Mkuu hapa hatumchambui ommy tu,tunaichambua jamii kwa ujumla,na kuhusu faulo unayozungumzia ni mapenzi tu,wanawake wengi huamini kuwa wakipewa mimba na mwanaume basi lazima aolewe na huyo Mwanaume,sasa ikitokea tofauti ndo hizo chuki huanzia hapo,sasa wengi wakienda huko ustawi wa jamii au mahakamani,huishiwa kuambiwa kuwa hawawezi kumlazimisha mwanaume amuoe kwa sababu amezaa naye,ila wanachoweza kumsaidia ni kupata matunzo ya mtoto, issue ya ndoa ni ya hiali baina yao wawili! Kama mmoja hamtaki mwenzie huwezi lazimisha wawe pamoja,isipokuwa ni kuangalia maslahi ya mtoto tu kwenye matunzo.