JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Kamishna wa Bima Tanzania, Dkt. Baghayo Saqware amesema ndege ya Precision Air iliyopata ajali ilikuwa na bima na kwamba fidia kwa shirika ni zaidi ya Dola Milioni 50 (Tsh. Bilioni 116)
Amesema bima ya ndege hiyo ni halali na ilikatwa kutoka kwa wakala wa ndani nan je ya Nchi ambapo waathirika wanaweza kupata fidia ya Dola Milioni 170 (Tsh. Bilioni 396).
Kamishna amesema hayo Dodoma, Novemba 10, 2022 wakati wa Semina ya Wabunge kuhusu usalama barabarani ambapo amesisitiza kuwa waathirika wa ajali hiyo ya ndege watalipwa fidia haraka iwezekanavyo.
Pia soma:
Bukoba: Ndege ya Precision Air yapata ajali Ziwa Victoria, watu 19 wafariki dunia