazima ufanye reconnaissance kujua nguvu za adui, lazima uwe na infantry na air cover, lazima uwe na artillery protection na command & control ya uhakika kufanya response ya attack itakayotokea kwa ghafla, lazima ufanye mine clearing kwenye path utakayopitisha vifaru. Na mambo mengine

Vifaru vinatoa firepower ya karibu kwa infantry, vinalinda vehicles nyingine ambazo hazina protection kubwa mfano IFV, APC na MRAPS, vinaondoa pockets za adui na fortifications. Huwezi kutumia mortar, howitzer au artillery kufidia tank ukaweza. Hivyo vyote vinahitaji call labda mortar ndogo ambazo hazina madhara makubwa sana: call for artillery strike, toa coordinates, subiri ruhusa ya kushambulia, jipange. Wakati kifaru kipo hapo na crew yake yumo tank commander anafanya maamuzi hapohapo na kifaru kipo accurate kuliko.

Rheinmetall watengenezaji wa Leopald 2 wamezindua prototype mpya ya MBT mjini Paris kwenye maonesho ya silaha juzi Jumatatu. Wakati huo UK ambao Challenger 2 yao imechoka wanataka ushirikiano na Ujerumani kutengeneza new MBT. Russia yuko na T-14 Armata hafanyi mass production, Uturuki yuko na Altay anahangaika nayo. Hivi vyote vinakuja na bado new protection systems are in development. Israel wana active protection system ya Trophy, Russia ana Shtora na Arena, na armour mpya zinaundwa. Vifaru tunavyo bado
 
unajua chochote kuhusu banyamulenge waliomsaidia Kabira kuingia madarakani...
Hawa walitumiwa tu na serikali ya Rwanda.
Rwanda ilikuwa na interest yakumuondoa Mobutu sababu alikuwa akisaidia waasi wa Rwanda.
Rwanda ilitumia wanyamurenge ambao ni wacongo ilikuepuka kelele za international community.
Ilikuwa rahisi kuwatumia wanyamurenge kwasababu walikuwa na shida zao na serikali kwa miaka.
Unafahamu chochote baada ya vita walipotakiwa kurudi kwao nini walifanya maeneo ya Kivu...?...
Kwao wapi tena? Hawa niwa Congo kama nilivyotaja.
Infact hawa wanyamurenge walikuja kupata shida kubwa baada ya Kabira kufukuza majeshi ya Rwanda.
Wanajeshi wa Rwanda warirudi lakini hawa wanyamurenge hawakuwa nasehemu yakwenda walibaki Congo,
Kilichotokea nikuanza kuuawa na majeshi ya Kabira.
Unajua chochote juu ya bodiguard Rashidi na Kifo cha Kabira Senior..?..
Unajua chochote juu ya kabira Junior..

Unafahamu chochote kuhusu Lairent Nkunda, Sultan Makenga na Bosco Ntaganda? unafahamu historia zao?....
Laurent Nkunda, Makenga na Ntaganda ninachojua nikwamba hawa wote niwa Congo.
Haijalishi wamezaliwa wapi lakini asili yao ni wa Congo.
Nkunda amefungiwa Rwanda,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…