Wababa mliotelekeza watoto subirini mpaka mtafutwe na watoto wenu, acheni usumbufu!

Ni kweli Kabisa.
Lakini kitu ambacho watoto wanacholalamika ni ukaribu na upendo WA mzazi,
Yaani usipompa mtoto hayo mambo umekwisha.
Angewekewa ukaribu, inawezekana angebweteka na asingekuwa alivyo leo
 
Sio kweli.

Watoto wengi waliotelekezwa huja kwa kusudi maalumu, ni Kama unavyomuona Yesu wa Nazareth.
Ukiwakumbatia hao wa nje, hawatafanikiwa kama inavyotakiwa, kwa sababu utakuwa unafukuza baraka za kufanikiwa kwao
 
Watoto wanaakili Wewe!
Usifikiri hawajui kile wanachokiona
Wanawake ndio wanamezesha sumu. Mtoto wangu wa kwanza mama yake anampa sumu sana kuhusu mimi wakati huwa namtafuta kwenda kumjulia hali na hela natoa ila mama sababu tuna ugomvi anaihamisha hadi kwa mtoto.

Nami kwa jeuri hata akinikataa huko mbele ni poa tu.
 
Hio situation ipo na kwangu,nimeamua kutulia na mwisho wa siku nimemwambia huyo mwanamke acha mm nibaki baba jina
 
Na sisi tuliolea watoto wa wanaume wenzetu kisha wakatukimbia baada ya kufanikiwa, wakawatafuta baba zao halisi, unatushauri nini?
 
Hizi mambo zimewahi kunikuta nikiwa mdogo,baada ya kuachana wazazi,mama yangu hakutaka msaada wowote ule wa baba,ilifikia hatua hata mshua akileta nguo alizichoma moto,baadae mshua akaamua kukaa pembeni na kutojihusisha na kutoa matunzo yoyote yale kwangu,ulipofika umri wa shule alinipa majina ya baba wa kambo aliyemuoa wakati huo,nilisoma mpaka chuo kikuu nikitumia hayo majina,nimebahtika kupata ajira,sasa nikipata kidgo namtumia biological father,hiyo hali ya kumtumia pesa baba yangu mzazi,mama yangu imekuwa inamkera mno ni vile tu nimekuwa mtu mzima anashindwa kunikemea au kunipangia ila anaumia sana! So wakati mwengine mama zetu huchangia hiyo hali,ndo maana mimi siwezi kutupa lawama kwa baba yake dimpoz,hatujui huko walikuwaje na mzazi mwenzake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…