Ndo maana nikakwambia kwenye hizi issue za watoto kutelekezwa na baba zao,sio wote wametelekezwa sometimes wazazi wa kike huchangia hizo mambo,japo kuna wengine wanatelekezwa kweli,kuna mama mwengine kwa sababu mapenzi yameisha na mzazi mwenzie basi vita anaileta kwa mtoto, anashindwa kujua tofauti zenu Kama wazazi mtoto hazimuhusu,Kuna siku moja nikiwa kazini yalikuja malalamiko kuwa mama analalamika ametelekezwa na mwanaume,hatoi huduma kwa mtoto wala kwake,ikabidi tumtumie summons yule mwanaume,kweli alifika kwenye shauli,katika maelezo yake alidai kuwa mzazi mwenzie walishatengana miaka miwili iliyopita,na kila mwezi amekuwa akitoa kiasi cha fedha 100,000 kwa ajili ya mtoto,na mtoto alimkatia bima ya afya akiwa na miezi miwili,ila alisema amesitisha kutoa hizo pesa miezi kadhaa nyuma kama mitatu kwa sababu, mzazi mwenzie alidai ametelekezwa na mwanaume! Kumbe si kweli, hivyo alipata hasira akaamua kutotoa hizo pesa kwa miezi hiyo mitatu.kwa hiyo ndugu yangu haya mambo ya matunzo ni mtambuka sana,Kuna wanawake wengine kweli wanatelekezwa since anapomwambia mwanaume nina mimba yako,na uhusiano unaishia hapo,na mwanaume hawajibiki tena kwa huyo mwanamke na mimba yake.